Tuesday, 27 June 2023

KILIMO CHA KARANGA

 


 

Email Shafii.ismail09@gmail.com 

Website http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

WhatsApp /call 0683308173 

T

YouTube channel https://www.youtube.com/@sharphy_Ismaily

KILIMO BORA CHA KARANGA​


Utangulizi

Karanga ni mojawapo ya mazao yanayotoa mafuta. Katika Tanzania zao hili hustawi zaid katika mikoa ya Kusini Mashariki, Dodoma na Morogoro. Pamoja na kutoa mafuta vile vile zao hutumika kwa njia nyingine mbali mbali, nazo ni pamoja na: Chakula cha wanyama / mifugo (Mashudu na majani), kurutubisha ardhi na chakula cha binadamu: kutafuna na kuunga kwenye mboga/chakula (Confectionary)


Kwa ujumla zao hili hutumika na wakulima kama zao la biashara.


Hali ya Hewa

Karanga hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye miinuko chini ya mita 1500 toka usawa wa bahari katika Tanzania, na hustawi zaidi katika maeneo ambayo yanapata mvua za wastani wa mm 750 hadi mm 1200 kwa mwaka.

Vile vile karanga hustawi vizuri kwenye udongo wa kichanga, inashauriwa kutopanda karanga kwenye udongo mzito (mfinyanzi) hii ni kutokana na sababu kwamba, karanga hazistawi kwenye sehemu zinazo simama maji, na udongo mzito huleta hasara wakati wa uvunaji.


Mbegu Bora Za Karanga

Kuna mbegu nyingi za karanga lakini zilizotangazwa hivi karibuni na zinazofanya vizuri zaidi ni hizi zifuatazo:

Pendo 2009

Naliendele 2009

Mangaka 2009

Mnanje 2009

Masasi

Nachingwea 2009

Soma hapa aina mpya za mbegu zilizotangazwa


Utayarishaji Wa Shamba

Shamba litayarishwe vizuri kuwezesha udongo kupenyesha maji na mizizi kirahisi. Karanga hupandwa kwenye matuta au sensa.


Utayarishaji Wa Mbegu

Karanga ambazo zinakusudiwa kwa mbegu zitunzwe na maganda yake bila kubanguliwa. Zibanguliwe karibu na msimu wa kupanda na kuchaguliwa. Baada ya kuchaguliwa zitiwe dawa, aina ya Fernasan D, Katika uwiano wa gramu 28 za dawa kwa kila kilo 10 za mbegu safi.



Upandaji Wa Karanga

Wakati wa kupanda: Uamuzi wa kuchagua wakati mzuri wa kupanda ni ule utakaoliwezesha zao hilo kukomaa wakati wa mvua za mwisho. Kuchelewa kupanda, hupunguza mavuno. Ni muhimu kuchagua aina ya mbegu ambazo uvunaji wake unafanana na mazingiza ya eneo hilo kihali ya hewa.


Kwa mikoa ya Kusini: karanga za muda wa kati na mrefu (Johari, Red Mwitunde) zipandwe kuanzia katikati, hadi mwishoni mwa mwezi Desemba. Karanga za muda mfupi (Spanish na Valencia) zipandwe kuanzia mwishoni mwa mwezi Desemba hadi katikati ya mwezi Januari.

Kwa mikoa ya mashariki na sehemu za mkoa wa Dodoma: karanga zipandwe mapema mwanzoni mwa mvua ndefu (Februari / March).


Nafasi Kati Ya Mimea

Inashauriwa kupanda karanga katika mistari. Nafasi kati ya mistari ni sentimita 50, na kati ya mimea ni sentimita 15 kwa karanga zinazotambaa (Virginia Spreading types). Kama karanga zinapandwa kwenye matuta ya sentimita 90, zipandwe mistari miwili, kila tuta. Kwa nafasi hii kiasi cha kil 60-75 za mbegu hutumika kwa hekta moja.


Kwa karanga zilizopo kwenye kundi la Spanish/Valencia (zisizotambaa), nafasi kati ya mistari ni sentimita 50, na kati ya mimea ni sentimita 10. Endapo karanga zimepandwa kwenye matuta ya sentimita 90, panda mistari miwili, inayofanya nafasi sawa na sentimita 50 kwa sentimita 10. Kiasi cha kilo 80-100 za mbegu hutumika kwa hekta moja kwa kutumia nafasi hii. Ambapo ni sawa sawa na kilo 32 hadi 40 kwa ekari.


Kwa aina zote za mbegu, panda mbegu moja safi, katika kila shimo.


Mahitaji Ya Mbolea Ya Karanga

Kufuatana na majaribio yaliyofanyika imeonekana kuwa karanga hustawi vizuri chini ya viwango vidogo vya phosphorus. Vyanza vya kirutubisho cha Phosphorus ni mbolea za kupandia nazo ni kama TSP, SSP na DAP. Mbolea hizi zote ziwekwe kabla ya kupanda au wakati wa kupanda lakini umakini unahitajika kutoruhusu mbolea kugusana na mbegu. Kiasi cha Kilo 90 za Phosphorus (= mifuko minne ya DAP) kinatosha kwa hekta moja ambayo ni sawa sawa na kilo 35 (= mfuko mmoja na nusu wa DAP) kwa ekari.


Vile vile katika sehemu nyingine, karanga zimefanya vizuri kwa kutumia samadi. Ubadilishaji wa mazao (Crop Rotation) husaidia kutunza rutuba, hivyo kupunguza kiasi cha mbolea kinachotumika. Karanga zinaweza kulimwa baada ya mahindi, ili kutumia masalia ya mbolea.



Upaliliaji

Karanga zipaliliwe zikiwa changa. Shamba lililotayarishwa vizuri na kuondolewa magugu ya muda mrefu (Perrenial weeds) linaweza kupalliwa mara moja, kwa sababu karanga hukua haraka, na zinaweza kushindana na magugu. Baada ya kutoa maua, karanga zisipaliliwe, hii inaweza kuharibu ‘pegs’, hatimaye kupunguza mavuno.


Magonjwa Na Wadudu Waharibifu Wa Karanga

Magonjwa Hatari Ya Karanga

(i) Ugonjwa wa kuoza (Aflatoxin)

Katika hali ya unyevu mwingi vimelea viitwavyo Aspegilus flavus huota ndani ya maganda na kushambulia mbegu za karanga. Vimelea hivyo hutoa kemikali ambayo ni sumu.


Kuzuia

Hakikisha kuwa karanga haziharibiwi wakati wa kuchimba.

Hakikisha karanga zinakaushwa vizuri (Unyevu wa 10%) kabla ya kuzitunza zitumike kama mbegu

Karanga za kupanda zitiwe dawa aina ya Fernasan-D.



(ii) Ugonjwa wa Madoa na Kutu (Cercospora Leaf Spots and Rust)

Magonjwa haya husababisha madoa ya rangi ya kikahawia hadi meusi kwenye majani. Vimelea vinavyosababisha magonjwa haya viko vya aina tatu:

Cersospora arachidicola. Husababisha Early Leaf Spot.

Phaeoisariopsis personata. Husababisha Late Leaf spot. Ugonjwa wa Early Leaf Spot hutangulia kuonekana, lakini magonjwa yote mawili yanaweza kujitokeza shambani kuanzaia wiki 3-5 baada ya karanga kupandwa.

Puccinia arachidis. Husababisha ugonjwa wa Kutu.


Kuzuia

Kupanda mapema.

Kuondoa maotea ya karanga wakati wa kiangazi.

Tumia dawa aina ya Chlorothalonil (Daconil 2787)


Dawa huwekwa kiasi cha kilo 1.6 katika lita 800 za maji kwa hekta moja, kila baada ya siku saba, kwa majuma machache kuanzaia maratu dalili za ugonjwa zinapoonekana. Uchunguzi juu ya aina zinazostahimili magonjwa haya bado unaendele kufanywa Naliendele.



(iii) Ugonjwa wa Rosette (Rosette virus disease)

Ugonjwa huu huambukizwa na wadud waitwao “Vidudu Mafuta” Aphids (Aphis cracivora). Mimea ambayo imeshambuliwa na ugonjwa huu hudumaa, na inakuwa na madoa ya njano.


Kuzuia

Kupanda mapema

Panda karanga zako shambani katika nafasi za karibu karibu.

Palilia na toa maotea shambani mwako.


(iv) Ugonjwa wa maganda matupu (Empty pods or pops)

Karanga zilizoshambaliwa na ugonjwa huu, huwa lazina mbegu (maganda matupu). Ugonjwa huu husababishwa na ukosefu wa madini ya Calcium (chokaa) kwenye udongo.


Kuzuia

Tumia Calcium katika hali ya Gypsum (Ca SO4) kwenye mimea au weka Chokaa (lime – CaO) kwenye udongo kabla ya kupanda. Ugonjwa huu uko kwenye mikoa ya kusini mwa Tanzania (Lindi, Mtwara na Ruvuma) na hushambulia sana karanga za muda mrefu kama vile Red Mwitunde.


Majaribio hapa Tanzania hayajathibitisha kuweka chokaa (Liming) kuwa ni jibu sahihi la kupambana na ugonjwahuu, lakini ili kupunguza, kupanda mapema ni muhimu.


Wadudu Waharibifu Wa Karanga

(i) Mafuta Aphids au “Vidudu Mafuta” (Aphis cracivora)

Hushambulia karanga kila msimu, lakini athari yao kubwa ni kueneza ugonjwa wa Rosette. Wakati wa mvua nyingi huoshwa toka kwenye majani, hivyo hawaleti madhara.


Kuzuia

Kupanda mapema

kupanda karanga karibu karibu


(ii) Groundnut hopper: Hilda patruelis

Hufyonza mizizi, “pegs”, na karanga changa, hivyo husababisha majani kuwa manjano, kunyauka, na mmea kukauka ungali mchanga. Wadudu hawa hushambulia mazao mengine kama vile maharage, kunde. alizeti na korosho, hivyo kunahitajika mzunguko (rotation) mzuri wa mazao.


Kuzuia

Kwenye mashamba makubwa, inashauriwa kutumia dawa aina ya Aldrin au chloropyrifos, kuchanganya kwenye ardhi kabla ya kupanda.

Kunyunyizia Dimethoate mara tu wadudu wanapoonekana

Kutochanganya na zao la korosho au mbaazi kwenye shamba moja na karanga.


(iii) Mchwa

Kuna aina mbili za mchwa ambao hushambulia na kusababisha uharibifu kwenye zao la karanga.


Aina ya kwanza ni wale ambao hutoboa sehemu ya chini kwenye mzizi, au kutengeneza matundu, na hukaa kwenye mmea wa karanga wakati wote zikiwa shambani.


Aina ya pili ni wale ambao hukata matawi yanayokua au kutambaa. Uharibifu huu huonekana zaidi kwenye shamba jipya. Kuchelewa kuvuna kunaweza kusababisha kupotea kwa mazao mengi, kutokana na kuharibika kwa mizizi, na kusababisha karanga nyingi kubakia shambani wakati wa kuvuna.


Kuzuia

Mchwa wanaweza kuzuiwa kwa kutumia dawa aina ya Alandrin 40% ya unga, kwa kiasi cha kilo 2.5 kwa hekta. Njia rahisi ni kuchanganya dawa na mbolea aina ya Phosphate (TSP au SSP) au mchanga na kumwaga shambani kabla ya kupanda karanga.


(iv) Panya

Hushambulia sana karanga zinapoanza kuota, na wakati zinapokaribia kuvunwa.


Namna ya Kuzuia panya:

Tumia dawa za kuua panya

Mitego

Kuwachimbua toka ardhini walikojificha.


(v) Ndege

Kama panya, ndege hasa kunguru hushambulia sana karanga kabla hazijaota (mara baada ya kupanda), zinapoanza kuota, zinapokaribia na wakati zimekwisha komaa.


Kuzuia

Kutumia mitego kama vile nyavu za kunasia ndege au ulimbo

Kuamia (…ni kukaa shambani na kufukuza ndege kila wanapokuja kula mazao)

Kuweka (kutundika/kuning’iniza) mzoga au kunguru mzima shambani.

Soma hapa wadudu hatari wa nyanya na namna ya kuyadhibiti


Kung’oa Karanga

Utajuaje kama karanga zako zimekomaa? Zifuatazo ni baadhi ya dalili za jumla ambazo huonekana kwenye karanga zilizokomaa:

Angalia majani: huwa yanabadilika rangi kuwa ya manjano na kuanza kupata au kuongezeka ugonjwa wa madoa madoa na hatimaye kudondoka

Ukichimba na kuangalia mapodo yanaonekana kuwa magumu na hupasuka kwa urahisi. Podo la karanga ambazo hazijakomaa huwa laini na hubonyea linapominywa.

Rangi ya ndani ya podo hubadilika kutoka nyeupe na kuwa ya kahawia.

Ukichimba karanga (katika maeneo mbalimbali ya shamba) na ukapata mashina saba au zaidi yaliyokomaa katika kila mashina 10, basi karanga zako zimekomaa, ngo’a.

Zinapokaribia siku za kukomaa kutokana na idadi ya siku inazochukua tangu kupanda hadi kukomaa. Hakikisha unakumbuka aina ya mbegu uliyopanda na muda inayotumia kukomaa, zichunguze karanga kadri zinavyozidi kukaribia.


Karanga zilizong’olewa


Kupurura Karanga

Kupurura ni kutenganisha mapodo ya karanga na shina. Tenganisha mapodo ya karanga na shina kwa kutumia mikono. Mapodo ya karanga pia yanaweza kupururwa kwa kutumia ncha ya jembe au pipa lililokatwa. Ukishapurura unapata karanga za mapodo. Shughuli hii hufanyika mara tu baada ya kung’oa. Mara baada ya kupurura, karanga za mapodo huchambuliwa na baadae kuanikwa juani ili zikauke na kuhifadhiwa mpaka zitakapo hitajika kwa matumizi au kuuza.


Kuchambua Karanga

Chambua mapodo ya karanga zilizopururwa kwa kutenga yaliyosinyaa, yasiyo na punje, yaliyooza au kutobolewa na wadudu. Lengo la kuchambua ni kupata mapodo ya karanga yaliyo bora. Mapodo ya karanga bora yatengwe tayari kwa kukaushwa au kusafirishwa.





Kuchambua karanga



Kukausha Karanga

Mapodo ya karanga hukaushwa vizuri ili kudhibiti uwezekano wa karanga kushambuliwa na magonjwa yatokanayo na ukungu wakati wa kuhifadhi. Kausha juani kwa kutandaza mapodo kwenye kichanja bora, maturubai au sakafu safi. Wakati wa kukausha zingatia yafuatayo:-

Hakikisha punje za karanga zimekauka hadi kufikia unyevu wa asilimia 9 kwa kutumia kipima unyevu au kadiria tu utakapoona zimekauka kiasi cha kutosha.

Ukaushaji wa kupita kiasi husababisha ngozi ya punje ya karanga kutoka wakati wa kubangua na hivyo kupunguza ubora wa zao.

Baada ya kukausha, fungasha mapodo ya karanga safi kwenye magunia yasiyozidi kilo 75.



Kuhifadhi Karanga Za Mapodo

Ili kuepuka uharibifu ni muhimu kuhifadhi karanga zikiwa kwenye mapodo. Karanga zilizobanguliwa huhifadhiwa kwa muda mfupi na hushambuliwa kwa urahisi na nondo na kusababisha upotevu kwa kiasi kikubwa. Hifadhi ya karanga zikiwa kwenye mapodo huwezesha karanga kuhifadhiwa kwa zaidi ya mwaka mmoja wakati zile zilizobanguliwa huweza kuhifadhiwa kwa muda usiozidi miezi miwili.


Kabla ya kuweka karanga ghalani zingatia yafuatayo: –

Safisha ghala ili kuondoa wadudu waharibifu na takataka.

Ziba sehemu zote ambazo zinaweza kuruhusu panya na wadudu wengine kuingia.

Magunia yapangwe kwa kupishanisha ili kuruhusu mzunguko wa hewa.

Karanga pia zinaweza kuhifadhiwa zikiwa katika hali ya kichele kwenye bini, silo, au vihenge.


Kubangua Mapodo Ya Karanga

Mapodo ya karanga hubanguliwa kwa kutumia mikono au mashine.


Kubangua kwa kutumia mikono

Mapodo ya karanga hubanguliwa kwa kuminya ganda kwa kutumia vidole. Njia hii ni ya suluba, huchukua muda mrefu na hufaa kwa kiasi kidogo cha karanga. Hata hivyo njia hii hupungu za upotevu wa mazao. Vilevile punje za karanga huwa bora Zaidi zinapobanguliwa kwa njia hii.







Kubangua karanga ni kazi ngumu sana. Mtu mmoja anaweza kubangua kiasi cha kilo 12-15 kwa siku. Karanga zilizopo kwenye kundi la Virginiahubangulika kirahisi kuliko aina ya Spanish au Valencia. Mashine za kubangulia karanga hupatikana hapa nchini, zinarahisisha kazi, lakini tahadhari isipochukuliwa huharibu karanga. Wastani wa kilo 160 za karanga zilizo kwenye mapodo hutoa kilo 100 za punje za karanga na kazi hii huchukua siku nane kwa mtu mmoja.


Kubangua kwa mashine

Mapodo ya karanga hubanguliwa kwa kutumia vyombo maalumu. Njia hii hubangua karanga nyingi zaidi na kwa muda mfupi. Mashine hizi huendeshwa kwa mkono, umeme au injini. Hurahisisha kazi na zina uwezo wa kubangua wastani wa kilo 40 kwa saa moja.


Kuchambua Karanga Zilizobanguliwa

Punje za karanga zilizosinyaa, zenye ukungu, zilizopasuka, zilizoharibiwa na wadudu na zilizokatika zitenganishwe na karanga bora.

Punje za karanga zilizooza na zenye magonjwa zisitumike kwa chakula cha binadamu wala wanyama.

Chambua kwa makini karanga zilizobanguliwa kwa kutumia vyombo maalum kwani nyingi hupasuka kutegemea aina ya karanga, ukavu wa mapodo na ufanisi wa mashine.


Kupanga Madaraja

Madaraja ya punje za karanga hupangwa kufuata ukubwa, aina na rangi. Pia zingatia viwango vya ubora vilivyowekwa kwa kila daraja la punje za karanga. Punje za karanga zilizo katika daraja la chini zitumike haraka kwani hushambuliwa na vimelea vya ukungu kwa urahisi zaidi. Punje za karanga zilizo bora (daraja la 1) zitumike kwa kuhifadhi, kuuzwa au kusindikwa.


Kufungasha

Fungasha karanga zilizobanguliwa kwenye magunia yenye ujazo usiozidi kilo 100. Karanga zilizobanguliwa zisihifadhiwe kwa muda mrefu, kwani hushambuliwa kwa urahisi na wadudu aina ya nondo na vimelea vya magonjwa ya ukungu.



Karanga ni mojawapo ya mazao yanayotoa mafuta. hulimwa lengo kubwa likiwa ni uzalishaji wa mafuta, chakula na malisho kwa ajili ya mifugo. Katika Tanzania zao hili hustawi zaid katika mikoa ya Kusini Mashariki, Dodoma na Morogoro. Kwa ujumla zao hili hutumika na wakulima kama zao la biashara.


Karanga ni zao maarufu sana duniani katika kilimo cha mzungunguko. Nchini Tanzania uzalishaji wa karanga ni wa chini sana kutokana na kutokuwa na mvua za uhakika, kiwango kidogo cha teknolojia miongoni mwa wakulima, wadudu na magonjwa, pamoja na kutokuwa na mbegu ya uhakika.


Mmea wa karanga ni moja ya mimea mifupi ambayo huota na kuwa na urefu wa sentimita 15-60 kwenda juu. Matunda yake huwa na kati ya mbegu moja mpaka tano, ambapo viriba vyake huwa chini ya ardhi. Mbegu zake huwa na kiasi kikubwa cha mafuta (38% – 50%), protini, kalishamu, potashiamu, fosiforasi, magnesiamu na vitamini. Inasadikiwa kuwa karanga pia zina aina fulani ya viini vinavyotumika kama dawa.


Kiasi kikubwa cha karanga inayozalishwa duniani hutumika kwa kutengenezea mafuta ambayo hutumika kwa kupikia chakula. Makapi yanayotokana na karanga baada ya kukamua karanga ni mazuri sana kwa malisho ya mifugo lakini pia hutumika kwa kutengenezea unga wa karanga ambao kwa kiasi kikubwa hutumika kwa chakula cha binadamu.


Karanga pia zinaweza kuliwa zikiwa mbichi, zikiwa zimechemshwa au kukaangwa. Zinaweza pia kutengenezwa kama kitafunwa kwa kuchanganywa na sukari au asali. Pia karanga hutumika kwenye supu, mchuzi, au kama kiungo kwenye aina nyingine za vyakula kama vile nyama na wali. Mabaki ya mimea yake ni malisho mazuri sana kwa wanyama.


Karanga hulimwa kama zao linalojitegemea, lakini pia hupandwa mseto na mahindi na hata mihogo. Ni zao zuri pia kuchanganya na mpunga unaolimwa sehemu za mwinuko, mtama, miwa na alizeti. Ili kupata mavuno mazuri inapendekezwa kuwa makini na nafasi tofauti na upandaji wa kienyeji.


Kwa maeneo mengine karanga hulimwa kwenye sehemu yenye miti ya mazao ya kudumu kama vile minazi, mipapai, na miti ya mawese. Karanga zinapopandwa mseto na mahindi kwenye sehemu zenye mwinuko husaidia kupunguza mmomonyoko wa ardhi. Mimea ya karanga pia hupunguza uwepo wa vidukari kwa kuwa huwa ni maficho ya wadudu rafiki. Kunakuwa na ongezeko la mavuno ya karanga zinapopandwa mseto na kunde zinazokomaa haraka.


HALI YA HEWA

Karanga hulimwa kwenye sehemu yenye joto, wastani wa mwinuko wa mita 1500 kutoka usawa wa bahari. Kiwango cha joto kinachohitajika kila siku ni kiasi cha jotoridi 30, na wakati wa ukuaji kinaweza kupungua mpaka jotoridi 15. Hali ya ubaridi huchelewesha karanga kuchanua.


Kwa kuwa viriba vya karanga huwa kwenye udongo na ni lazima kuchimbuliwa wakati wa mavuno, huku vikiwa ni vyepesi kuvunjika, ni vizuri kuwa na udongo mkavu, lakini mmea hukua na kustawi vizuri kwenye udongo wa kichanga!


MVUA

Kiasi cha milimita 500-600 cha maji katika msimu wote wa ukuaji wa karanga kinatoa fursa nzuri ya uzalishaji. Hata hivyo karanga ni moja ya mazao yanayostahimili ukame, na linaweza kuvumiliwa ukosefu mkubwa wa maji. Hali inapokuwa hivyo hupunguza kiasi cha mavuno.


Inashauriwa kutopanda karanga kwenye udongo mzito (mfinyanzi) hii ni kutokana na sababu kwamba, karanga hazistawi kwenye sehemu zinazo simama maji, na udongo mzito huleta hasara wakati wa uvunaji.


MBEGU BORA ZA KARANGA

Kuna aina kuu tano bora za Mbegu Za karanga ambazo zimetolewa kwa wakulima hapa nchini.


A. RED MWITUNDE

Ilitolewa kwa wakulima miaka ya 1950. Mbegu za muda mrefu (Virginia Spreading bunches). Huchukua muda wa siku 120 -140 toka kupanda hadi kukomaa. Ina uwezo wa kutoa kilo 1000 kwa hekta. Mbegu zake ni kubwa na zina rangi nyekundu.


B. NYOTA

Ilitolewa mwaka 1983. Mbegu ya muda mfupi ( Spanish Errect Banch).

Huchukua siku 90-100 tangu kupanda hadi kukomaa. Ina uwezo wa kuzaa wastani wa kilo 1500 kwa hekta. Mbegu zake ni ndogo, na zina rangi ya udongo (Tan). Aina hii ya mbegu zina tabia ya kuanza kuota tena shambani mara tu zikiisha komaa, hivyo ni muhimu kuzivuna mapema zikisha komaa.


C. JOHARI:

Ilitolewa mwaka 1985. Mbegu ya muda wa kati (Virginia Spreading Bunches).

Huchukua siku 110 – 120 toka kupanga kuvuna. Mbegu zake ni kubwa na zina rangi ya udongo (Tan). Ina uwezo wa kutoa wastani wa kilo 1000 kwa hekta moja.


D. PENDO:

Ilitolewa mwaka 1998. Mbegu ya muda mfupi ( Spanish Errect Banch). Huchukua siku 90-100 tangu kupanda hadi kukomaa. Ina uwezo wa kuzaa wastani wa kilo 1500 kwa hekta. Maganda yake ni laini na mbegu zake ni kubwa, na zina rangi ya udongo (Tan). Kama Nyota, aina hii ya mbegu ina tabia ya kuanza kuota tena shambani mara tu zikisha komaa, hivyo ni muhimu kuzivuna mapema zikisha komaa.


E. SAWIA:

Ilitolewa mwaka 1998. Mbegu ya muda wa kati (Virginia Spreading Bunches).

Huchukua siku 110 – 120 toka kupanga kuvuna. Mbegu zake ni kubwa na zina rangi ya udongo (Tan). Ina uwezo wa kutoa wastani wa kilo 1000 kwa hekta moja.


Pamoja na mbegu zilizotajwa, kuna aina nyingine nyingi za kienyeji (local varieties) zinazotumiwa na wakulima katika sehemu mbali mbali.


UTAYARISHAJI WA SHAMBA

Shamba litayarishwe vizuri kuwezesha udongo kupenyesha maji na mizizi kirahisi. Karanga hupandwa kwenye matuta au sensa (shamba tambarare).


Karanga ambazo zinakusudiwa kwa mbegu zitunzwe na maganda yake bila kubanguliwa. Zibanguliwe karibu na msimu wa kupanda na kuchaguliwa. Baada ya kuchaguliwa zitiwe dawa, aina ya Fernasan D, Katika uwiano wa gramu 28 za dawa kwa kila kilo 10 za mbegu safi.


WAKATI WA UPANDAJI

Inapendekezwa kupanda kwenye sehemu ambayo udongo una kina na ambao chembechembe zake ni laini. Kuwa makini na uhakikishe kuwa sehemu ya kitalu haina magugu. Kitalu chenye udongo usiokuwa na chembe laini na tambarare inaweza kusababisha upotevu mkubwa wa mimea.


Inapendekezwa kuwa na kiasi cha mimea 200,000 – 250,000 kwenye hekari moja, hasa kwa aina ambayo ni ya muda mfupi. Kwenye nchi nyingi karanga hulimwa kwa kupanda kwenye mistari, ambayo mingi huwa na nafasi ya sentimita 40 x 20 mpaka sentimita 30 x 20.


Baada ya kulima na kusawazisha vizuri, tengeneza matuta yenye mwinuko wa sentimita 80, na sehemu ya juu iwe bapa ili uweze kupanda mistari miwili ya karanga kwenye kila tuta. Ni lazima kuchagua mbegu za kupanda kwa umakini. Ni lazima ziwe safi, zilizojaa vizuri na bila kuwa na mikwaruzo yoyote.


Mbegu zinazokusudiwa kupandwa ni lazima ziachwe kwenye viriba vyake na kumenywa siku chache kabla ya kupanda. Kina cha upandaji wa karanga ni sawa na mahindi ambapo huwa kati ya sentimita 5-8.


Uamuzi wa kuchagua wakati mzuri wa kupanda niule utakaoliwezesha zao hilo kukomaa wakati wa mvua za mwisho. Kuchelewa kupanda, hupunguza mavuno. Ni muhimu kuchagua aina ya mbegu ambazo uvunaji wake unafanana na mazingiza ya eneo hilo kihali ya hewa.


Kwa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma, karanga za muda wa kati na mrefu (Johari, Red Mwitunde) zipandwe kuanzia katikati, hadi mwishoni mwa mwezi Desemba. Karanga za muda mfupi (Spanish na Valencia) zipandwe kuanzia mwishoni mwa mwezi Desemba hadi katikati ya mwezi Januari. Kwa mikoa ya Tanga, Morogoro na sehemu za mkoa wa Dodoma, karanga zipandwe mapema mwanzo wa mvua ndefu. (Februari/March).


NAFASI KATI YA MIMEA

Inashauriwa kupanda karanga katika mistari. Nafasi kati ya mistari ni sentimita 40, na kati ya mimea ni sentimita 15, kwa karanga zinazotambaa (Virginia Spreading types). Kama karanga zinapandwa kwenye matuta ya sentimita 90, zipandwe mistari miwili, kila tuta. Kwa nafasi hii kiasi cha kil 60-75 za mbegu hutumika kwa hekta moja.


Kwa karanga zilizopo kwenye kundi la Spanish/Valencia (zisizotambaa), nafasi kati ya mistari ni sentimita 40, na kati ya mimea ni sentimita 10. Endapo karanga zimepandwa kwenye matuta ya sentimita 90, panda mistari miwili , inayofanya nafasi sawa na sentimita 40 kwa sentimita 10. Kiasi cha kilo 80-100 za mbegu hutumika kwa hekta moja kwa kutumia nafasi hii.Kwa ina zote za mbegu, panda mbegu moja safi, katika kila shimo.


MBOLEA

Kufuatana na majaribio yaliyofanyika imeonekana kuwa karanga hustawi vizuri chini ya viwango vidogo vya phosphorus. Vyanza vya kirutubisho cha Phosphorus ni mbolea za kupandia nazo ni kama TSP, SSP na DAP. Mbolea hizi zote ziwekwe kabla ya kupanda au wakati wa kupanda lakini umakini unahitajika kutoruhusu mbolea kugusana na mbegu. Kiasi cha Kilo 90 za Phosphorus (= mifuko minne ya DAP) kinatosha kwa hekta moja ambayo ni sawa sawa na kilo 35 (= mfuko mmoja na nusu wa DAP) kwa ekari.


Vile vile katika sehemu nyingine, karanga zimefanya vizuri kwa kutumia samadi. Ubadilishaji wa mazao (Crop Rotation) husaidia kutunza rutuba, hivyo kupunguza kiasi cha mbolea kinachotumika. Karanga zinaweza kulimwa baada ya mahindi, ili kutumia masalia ya mbolea.


UPALILIAJI

Karanga zipaliliwe zikiwa changa. Shamba lililotayarishwa vizuri na kuondolewa magugu ya muda mrefu (Perrenial weeds) linaweza kupalliwa mara moja, kwa sababu karanga hukua haraka, na zinaweza kushindana na magugu. Baada ya kutoa maua, karanga zisipaliliwe, hii inaweza kuharibu ‘pegs’, hatimaye kupunguza mavuno.


MATUNZO

Ili kuwa na mavuno ya hali ya juu, ni lazima magugu yadhibitiwe kabisa. Karanga ni dhaifu sana katika kukabiliana na magugu hasa katika kipindi cha mwanzo cha ukuaji. Ni lazima palizi ifanyike mapema wakati huo miche ikiwa inachomoza kwenye udongo. Miche ikashachomoza palizi ifanyike kwa mikono ili kuepuka usumbufu kwa karanga changa au kuharibu maua. Palizi ya kawaida inaweza kufanyika mpaka kwenye kipindi cha wiki 6 na palizi ya mikono ifanyike baada ya hapo.


Virutubisho pekee vinavyohitajika kwenye shamba la karanga ni kalishamu. Kalishamu hunyonywa moja kwa moja na viriba vya karanga endapo udongo una unyevu unyevu. Kama kutakuwepo upungufu wa kalishamu, viriba vya karanga vitakuwa vitupu bila kuwa na karanga. Mimea inayohitaji Naitrojeni inaweza kupatikana kwa kushirikisha mimea mingine kama vile kunde, badala ya kuweka mbolea ya Naitrojeni kwenye udongo.


MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU:


MAGONJWA

(I) UGONJWA WA KUOZA (AFLATOXIN)

Katika hali ya unyevu mwingi vimelea viitwavyo Aspegilus flavus huota ndani ya maganda na kushambulia mbegu za karanga. Vimelea hivyo hutoa kemikali ambayo ni sumu.


KUZUIA

Hakikisha kuwa karanga haziharibiwi wakati wa kuchimba Hakikisha karanga zinakaushwa vizuri (Unyevu wa 10%) kabla ya kuzitunza zitumike kama mbegu Karanga za kupanda zitiwe dawa aina yaØ Fernasan-D.


(II) UGONJWA WA MADOA NA KUTU: (CERCOSPORA LEAF SPOTS AND RUST)

Magonjwa haya husababisha madoa ya rangi ya kikahawia hadi meusi kwenye majani. Vimelea vinavyosababisha magonjwa haya viko vya aina 3:


(a) Cersospora arachidicola. Husababisha Early Leaf Spot.

(b) Phaeoisariopsis personata. Husababisha Late Leaf spot.

Ugonjwa wa Early Leaf Spot hutangulia kuonekana, lakini magonjwa yote mawili yanaweza kujitokeza shambani kuanzia wiki 3-5 baada ya karanga kupandwa.

(c) Puccinia arachidis. Husababisha ugonjwa wa Kutu.


Kuzuia:

Kupanda mapema. Kuondoa maotea ya karanga wakati wa kiangazi.Tumia dawa aina yaØ Chlorothalonil (Daconil 2787). Dawa huwekwa kiasi cha kilo l.6 katika lita 800 za maji kwa hekta moja, kila baada ya siku saba, kwa majuma machache kuanzaia maratu dalili za ugonjwa zinapoonekana. Uchunguzi juu ya aina zinazostahimili magonjwa haya bado unaendele kufanywa kwenye kituo cha utafiti wa kilimo Naliendele.


(III) UGONJWA WA ROSETTE (ROSETTE VIRUS DISEASE)

Ugonjwa huu huambukizwa na wadudu waitwao “Mafuta” Aphids (Aphis craccivora). Mimea ambayo imeshambuliwa na ugonjwa huu hudumaa, na inakuwa na madoa ya njano.


Kuzuia:

Kupanda mapema, Panda karanga zako shambani katika nafasi za karibu karibu.Palilia na toa maotea shambani mwako.Ø


(IV) UGONJWA WA MAGANDA MATUPU (EMPTY PODS OR POPS)

Karanga zilizoshambaliwa na ugonjwa huu, huwa lazina mbegu (maganda matupu). Ugonjwa huu husababishwa na ukosefu wa madini ya Calcium (chokaa) kwenye udongo.


Kuzuia:

Tumia Calcium katika hali ya Gypsum (Ca SO4) kwenye mimea au weka Chokaa (lime – CaO) kwenye udongo kabla ya kupanda. Ugonjwa huu uko kwenye mikoa ya kusini mwa Tanzania (Lindi, Mtwara na Ruvuma) na hushambulia sana karanga za muda mrefu kama vile Red Mwitunde. Majaribio hapa Tanzaniia hayajathibitisha kuweka chokaa (Liming) kuwa ni jibu sahihi la kupambana na ugonjwa huu, lakini ili kupunguza, kupanda mapema ni muhimu.


2. WADUDU WAHARIBIFU

(I) MAFUTA APHIDS AU “MAFUTA” (APHIS CRACIVORA)

Hushambulia karanga kila msimu, lakini athari yao kubwa ni kueneza ugonjwa wa Rosette. Wakati wa mvua nyingi huoshwa toka kwenye majani, hivyo hawaleti madhara.

Kuzuia:

• Kupanda mapema

• Kupanda karanga karibu karibu


(II) GROUNDNUT HOPPER: HILDA PATRUELIS

Hufyonza mizizi, pegs, na karanga changa, hivyo husababisha majani kuwa manjano, kunyauka, na mmea kukauka ungali mchanga. Wadudu hawa hushambulia mazao mengine kama vile maharage, kunde. alizeti na korosho, hivyo kunahitajika mzunguko (rotation) mzuri wa mazao.

Kuzuia:

• Kwenye mashamba makubwa, inashauriwa kutumia dawa aina ya Aldrin au chloropyrifos, kuchanganya kwenye ardhi kabla ya kupanda.

• Kunyunyizia Dimethoate mara tu wadudu wanapoonekana.

• Kutochanganya na zao la korosho au mbaazi kwenye shamba moja na karanga.


(III) MCHWA.

Kuna aina mbili za mchwa ambao hushambulia na kusababisha uharibifu kwenye zao la karanga. Aina ya kwanza ni wale ambao hutoboa sehemu ya chini kwenye mzizi, au kutengeneza matundu, na hukaa kwenye mmea wa karanga wakati wote zikiwa shambani.


Aina ya pili ni wale ambao hukata matawi yanayokua au kutambaa. Uharibifu huu huonekana zaidi kwenye shamba jipya. Kuchelewa kuvuna kunaweza kusababisha kupotea kwa mazao mengi, kutokana na kuharibika kwa mizizi, na kusababisha karanga nyingi kubakia shambani wakati wa kuvuna.


Kuzuia:

Mchwa wanaweza kuzuiwa kwa kutumia dawa aina ya Alandrin 40% ya unga, kwa kiasi cha kilo 2.5 kwa hekta., Njia rahisi ni kuchanganya dawa na mbolea aina ya Phosphate (TSP au SSP) au mchanga na kumwaga shambani kabla ya kupanda karanga.


(IV) PANYA:

Hushambulia sana karanga zinapoanza kuota, na wakati zinapokaribia kuvunwa.

Namna ya Kuzuia panya:

• Tumia dawa za kuua panya

• Mitego

• Kuwachimbua toka aridhini walikojificha.


(V) NDEGE

Kama panya, ndege hasa kunguru hushambulia sana karanga kabla hazijaota (mara baada ya kupanda), zinapoanza kuota, zinapokaribia na wakati zimekwisha komaa.


Kuzuia

• Kutumia mitego

• Kuamia

• Kuweka (kutundika/kuning’iniza) mzoga au kunguru mzima shambani.


UBANGUAJI NA UTUNZAJI WA KARANGA

MAVUNO

Karanga zinazokomaa kwa muda mfupi zinaweza kuvunwa kati ya siku 85-100 tangu kupandwa, na zinazochukua muda mrefu zinaweza kuvunwa katika kipindi cha siku 110-130 tangu kupandwa. Ng’oa mashina machache kuona kama karanga zimeshakomaa. Karanga zilizokomaa ni lazima ziwe na rangi ya kahawia kwa nje, ngumu na zilizokauka.


Kwa kawaida karanga zilizokomaa ndani ya kiriba huwa na rangi ya kahawia, na hutoa sauti inapotikiswa. Magonjwa yanaposhambilia majani ya karanga yanaweza kusababisha karanga kuvunwa kabla hazijakomaa sawa sawa. Ni lazima karanga zichimbwe kwa umakini ili kuepuka karanga kupasuka na kubakia ardhini. Anika kwa siku 2-3, kisha zikwanyue na uanike tena kwenye jamvi kwa siku 7-10 ili kuondoa unyevu kufikia asilimia kumi.


Ubambuaji wa karanga ufanyike kwa mikono au kwa mashine maalum. Karanga zilizopondeka, chafu au kuharibika zitengwe kwani zitapunguza ubora wa karanga na kupunguza bei ya kuuzia. Endapo karanga hazikuhifadhiwa vizuri zinaweza kushika unyevu unyevu ambao husababisha sumu inayojulikana kama aflatoxin ambayo ni hatari sana kwa afya ya binadamu hasa ini. Karanga ambazo zitatumika kwa ajili ya kupanda (mbegu) msimu unaofuata zisibamGuliwe kutoka kwenye viriba. Ubora na uwezo wa karanga kuota huanza kupotea mara baada ya kubanguliwa


Kubangua karanga ni kazi ngumu. Mtu mmoja anaweza kubangua kiasi cha kilo 12-15 kwa siku. Karanga zilizopo kwenye kundi la Virginia hubangulika kirahisi, kuliko aina ya Spanish au Valencia. Mashine za kubangulia karanga hupatikana hapa nchini, zinarahisisha kazi, lakini tahadhari isipochukuliwa huharibu karanga.


Karanga zinazokusudiwa kutunzwa kwa muda mrefu, zitunzwe na maganda yake kwenye ghala. Ghala iwe kavu, yenye kupitisha hewa, na imara kuzuia wanyama waharibifu kama vile panya.Ubora na uwezo wa karanga kuota huanza kupotea mara baada ya kubanguliwa.

0 comments: