KILIMO CHA PILIPILI MWENDOKAS
MBEGU NA JINSI YA KUSIA
Andaa kitaru chako vizuri chenye ukubwa wa mita moja kwa sita ((1 x 6) m),Ili hewa iweze kuzunguka vizuri kwenye udongo unashauriwa kutengeneza kitaru mbinuko.Kama una mbolea aina ya samadi iliyooza vizuri (Well decomposed) changanya debe 3 kwenye kitaru cha mita moja kwa sita.Hakikisha unachanganya vizuri udongo na samadi hadi ushindwe kutofautisha kati ya samadi na udongo,baada ya kuchanganya samadi na udongo sasa sawazisha vizuri,hakikisha hakuna mabongemabonge.
Kama huna mbolea ya samadi tumia DAP baada kuanda kitaru chako rushia DAP kiasi cha 180g kwa kitaru cha mita moja kwa sita au kwa lugha nyingine ni 30g kwa kila square mita moja
Baada ya kuweka mbolea tengeneza mistari inayopishana kwa umbali wa sentimita 4 na baada ya hapo sia/mwaga mbegu zako kwenye hiyo mistari NB:Usibananishe mbegu.
Baada ya kuweka mbegu kwenye hiyo mistari fukia vizuri kwa kutumia udongo laini na kisha tafuta majani makavu na tandika kitaru chako vizuri na baada ya hapo mwagilia maji ya kutosha kwa kutumia Keni ya kumwagilia.
Mbegu zitaota baada ya siku 7-10 na baada ya kuota toa majani na kama ni masika tengeneza kichanja na tandika juu ya kichanja,kama ni kiangazi unaweza kuacha kuweka kichanja.
Siku mbili baada ya mbegu kuota mwagilia maji ya kutosha na kisha pulizia Actara au dawa yoyote yenye kiambato sawa na Actara.Pulizia dawa nyingi mpaka udongo ulowane zaidi(Drenching).Pima Actara 8g/20L.
Siku 4 baada ya mbegu kuota pulizia Ridomil gold au ....pima 50g/20L. Baada ya siku 14 tangia upulizie Actara rudia kupulizia tena na vivyohivyo kwa Ridomil gold na pia rushia Yaramila winner kidogo.
Miche ya pilipili mbuzi hukaa kwenye kitaru siku 30-35 na baada ya hapo unahamishia shambani.
UPANDAJI.
Andaa shamba lako vizuri,muonekano wa shamba utategemea njia unayotumia kumwagilia.Panda kwa kuzingatia nafasi. Kutoka mmea na mmea iwe kati ya 30-60 cm na mstari na mstari iwe kati ya 70-100 cm (Kulingana na aina ya mbegu).Pandia DAP 5g /mmea.Hakikisha mbolea haigusani na mizizi au Panda miche bila mbolea mwagilia maji na kisha tengeneza starter solutions.NB:Chukuwa kilo 3 za DAP weka kwenye maji lita 200 na kisha kologa mpaka mbolea yote iyeyuke na kisha chota kwa kutumia kikombe cha chai kidogo na mwagilia miche yako aliyopanda siku hiyo,hakikisha maji yenye mbolea hayagusi majani ya miche yako...mwagilia chini kwenye udongo tu sio majani.
MBOLEA.
Siku 10 Baada ya kupanda sasa endelea kukuzia mbolea,wakati huu tumia Yaramila winner 5-10g kwa mche.NB:Usitupie juu..hakikisha mbolea unaifukia kuzunguka mmea na usiweke karibu sana na mmea,weka 4-6 cm kutoka kwenye mmea.
Na kila baada ya siku 21 weka mbolea aina ya Yaramila winner au NPK Isipokuwa wakati maua yameanza weka Yaramila nitrabo au CAN 10g /plant,na baada ya hapo utaendelea na Y-winner mpaka mwisho wa mavuno.
WADUDU
Pilipili mbuzi hushambuliwa na ;
A) Wadudu mafuta ( Aphids)
Kuwadhibiti.
Tumia Actara 8g/20L.
Au tumia wadudu wanaokula wadudu mafuta,mfano special beetles.
B) Crickets
Hawa wadudu hukaa aridhini karibu na mmea na usiku hutoka walipo jificha na kukata miche michanga.
Kawadhibiti.
Unapo andaa shamba andaa vizur ili nyumba zao zife na kuwaacha katka halu ya hatari ya kuliwa na ndege na wadudu wengine ,kama ni miche na iko kwenye tray...basi weka hizo tray juu ya kichanja.
C) Beetle.
Tuma Karate 40cm/20L.
D) Utitiri
Dawa:Tumia Dynamec au yoyote yenye Abamectin.
E) Nematodes na nk.
Tumia solvigo.
MAGONJWA.
1) Fusarium wilt (Mnyauko)
Njinsi ya kuepuka.
.Tandika shamba lako na majani makavu ili kupunguza joto.
.Ng'oa mimea yote iliyougua na choma moto mabaki.
.Epuka kusambaza ugonjwa kwa kusafisha vizur vifaa vya shamba na chini ya miguu uingiapo shambani.
.Jitahidi mimea iwe na afya nzuri kwa kuweka mbolea na maji ya kutosha.
.Pulizia dawa ya fangas kama vile ortiva.
2) Southern blight ( Sclerotium wilt)
Huu ungonjwa utaona kwenye shina china panaota fangasi weupeweupe (Whitish fungal growth on the stems of infected plant) .Majani ya chini huweza kunyauka,Huu ungonjwa hutokea muda mfupi kipindi cha joto kali.
Kuepuka/Kuzuia.
.Wakati wa kulima ..lima hadi chini sana ili hao fangasi waende chini sana ambapo mizizi haifiki.
.Mimea iliyoshambuliwa...Ing'oe yote na choma moto lakini chomea nje ya eneo la shamba.
.Pulizia Ortiva.
3) Anthracnose.
Huu ni ugonjwa wa kawaida kwenye pilipili mbuzi na huu ugonjwa huweza kukaa ardhini muda mrefu.Dalili zake utaona matunda kama kuna sehemu zinakuwa nyeusi na panajaa majimaji ...dalili hii huenea sehemu kubwa ya tunda na baadaye tunda huoza.
Kuepuka.
Kuepuka ugonjwa kujirudia musimu na musimu..Baada ya kuvuna choma mabaki yote.
.Shamba ambalo ulilima pilipili usirudie kulima pilipili mfululizo zaidi ya mara mbili...badilisha zao kwa kupanda zao ambalo sio jamii moja na pilipili mbuzi (Do crop rotation)
.Pia huu ugonjwa huweza kupitia mbegu...kwa hiyo mkulima lazima achukue mbegu kutoka kwa wakala aliyeidhinishwa na mwaminifu...mbegu hazitakiwi kutengenezwa kutoka kwenye mimea iliyoathirika na ugonjwa.
4) Bacteria.
Madoamadoa ya bacteria kwenye matunda....huweza kutokea na kusambaa haraka wakati wa joto kali na unyevu kwenye udongo.Pia huu ugonjwa huweza kuenea kupitia mbegu.
Dalili zake utaona madoamadoa ya kama brown chini ya majini na pia kwenye matunda.
Kuepuka.
.Usitengeneze mbegu kutoka kwa mimea iliyoathirika na huu ugonjwa.Nunua kutoka kwa wakala.
.Pulizia dawa yoyote copper.
5) Virusi.
Kuna aina nyingi ya virusi ambao hushambulia pilipili mbuzi.
Dalili zake ni majani kuwe ba njano na kujikunja .
Kuepuka.
.Nunua mbegu bora
.Pulizia dawa za wadudu kuanzia kwenye kitaru na kuendelea.Wadudu wanaosababisha virus sanasana na wadudu mafuta (Aphids) kwa hiyo akikisha muda wote shambani hakuna hao wadudu kwa kupulizia Actara.
NBamoja na maelezo yote hapo juu.Usikae zaid ya siku 14 bila kupiga dawa ya wadudu na ukungu/fangasi hata kama hakuna ugonjwa wala wadudu.
Mavuno.
Utaanza kuvuna baada ya siku 90 tangia uhamishie miche shambani na utaendelea kuvuna kwa muda wa miezi 6-12 kulingana na matunzo yako.
Kila wiki unavuna na kila ukivuna kwa ekari moja hutoa gunia 10-20 kulingana na huduma yako pia.
Soko na bei.
Soko la pilipili mbuzi Tz ni kubwa sana japo kuna muda zinashuka bei lakini bado mkulima anapata faida.
Bei ikipanda sana huwa Debe ni Tsh 30 000-60 000.Hii mara nyingi hutokea miezi ya 1-7 na bei ikishuka huwa Debe ni Tsh 10 000-25 000 .Hii mara nyingi hutokea miezi ya 7-12.
Changamoto
Usipozingatia maelekezo ya wataalam au wakulima wazoefu unaweza ukapata hasara kubwa
WhatsApp/call 0683308173
Email shafii.ismail09@gmail.com
0 comments: