Wednesday, 31 May 2023

SABABU ZINAZOPELEKEA ZAO LA KOROSHO KUSHUKA KATIKA UZALISHAJI NYANJA ZA KUSINI MWA TANZANIA

WhatsApp /call. 0683308173

Email. Shafii.ismail09@gmail.com

Http//wwww.kilimoniuhaiblog.blogspot.com



LEO tunaangalia SABABU za kushuka kwa uzalishaji zao hili LA KOROSHO..

Zifuatazo ni baadhi tu ya SABABU nilizofanyia utafiti

Nikagundua znapelekea kushuka kwa zao LA KOROSHO..

1.ELIMU YA UZALISHAJI

Elimu juu ya uzalishaji wa KOROSHO ni changamoto mkubwa Sana inayowakumba wakulima. Hii inatokana kukosekana kwa mabwana shamba baadhi ya maeneo hvyo mkulima hufanya kilimo kwa nadhalia tu, Bila utaalamu wa bwana shamba..

_mkulima anashindwa JINSI YA kutumia dawa.. Hii ni kwa ajili ya kukosa Elimu juu ya uchanganyaji dawa

_mkulima anakua hajui muda nzur wa kufanya palizi na muda sahihi wakuanza kutia dawa mikoroshoni

_mkulima hajui Aina za magonjwa yanayosumbua mikorosho

_pia hatambui wadudu wahalibifu wa zao LA KOROSHO

_hali kadhalika mkulima hajui vipi ayaandae mazao yake baada ya kuyatoa kutoka shambani

Hivyo Elimu inahitajika mno Tena kwa upana kuwapelekea wahusika ambao ni wakulima.

2.WADUDU NA MAGONJWA

Wadudu wahalibifu ni wadudu ambao wanazolotesha uzalishaji wa KOROSHO ambao hupelekea zao hili kushuka. SABABU wadudu hushambulia maua ya KOROSHO, hvyo KOROSHO hushindwa kufanyika kwa ukuaji wa Hilo ua ili ifikie kuwa KOROSHO

Magonjwa pia huzolotesha uzalishaji wa korosho. Kuna baadhi ya magonjwa yakivamia ktk mikorosho. Mikorosho hushindwa kabisa kufanya uzalishaji, uzalishaji huwa kidogo na kutoa korosho ambazo sio bora.

3. VIWATILIFU

Tunazungumzia viwatilifu Kuna mara mbili.

(a) ubora wa viwatilifu

(b) matumizi yasio sahihi ya viwatilifu

_ubora wa viwatilifu hili pia ni tatizo, Kuna baadhi ya makampuni huleta janja janja. Ambazo huwaletea wakulima dawa ambazo hazina viwango au ambazo zimepoteza muda. Hvyo hizi dawa zenye mfano huo haziwezi kuleta tija ya kilimo.

_mkulima akishindwa kutumia vizuri viwatilifu vitapelekea kuongeza au kupunguza vipimo. SABABU akiongeza kipimo huunguza zao na akipunguza dawa itashindwa kufanya KAZI kwa ufanisi.

4.MABADILIKO YA HALI YA NCHI

HII ni Khali ambayo haiwezi kukingika SABABU ni matokeo ambayo yako nje ya uwezo wa binadamu.

Sababu mvua, upepo, joto, au baridi hutokea kwa maamuzi ya muumba.

Ila ndo hvyo mabadiliko haya yakitokea hupelekea shughuli za kilimo nacho kubadilika.

Kwa zao LA KOROSHO baridi ikizidi Sana huwa shida katika uzalishaji wake.

5.MIKOROSHO YENYE UMRI MKUBWA

Mikorosho hupungua uzalishaji endapo itakua na UMRI mkubwa. Yaan mikorosho inakua ishazeheka ndo mana inashindwa kuzaa kutokana UMRI kuwa mkubwa Sana. Hii nayo ni tatizo linalopelekea kilimo cha korosho kushuka uzalishaji

6.AINA ZA MBEGU.

Unapoandaa shamba LA mikorosho jitahidi kuchagua MBEGU bora. Sababu mbegu zikiwa bora zitapelekea uzalishaji kuwa mzuri Sana. Lakini ukichagua mbegu ambazo si bora basi huwezi kupata mazao yalio bora ndipo kilimo cha korosho knapozidi kuzolota na kushuka uzalishaji.

7.SOKO NA TOZO

TOZO NA SOKO LA KOROSHO nalo ni changamoto kutokana na tafiti zangu nmegundua baadhi ya wakulima wameamua kuacha kilimo hiki wengine kuamua kukata kabisa mikorosho na kuamua kuanzisha kilimo kingine TOFAUTI na Mikorosho.. Baada ya kufanya nao mahojiano wengi wao walilalama kuhusu TOZO. Wanasema TOZO kuhusu uendeshaji wa korosho huwa kubwa Sana kitu amacho kinapelekea kutowanufaisha wakulima, na kuwanufaisha watu ambao hata kilimo cha korosho hata hawakijui. SOKO LA KOROSHO nalo linashuka Sana hvyo mkulima hula hasara kila mwaka akilinganisha na gharama zake za uendeshaji shamba. Haya ni malalamiko ya wakulima walioamua kubadilisha kilimo cha korosho na kuanza Aina ya vilimo vingine..

8.WAKULIMA

Tatizo lingine Linalosababisha kushuka uzalishaji ni wakulima wenyew.. Katika tafiti zangu pia nmegundua kuwa wakulima nao ni tatizo pia. Mkulima huwa na tabia ya ukaidi. Anaweza akapewa matumizi sahihi ya kiwatilifu fulani Lakini yeye akaleta ubishi usio na tija.,nakuamua kujiongeza kwa kuona kipimo alichoambiwa ni kidogo na kuhisi hakitafanya KAZI kwa Haraka. Hvyo huongeza kipimo mwisho wa siku hupelekea kuunguza zao au kusitisha kabisa uzaaji wa zao husika..

Hizo ni baadhi tu ya visababishi vya kushuka na kudholota kwa zao LA KOROSHO

Yapo mengi Sana Zaidi ya hayo yanayopelekea kushuka kwa zao hili.

Mwisho kabisa :- ukweli na uaminifu ndio utapelekea zao hili kupanda kupitia serikali, makampuni, mabwana shamba na wenyewe wakulima.. TOFAUTI na hivyo kilimo cha korosho baada ya miaka mbeleni hakitakuwepo na itabaki kuwa historia tu..

Read less
image

0 comments: