Tuesday, 23 May 2023

 Bado tunasonga mbele na sekta yetu ya kilimo na Leo tuone kwa ufupi kuhusu upande wa uwekezaji katika miti ya mbao. 




Kwa waliowekeza tayari katika kupanda miti au wanaotarajia kuwekeza, bila Shaka tunajua miti ni moja ya raslimali muhimu sana na yenye faida kubwa kutokana na matumizi yake mbalimbali ambayo ni karbia Kila sehemu utakuta Kuna kitu kimetengenezwa kwa matokeo ya mti, yaani mbao, nguzo za umeme n.k . Hebu kwa ufupi tuone Nini changamoto katka uwekezaji huu.



## ndugu wawekezaji miti ni moja ya raslimali ambazo hudumu kwa mda mrefu kdg tangu kupanda mpka kuvuna na kupata faida, tofauti na mazao mengine kwani miti huchukua miaka kadhaa ili uweze kuvuna. Je? Changamoto zipi utakutana nazo katika uwekezaji huu. 



(1) ARDHI MITI ILIPOPANDWA


licha ya kua changamoto hii sio sana lakini Kuna baadhi ya maeneo utakuta ukuaji wa miti unaenda polepole Sana tofauti na eneo lingine. Hi ni kwasababu ya miti kupandwa kwenye eneo ambalo ni mlima wenye mawe Sana chini au kokoto, ikiwa miti ipo eneo la hivyo basi ni kawaida kuona miti yako inakua polepole  tofauti na pahala pengine pasipo na changamoto hio, kwani miti huñg'ang'ana kutafuta chakula na maji chini ya udongo. Hivyo ukiona umepanda miti na inakua polepole shida ni hiyo. Lakini Kama eneo lako zuri tuu na miti una uhakika inasuasua basi waulize wataalamu wa kilimo.


(2) AJALI ZA MOTO


hi ndio changamoto kuu na tishio katika uwekezaji huu wa miti. Kila utakapoenda utakuta wawekezaji wanalia wamepata hasara ya miti kuungua. Nadhani hii ndio shida haswaa baadhi ya watu huuogopa kuwekeza kwenye miti. Mpaka inafika kipindi utasikia mtu anakutania akisema " sahivi huwezi kukopa hela na miti iwe dhamana kwani inafanya ukose usingizi" kisa Cha kauli kama hizi hutokana na Moto kutafuna Sana miti kwenye misitu ya maboss zetu(wawekezaji).


## NINI KINAFANYIKA MITI ISIUNGUE AU IUNGUE#




( A) Fire break/ Banda lesi au barabara ya Moto.


Hii ni njia ambayo hutumika Sana kuzuia Moto kuleta athari katika shamba la miti, njia hii inahusisha utengenezaji wa barabara kulizungua shamba la miti ili kuzuia wakati Moto ukitokea ushindwe kupenya, hapa inamaana kwa Moto unaowaka nje ya shamba yaani eneo jirani ushindwe kuingia shambani kwako, angalizo ikiwa unajua kabisa shamba lako lipo eneo lenye upepo mkali tafadhari weka barabara pana, mpaka mita 15 upana ukiweza, maana ikiwa finyu mno, ndo pale unakuta shambani Moto unawaka hata hujui umepitia wapi.



(B) shamba kuwa karbu na malisho ya mifugo mf. Ng'ombe



Mashamba yaliyo ktk eneo hili Yana hatari zaidi, kwani kipingi Cha kiangazi kinapokarbia , wafugaji wengi huchoma Moto maeneo ili kuua magugu makavu ili mapya yaote kwaajili ya kulishia ng'ombe. Maranyingi Moto huwashwa kisiri Sana hasa usiku, Sasa Kama shamba lako lipo  maeneo haya inamaana wewe Kila mwaka utakua hutulii, moyo wako unadunda mda wote. Cha kufanya unaponunua hebu angalia ikiwa machungio yapo jirani au laa, ila Kama umepanda tayri karbu na maeneo haya basi hakikisha unawahi kutengeneza firebreak mapema Sana pale mvua zinapokata na kiangazi kuingia.


(C,) kilimo Cha mabondeni/ vinyungu au hata mashamba ya kawaida


Hii ni pale shamba la miti linapokuwa karbu na shamba lingine lenye mazao ya misimu, walimaji wa maeneo haya maranyingi hutorosha moto kwa bahati mbaya pingi wanaposafisha mashamba yao. Hasa kilimo Cha mabondeni maana ndicho hulimwa kipingi Cha kiangazi, mwekezaji chunguza karbu na shamba lako ili uchukue tahadhari maana utapata hasara na ukisema utamshitaki aliechoma Bado ni maumivu tuu. 


(D) kuchelewesha malipo kwa vibarua wako.


Hapa sasa, unaepelekea shamba liungue ni wewe mwenyewe mwekezaji,  unaweka vibarua wapluni miti yako au kufyekelea au hata Kaz yoyote shambani kwako, matokeo yake kazi ikiisha unawazungusha vibarua kuwalipa pesa zao. Japo ni tabia mbaya mtu kuchoma shamba la mtu lakini Kuna vibarua huchoma mashamba kwa makusudi kabisa endapo wanahisi kutapeliwa. Na hii Wala mwekezaji hutajua maana hufanywa kisiri, na sababu ni hasira. Hivyo hata Kama unajua unapesa usisahau kibarua ni mfalme wako.


(E)migogoro ya kifamilia kwenye ARDHI. 


Kuna baadhi ya mashamba hupigwa Moto na baadhi ya wanafamilia kisa hakuna maelewano kwenye shambani husika, ko wewe Kama umenunua shamba hakikisha umenunua kihalali na hakuna migogoro .


(F) uvunaji wa asali


Mwekezaji, inawezekana ukapata changamoto ya Moto kutokana na mizinga ya nyuki kuwa  jirani, watu wengi huvuna asali zao kwa kutumia Moto matokeo yake wanawasha mapoli.


(G) Mwekezaji Kama upo mbali, tumia msimamizi mwaminifu shambani kwako. 


Kutokana na ukweli kwamba wawekezaji wengi wanakuwa na miradi mingi ama nao hufanya kazi pahala pengine, na hivyo sio rahisi kuwa karbu na shamba. Hakikisha unakua na msimamizi(foreman) wako mwamijifu kwani atahakikisha vibarua wameridhika kwa kuwalipa kwa wakati, lkn pia pindi unapopata dharula ya kifedha karbia na malipo ya vibarua Basi awe na ulimi wa busara. Lkn pia Kama unaye, Basi yeye ndo anaweza kuwa anaenda shambani na kubaini ikiwa Kuna hatarishi ya Moto.


(H) epuka malumbano yasiyo ya lazima na wawekezaji wenzako uliokarbu nao kwenye mradi wako.


Mda mwinginge, wewe Kama mwekezaji hata kama una nguvu ya pesa, usiwe mwepesi kuwa mkorofi dhidi ya wawekezaji wenzako hasa wa chini yako, saana wale wakulima wadogo wenye mashamba jirani na mradi wako wa miti. Tabia hutofautiana Kuna wengine huwasha Moto ili kumkomoa tu mtu. Hata kama wanafanya makosa flan hebu ongea nao kwa busara tuu! (Friendly talk). 


NB: Hapo juu ni dondoo chache tuu kuhusu kukabiliana na changamoto ya miti, zipo nyingne nyiiingi tuu tofauti na hapo, kwani changamoto hizi hutofautiana kutoka eneo moja na jingine.

WhatsApp/call 0683308173

Email shafii.ismail09@gmail.com


http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

0 comments: