Saturday, 3 June 2023

FAIDA YA MDUDU MAJIMOTO KATIKA MAZAO

 FAIDA ZA MDUDU MAJIMOTO

Utangulizi
Majimoto (Oecophylla longinoda) ni wadudu maarufu sana katika Kanda ya Kusini mwa Tanzania. Wanaitwa Majimoto kwa sababu wanapouma,, huleta maumivu kama ya maji ya kukandia jeraha!. Kwa msingi huo huo, wayao huwaita “malumila” wasambaa huwaita “madadada” na Wamwera nao huwaita “ mangongongo”. Majimoto ni maarufu sana kwa uhodari wao wa kujenga viota kwa kufuma majani mabichi .
Ukubwa wa kiota hutegemea ukubwa wa ukoo, aina ya mti na majani yatumikayo na ulaini wa majani yenyewe. Kuna aina ya miti zaidi ya 75 ambayo Majimoto wameonekana kujenga viota vyao, ikiwa ni pamoja na mikorosho, michungwa, miembe na mengineyo.
Utafiti wa awali uliofanyika kwa mahojiano na wakulima mbalimbali, umeonyesha kwamba wengi hawajui faida yoyote toka kwa wadudu hawa, zaidi sana walisimulia athari zao kwamba ni wadudu wanaouma sana na kuleta maumivu makali. Nimeandaa makala hii ili kuhamasisha na kufundisha watu kwamba Majimoto ni rafiki wa mkulima.
Ukoo wa Majimoto una malkia mmoja tu ambaye analishwa na watenda kazi wakuu, ambapo yeye kazi yake ni kutaga mayai. Akitaga mayai watenda kazi wadogo (minor workers) ndio huchukua na kuatamia na hatimaye kuwatunza wachanga wanapototolewa.

Watenda kazi wakuu ndio hufanya mawindo na mashambulizi makali katika mti hadi ardhini, nao hukamata wadudu aina nyingi tu ambao wanakutana nao. Mmoja akimshika mdudu, hutoa harufu ya tahadhari na kufumba na kufumbua Majimoto wengi hujikusanya na kusaidia mashambulizi hadi kuua na hatimaye kupeleka chakula katika viota vyao

MATUMIZI
Majimoto hutumika kuthibit wadudu wahalibifu inawezekana ikawa katika michungwa, miembe, au milimao.
Wadudu hawa hutumika kuwadhibiti wadudu kama vile mbu wa mikorosho na minazi. Mikorosho hushambuliwa na mbu hvyo wadudu hawa hutumika kufanya ulinzi hususani katika tegu.
JINSI YA kuwaeneza
,, Ili wawe walinzi wa mikorosho unahitajika kuwaeneza na wawe wengi Zaid kitu ambacho kitapelekea kuwa na uwezo mkubwa wa kupambna na wadudu wahalibifu.
1.kiota hii ni njia moja wapo ya kuwaeneza ktk shamba lako hamisha kiota kutoka mti mmoja kwenda mwingine, ukifanya hivi watazaliana na mwisho wa siku mikorosho yako yote itakua Tayari wako Majimoto na kukuimalishia ulinzi.
2.Njia ya kamba, njia hii pia itakusaidia kuwahamisha Majimoto kutoka mti mmoja kwenda mwingine, unafunga kama mti ambao una Majimoto kwenda ktk mti mwingine ambao hauna maji moto. Hvyo kamba itatumika kama njia yao kwenda ktk mti mwingine.
ANGAGALIZO
Koo za Majimoto ni korofi sana kama zikikutana koo TOFAUTI, hvyo kuepuka mwingiliano wa koo hakikisha unawapandikiza Majimoto katika mti ambao hauna Majimoto wengine. Kwahyo chunguza mti Kama hauna Majimoto ndipo upandikize.
3thibiti adui wa Majimoto
Kuna baadhi ya wadudu ni adui wa maji moto, kama vile sisimizi na sangara hawa ni maadui wakubwa sana.. Hvyo kama ktk mti huo kuna hawa wadudu puliza dawa za kuwaua, na uhakikishe wote wamekuta ndipo upandikize hawa Majimoto..

http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

Read less
image

0 comments: