Kiwavi ni hatua ya ukuaji wa mdudu wa oda ya Lepidoptera (wadudu kama vipepeo na nondo). Kwa kawaida hula majani. Wakitokea kwa wingi, k.m. viwavijeshi, wanaweza kuharibu mimea na hasa mashamba. Hivyo ni adui wakubwa wa wakulima.
Jinsi ilivyo kwa wadudu wengi, maisha ya kiwavi huanza kama yai. Inatoka kwa umbo la kiwavi. Baada ya muda kiwavi huwa bundo. Ndani ya bundo hugeuka kuwa kipepeo anayetoka na kutaga mayai tena. Mzunguko huo kwa jumla ni metamofosisi.
WhatsApp /call. 0683308173
Email address. Shafii.ismail09@gmail.com
0 comments: