Friday, 9 June 2023

Aina za mbolea na wakati wakutumia

KILA MBOLEA INAWAKATI WAKE WAKUITUMIA

Email Shafii.ismail09@gmail.com 

WhatsApp /call 0683308173 

Website http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

 KUPANDIA

Mmea ukiwa mdogo yaan wakati unahamishia shambani unataka phosphate ili ukuze mizizi. Hii inapatikana kwenye DAP, MAP (ya drip) na NPK. Vyema kutumia DAP sababu ina Phosphate nyingi zaidi ya zote. KUKUZIA Mmea unataka zaidi nitrate hii inapatikana kwenye CAN, UREA, S.A, NPK, DAP etc. Vyema kutumia CAN au NPK sababu inakupa nitrate kabisa nyingine zinakupa Ammonium, DAP haifai sababu ina Ammonium kidogo sana ndio maana huwa tunapandia tu. UREA nzuri pia lakini jua ukiiweka inaanza kufanya kazi baada ya siku 18 na inakirutubisho kimoja tu. S.A inatabia ya kubadili udongo sababu ya Sulphur ila kwa pilipili unaweza kua na advantage ukiitumia kwa kuzalisha pilipili kali zaidi(sulphur ndio ile harufu ya ukali ya pilipili). WAKATI WA MAUA Wakati wa mmea kutoa maua na matunda unataka zaidi calcium na potassium ili kutoa maua, kuzuia maua yasidondoke, kutoa matunda, kutengeneza ngozi ya tunda na kutengeneza Mbegu. Hivyo hapa unaweza tumia CAN, MOP au NPK. Sasa CAN ina nitrate na calcium, MOP ina potassium pekee na NPK ina nitrate, phosphorous na potassium. Utaona kupata madini mawili ya stage hii lazima utumie mbolea mbili sasa ukitumia CAN na NPK utaona una double nitrate hivyo mmea utakua zaidi hautajua unatakiwa uzae sasa, hivyo vyema kutumia CAN na MOP sababu utapata calcium, nitrate na potassium. UCHANGANYANJI WA MBOLEA Kuhusu kuchanganya the more the better, calcium inatabia ya kureact na madini mengine but hiyo ni text book situation ambapo tunachukulia one element plus one element, ukija kwenye reality ukichanganya CAN na MOP inamaana mchanganyiko wako unakua na calcium, nitrate na potassium plus carrier materials sio rahisi kureact sababu haziko sehemu moja unaweza kuta MOP zimekaa zenyewe au calcium zimekaa zenyewe so hiyo theory imeprove failure

0 comments: