Email address Shafii.ismail09@gmail.com
WhatsApp /call 0683308173
Website http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com
YouTube channel https://www.youtube.com/@sharphy_Ismaily
PILIPILI HOHO
Zao la pilipili Hoho ni zao lisilo na msimu maalumu, ni zao lisiloyumba saana soko lake na ni moja ya zao la mbogamboga linalotumiwa zaidi Tanzania baada ya zao la Nyanya na kitunguu maji.
Mkulima akiamuwa kulima zao hili la pilipili hoho kitaalamu zaidi kwa kuchaguwa mbegu bora na kufuata Kanuni bora zaidi za Agronomia bhasi ni zao lisilomuangusha mkulima abadani.
Kwani Mkulima anauwezo wa kuhudumia na kuendelea kuvuna zao la pilipili hoho kwa muda mrefu zaidi.
AINA YA MBEGU ZA PILIPILI HOHO ZA KIJANI (GREEN PEPPER)
Mbegu za pilipili hoho zinazo patikana Tanzania ni;
Calfornia wonder
Yolo wonder
MBEGU BORA ZA HOHO, NYANYA, TIKITI, VITUNGUU N.K
MBEGU BORA ZAIDI KIBIASHARA NI:
CONTINENTAL SUPER BELL F1
INDRA F1
HERCULES F1
PLATO F1
Hizi ni mbegu zenye kurefuka na zenye uwezo wa kuzaa matunda makubwa pia uwezo wa kuendelea kuzaa kwa muda mrefu zaidi.
Super Bell F1
UCHAGUZI WA ENEO
Ni vyema eneo litakalotumika katika kilimo cha pilipili hoho liwe na rutba na upatikanaji rahisi wa wa maji wa uhakika.
Chaguwa shamba lisilo na historia ya ugonjwa wa mnyauko kabla ya kupanda zao la pilipili hoho au pima udongo wako kabla.
MAHITAJI YA KIIKOLOJIA
Pilipili hoho hustawi katika maeneo yenye hali joto tofauti kuanzia nyuzi joto za sentigredi 16 mpaka 28⁰C lakini hustawi vizuri zaidi katika maeneo yenye joto la nyuzi za sentigredi 25 mpaka 30⁰C.
UDONGO
Pilipili hoho hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba, usiotuamisha maji na wenye uwezo wa kuifadhi maji vizuri.
Udongo wenye tindikali nyingi huzorotesha ukuaji wa pilipili hoho hivyo udongo mzuri kwa pilipili hoho ni ule wenye tindikali kati ya Ph 6.0 – 6.8.
KUANDAA SHAMBA
Muda wa Kuandaa
Kwa kilimo cha kutegemea Mvuwa Shamba la pilipili hoho liandaliwe mapema mwezi mmoja kabla ya kupandikiza miche shambani kabla ya kuanza kwa mvua za masika.
KUPANDA
NAFASI YA KUPANDIA
Kabla ya kupima matuta ni muhimu pia kujua nafasi ya kupandia utakayo tumia ili kupata ukubwa sahihi wa kila tuta. Kwa mfano kwa nafasi ya kupandia ya sm 60 × sm 40 kwa matuta makubwa unaweza kutengeneza kila tuta katika upana wa mita 1.2 na urefu wowote. Acha nafasi ya m 1 kuzunguka shamba na njia kila baada ya tuta upana wa sm 50.
UPANDAJI KATIKA MATUTA
Inashauliwa kupanda pilipili hoho katika matuta ili kusaidia mizizi kukua vizuri na udongo kuhifadhi maji. Wakati wa kiangazi, tengeneza matuta yaliyodidimia kidogo ili kufanya maji yaweze kukaa kwenye udongo na wakati wa masika matuta yainuliwe kidogo toka kwenye usawa wa ardhi ili kuzuia maji yasituame. Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili na matuta madogo hupandwa mstari mmoja. Tengeneza matuta kwa kufuata alama zilizowekwa wakati wa kupima shamba.
Shamba la pilipili Hoho baada ya kupandikizwa
KUSIA MBEGU
Sia mbegu za pilipili hoho kitaluni au katika trays ambapo miche huoteshwa na kutunzwa siku 21 hadi 40 kabla ya kupandikizwa shambani.
Kwa wanaotegemea Mvuwa; Kitalu kiandaliwe mapema kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua. Hakikisha unafuata taratibu zote za uandaaji na utunzaji wa miche kitaluni.
Miche ya pilipili hoho katika tray: Namna ya uhakika ya kuotesha miche
KIASI CHA MBEGU KWA EKARI
Kulingana na kampuni ya mbegu ya seminis na continental kiasi cha gramu 125 za mbegu za pilipili hoho kinatosoha kupanda eneo la ekari moja ambalo huchukua miche karibu 11,000 hadi 15,000.
Gram 125 za super bell F1 zinatosha kuotesha ekari moja
KUPANDIKIZA
Tabia za miche ya kupandikizwa
Mche uliopandikizwa
Miche ya pilipili hoho inayofaa kupandikizwa shambani ni ile yenye afya na yenye kimo cha sm 10 hadi 15 ikiwa na majani halisi matano mpaka sita.
Pandikiza miche wakati wa jioni ili iweze kupona kwa urahisi na kuzoea hali ya shambani bila ya kupata mshtuko.
Nafasi ya kupandia
Miche ipandikizwe kwa kuzingatia nafasi pendekezwa katika mistari iliyonyooka. Pilipili hoho kutegemeana na aina huweza kupandwa katika nafasi tofauti tofauti sm 60 mpaka sm 75 mstari hadi mstari na sm 30 mpaka sm 45 shimo hadi shimo. Ni muhimu kusoma pakiti ya mbegu husika kujua nafasi pendekezwa kabla ya kuchagua nafasi ya kutumia.
Picha yenye ukungu ikionesha mimea ya pilipili hoho Shambani
Hatua za Kupandikiza
Unaweza kupandikiza miche shambani kwa kufuata hatua zifuatazo;
Mwagilia maji mengi shambani na kitaluni masaa 12 hadi 24 kabla ya kupandikiza ili kulainisha udongo kurahisisha upandikizaji.
Waweza mwagia shamba jioni ukapandikiza asubuhi ya kesho yake.
Chimba mashimo ya kupandia yenye kina cha sm 7 katika nafasi iliyopendekeźwa hapo awali.
Weka viganja viwili vya mkono vya samadi iliyoiva katika shimo la kupandia kisha changanya na udongo kupata mchanganyiko mzuri.
KUPANDIKIZA
Hamisha miche kwa kutifua kwa kutumia umma wa shambani kisha pandikiza miche ikiwa na udongo wake katika mashimo ya kupandia kisha fukia kwa udongo ulio pembeni.
Mche uliotayari kupandikizwa
MATUMIZI YA MBOLEA NA VIUATILIFU KATIKA KILIMO CHA PILIPILI HOHO.
WIKI YA 1-2 BAADA YA KUPANDIKIZA
Mbolea: weka mbolea ya DAP, Yara mila winner, au Yaramila otesha 50 kg kwa ekari kuchochea ukuaji wa mizizi na ustawi wa zao shambani.
Kudhibiti magonjwa ya ukungu/barafu: pulizia sumu ya Ridomil, Ivory 72, Ebony 72, Innovex , Xantho au Fungiwill kukinga au kutibu magonjwa yote ya ukungu/kuvu shambani kama vile kata kiuno, bakajani wahi, bakajani chelewa, ubwiru chini, ubwiru unga.
Kumbuka: pulizia madawa ya ukungu kila baada ya wiki 1-2 kuepusha ueneaji wa magonjwa shambani.
Kudhibiti wadudu waharibifu:pulizia sumu ya dudumectin, Duduacelamectin, Snowmectin, snowplus, wilcron au duduwill kudhibiti jamii yote ya wadudu waharibifu, kama vile Vithiripi, vimamba, vipepeo weupe, leaf minner, vimamba n.k
WIKI YA 3-4 BAADA YA KUPANDIKIZA
Mbolea: weka mbolea ya kukuuzia kama vile NPK, Yara mila winner, UREA, n.k 50 kg/ekari ili kustawisha mmea Zaidi shambani.
Kumbuka kupiga sumu ya ukungu kila baaada ya wiki 1-2 na kupiga dawa ya wadudu waharibifu shambani kwa afya nzuri ya mmea.
MAUWA YAKIANZA KUSHAMIRI
Mbolea; weka mbolea ya CAN, yaraliva nitrabor au yaraliva calcinity 50 kg/ekari
Pulizia sumu ya wadudu na Kuvu kudhibiti magonjwa na wadudu wengine wote waharibifu.
SOMA: MUONGOZO MFUPI KILIMO CHA VITUNGUU MAJI
MATUNDA YAKISHA TOKA
Mbolea: weka mbolea ya CAN au yaraliva nitrabor changanya na NPK/ yaramila winner/CAN/ UREA kujenga tunda la hoho lenye Afya, umbo kubwa na kuongeza maisha rufani baada ya kuvunwa.
BAADA YA MICHUMO MIWILI MIWILI
Mbolea: weka mbolea ya CAN au yaraliva nitrabor changanya na NPK/ yaramila winner/CAN/ UREA kuongeza uzakishaji zaidi na kujenga tunda la hoho lenye Afya, umbo kubwa na kuongeza maisha rufani baada ya kuvunwa.
Aina nzuri ya pilipili hoho kwa muda wa mavuno
KUMBUKA: Pulizia Sumu za wadudu mara uonapo dalili ya mavamizi
Pia pulizia sumu ya kukinga kuvu au ukungu kila baada ya siku 7 hadi 14 kutegemea na Hali ya hewa
0 comments: