FAIDA ZA KUUNGANISHA/KUBEBESHA MICHE (Grafting/budding)
Sehemu mbili za mimea ya jamii moja (muembe kwa muembe, mparachichi kwa mparachichi) au miche ya aina tofauti kidogo ila jamii moja (mchungwa kwa mlimao) ndiyo inayoweza kuunganishwa au kubebeshwa. Hii kwa kitaalamu huitwa Grafting au Budding. Teknolojia hii ya ubebeshaji wa mimea husababisha upatikanaji wa matunda yenye sifa ambazo wakulima wanazihitaji kwa mfano ladha nzuri, ukubwa wa matunda na ubora unaokidhi soko.
Grafting/Budding Hii huusisha sehemu muhimu mbili:
(a) Sehemu ya shina (mche shina) ambayo hutokana na kuotesha mbegu za mmea ulichaguliwa kuwa mmea shina.
(b) Sehemu ya tawi (kikonyo) huchukuliwa kutoka mti mama wenye sifa za kuzaa matunda mengi na yaliyo bora, ambayo ndiyo yanayotakiwa kama zao.
Mche uliyounganishwa kwa kutumia kikonyo au kitawi kilichochukuliwa kutoka kwa mche mama uliokwisha zaa, utazaa matunda mapema. Kwa mfano, miche ya miembe na michungwa na jamii yake huzaaa baada ya miaka 3-4 hivi ukilinganisha na miaka 7-8 kama miche itapandwa moja kwa moja kutokana na mbegu bila kuunganishwa.
Mche uliounganishwa unadumisha/endeleza sifa halisi ya mmea mama ambao kikonyo chake kimetumika kwenye kuunganisha.
Kuunganisha mche kunatoa nafasi ya kutumia mimea shina ambayo inauwezo kwa mfano wa kuvumilia ukame, magonjwa na ama hali ya udongo ambayo mmea tawi usingeweza kuvumilia
Mimea inaweza kuunganishwa kwa sababu mbalimbali zingine. Kwa mfano kuna aina ya mimea ambayo haina uwezo wa kutoa mbegu (ndimu zisizo na mbegu, machungwa yasiyo na mbegu). Miche inaweza kuunganishwa kwa sababu za kudhibiti magonjwa au wadudu, Pia miti iliyounganishwa itakuwa na umbile dogo endapo mmea shina una asili ya kuwa na umbile dogo.
Kuna njia kuu mbili zinazoweza kutumika katika kuunganisha miche. Njia hizi zimegawanya kufuatana na aina ya kikonyo kinachotumika katika uunganishaji.
• Kuunganisha kwa kutumia kijicho (budding) – Hii hufanyika kwa mimea jamii ya chungwa, limao ndimu nk
• Kuunganisha kwa kutumia kitawi / kikonyo (grafting)- Hii hufanyika kwa mimea kama miembe, parachichi.nk
KWA ELIMU ZAID KUHUSU UBEBESHAJI
NICHEKI
WhatsApp/call. 0683308173
Email. shafii.ismail09@gmail.com
0 comments: