Wednesday, 14 June 2023

KILIMO CHA NJUGU

 YouTube channel.https://www.youtube.com/@sharphy_Ismaily

Email address. Shafii.ismail09@gmail.com


WhatsApp /call. 0683308173


Website.http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com


NJUGU
Njugu ni mbegu za mmea wa njugu. Mmea huo unapoendelea kusitawi huwa unachanua maua ya manjano ambayo hujichavusha yenyewe. Kilimo hiki kina faida hasa pale mkulima anapoamua kujiwekeza katika kulima kilimo hiki.

Njugu husitawi vizuri katika maeneo yenye joto na mvua ya wastani. Kuna kipindi cha siku 120 au 160 kati ya wakati wa kupanda na kuvuna, ikitegemea aina ya njugu na hali ya hewa. Wakati wa kuvuna, ni lazima wakulima wa njugu wachimbue mimea hiyo na kuipindua, halafu wanaiacha ikauke ili isioze wakati inapohifadhiwa.

Njugu ni chakula chenye virutubisho vingi sana. Njugu husaidia sana umeng’enyaji wa chakula, na zina vitamini 13 na madini 26. Vingi kati ya virutubisho hivyo havipatikani katika vyakula vya kisasa. “Njugu zina protini nyingi zaidi, madini mengi zaidi, na vitamini nyingi kuliko maini ya ng’ombe.” Lakini watu wanaotaka kupunguza uzito wao wanapaswa kutahadhari! Njugu zina “mafuta mengi kuliko malai nzito” na “kalori nyingi kuliko sukari.”

Lakini mbali na kutumiwa kama chakula, njugu zina matumizi mengineyo. Katika bara lote la Asia, njugu hutumiwa kutengeneza mafuta ya kupikia. Mafuta ya njugu yanaweza kutumiwa pia kupikia vyakula vinavyohitaji kupikwa kwa moto mkali, na hayapati harufu ya vyakula vinavyopikwa.

Read less
imageimage

0 comments: