Email Shafii.ismail09@gmail.com
WhatsApp /call 0683308173
USITUMIE MAZIWA KAMA UMEADHIRIWA NA SUMU ZA VIUATILIFU
maziwa yanaipa nguvu sumu itokanayo na viuatilifu kushambulia seli za mwili wa mwanadamu. Utafiti kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu nchini Tanzania (TPHPA), walisema viuatilifu vinapenda kusafiri katika sehemu zenye mafuta kwenye mwili wa mwanadamu.
Kwa kuwa maziwa yana mafuta, inakuwa rahisi kwa viuatilifu kushambulia seli za mwili kupitia katika mafuta kwenda kwenye damu. WAlitoa onyo walipowasilisha matokeo ya utafiti wa athari za matumizi holela ya viuatilifu katika mbogamboga na matunda.
wakulima wanapoathiriwa na sumu hiyo, kitu cha kwanza wanatakiwa kuwekwa katika sehemu ya wazi yenye upepo wa kutosha kisha kuchukua mkaa na kuusaga na kuuchanganya na maji na kumpa mwathiriwa anywe huku taratibu za kumpeleka hospitali zikiendelea.
“Madhara ya viuatilifu yanatofautiana, kuna ya papo kwa hapo halafu kuna madhara ya muda mrefu, madhara ya papo kwa hapo anayopata mkulima kwanza anatakiwa kuondoka katika mazingira ya viuatilifu, kama imemwagikiwa anapaswa kuoga kwa maji yanayotiririka muda huo huo,”
ikiwa mkulima ameathiriwa na kiuatilifu kupitia mdomoni au katika mfumo wa hewa, kitu cha kwanza anatakiwa kuchukuliwa haraka na kuwekwa katika sehemu ya wazi yenye upepo wa kutosha na kunyweshwa mkaa uliopondwapondwa na kukorogwa na maji.
Wakati hayo yakiendelea, utaratibu wa kumpeleka hospitali ufanyike huku chombo cha kiuatilifu kilichomdhuru kikipelekwa pia kwa daktari ili kumfanya atambue aina ya kiuatilifu na matibabu stahiki kwa haraka.
“Sumu za viuatilifu haziondolewi kwa kunywa maziwa kama ilivyozoeleka kwa mtu aliyeathiriwa na dawa, mwathiriwa anatakiwa akorogewe mkaa na apewe anywe lakini si maziwa,”
kwa watu wanaotumia viuatilifu katika sehemu mbalimbali wanapomaliza kunyunyiza hata kama hawakuathiriwa, wasipendelee kunywa maziwa badala yake wanywe maji kwa sababu ikiwa kuna kiuatilifu kilichojipenyeza mdomoni maziwa yatahatarisha maisha yake.
http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com
0 comments: