Friday, 9 June 2023

Kilimo cha bilinganya

Email address Shafii.ismail09@gmail.com 

WhatsApp /call 0683308173 

Website http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

MADA. BILINGANYA

 

KILIMO CHA ZAO LA BILINGANYA

Historia ya zao la Bilinganya
Zao hili asili yake ni sehemu za nchi ya India nchi inayo ongoza dunia kwa kilimo cha Bilinganya ni uchina hasa katika pwani za kusini mwa china inayo lima asilima 59% duniani ikifuatiwa na India Uturuki,Misri Irani na Italy.
Masoko ya zao.
Zao hili ni zao lililo na masoko ya Nje na ndani kama ilivyo katika utangulizi hulimwa kwa wingi Uchina lakini lina masoko Ulaya na ,Marekani na hata katika masoko ya ndani halina ushindani mkubwa katika masoko ya ndani kama ilivyo mazao ya bustani kama nyanya.
Matumizi
Ni zao linalotumika kama mboga au kiungo cha Mboga peke yake au kuchanganywa na mboga zingine
 MAHITAJI YA ZAO KATIKA UZALISHAJI
Hali ya Hewa
Zao hili huhitaji haliyahewa ya joto huweza pia kulimwa si chini ya nyuzi 10*c lakini hustawi vizuri katika nyuzi 26*c hadi 29* c
Udongo
.Japo zao hili lina mea vizuri kwenye kila aina ya udongo hukuwa na kustawi vema katika udongo tifutifu usio twamisha maji.Udongo ulio katuliwa vizuri huwezesha mizizi kumea vizuri katika  urefu wa mm 600.Hivyo ni mhimu kuliandaa shamba lako vizur kabla ya kupanda
Miezi mizuri inayoshauriwa katika kilimo hiki ni miezi isiyokuwa na Mvua nyingi kwa kuwa kukiwa na unyenyevu mwingi zao hili huwa halitoi mazao ya kutosha na pia kwenye ukame kusipokuwa na maji ya kutosha huwa halitoi mazao mengi ya kutosha  na Inasemekana kutokana na sifa hizi huwenda ndiyo husababisha kutokuwa na Mafuriko mengi ya zao hili.
Uoteshaji wa Mbegu
Mbegu huweza kuoteshwa kwenye vitalu au kupanda moja kwa moja kwenye mashimo na baadae kupinguzia umbali wa 1.8 hadi 2.5 mita mche hadi mche kulingana na rutuba ya udongo miche 10000 huweza kupandwa kwenye ekari moja.

0 comments: