Headlines
Loading...

Wednesday, 31 May 2023

SABABU ZINAZOPELEKEA ZAO LA KOROSHO KUSHUKA KATIKA UZALISHAJI NYANJA ZA KUSINI MWA TANZANIA

WhatsApp /call. 0683308173

Email. Shafii.ismail09@gmail.com

Http//wwww.kilimoniuhaiblog.blogspot.com



LEO tunaangalia SABABU za kushuka kwa uzalishaji zao hili LA KOROSHO..

Zifuatazo ni baadhi tu ya SABABU nilizofanyia utafiti

Nikagundua znapelekea kushuka kwa zao LA KOROSHO..

1.ELIMU YA UZALISHAJI

Elimu juu ya uzalishaji wa KOROSHO ni changamoto mkubwa Sana inayowakumba wakulima. Hii inatokana kukosekana kwa mabwana shamba baadhi ya maeneo hvyo mkulima hufanya kilimo kwa nadhalia tu, Bila utaalamu wa bwana shamba..

_mkulima anashindwa JINSI YA kutumia dawa.. Hii ni kwa ajili ya kukosa Elimu juu ya uchanganyaji dawa

_mkulima anakua hajui muda nzur wa kufanya palizi na muda sahihi wakuanza kutia dawa mikoroshoni

_mkulima hajui Aina za magonjwa yanayosumbua mikorosho

_pia hatambui wadudu wahalibifu wa zao LA KOROSHO

_hali kadhalika mkulima hajui vipi ayaandae mazao yake baada ya kuyatoa kutoka shambani

Hivyo Elimu inahitajika mno Tena kwa upana kuwapelekea wahusika ambao ni wakulima.

2.WADUDU NA MAGONJWA

Wadudu wahalibifu ni wadudu ambao wanazolotesha uzalishaji wa KOROSHO ambao hupelekea zao hili kushuka. SABABU wadudu hushambulia maua ya KOROSHO, hvyo KOROSHO hushindwa kufanyika kwa ukuaji wa Hilo ua ili ifikie kuwa KOROSHO

Magonjwa pia huzolotesha uzalishaji wa korosho. Kuna baadhi ya magonjwa yakivamia ktk mikorosho. Mikorosho hushindwa kabisa kufanya uzalishaji, uzalishaji huwa kidogo na kutoa korosho ambazo sio bora.

3. VIWATILIFU

Tunazungumzia viwatilifu Kuna mara mbili.

(a) ubora wa viwatilifu

(b) matumizi yasio sahihi ya viwatilifu

_ubora wa viwatilifu hili pia ni tatizo, Kuna baadhi ya makampuni huleta janja janja. Ambazo huwaletea wakulima dawa ambazo hazina viwango au ambazo zimepoteza muda. Hvyo hizi dawa zenye mfano huo haziwezi kuleta tija ya kilimo.

_mkulima akishindwa kutumia vizuri viwatilifu vitapelekea kuongeza au kupunguza vipimo. SABABU akiongeza kipimo huunguza zao na akipunguza dawa itashindwa kufanya KAZI kwa ufanisi.

4.MABADILIKO YA HALI YA NCHI

HII ni Khali ambayo haiwezi kukingika SABABU ni matokeo ambayo yako nje ya uwezo wa binadamu.

Sababu mvua, upepo, joto, au baridi hutokea kwa maamuzi ya muumba.

Ila ndo hvyo mabadiliko haya yakitokea hupelekea shughuli za kilimo nacho kubadilika.

Kwa zao LA KOROSHO baridi ikizidi Sana huwa shida katika uzalishaji wake.

5.MIKOROSHO YENYE UMRI MKUBWA

Mikorosho hupungua uzalishaji endapo itakua na UMRI mkubwa. Yaan mikorosho inakua ishazeheka ndo mana inashindwa kuzaa kutokana UMRI kuwa mkubwa Sana. Hii nayo ni tatizo linalopelekea kilimo cha korosho kushuka uzalishaji

6.AINA ZA MBEGU.

Unapoandaa shamba LA mikorosho jitahidi kuchagua MBEGU bora. Sababu mbegu zikiwa bora zitapelekea uzalishaji kuwa mzuri Sana. Lakini ukichagua mbegu ambazo si bora basi huwezi kupata mazao yalio bora ndipo kilimo cha korosho knapozidi kuzolota na kushuka uzalishaji.

7.SOKO NA TOZO

TOZO NA SOKO LA KOROSHO nalo ni changamoto kutokana na tafiti zangu nmegundua baadhi ya wakulima wameamua kuacha kilimo hiki wengine kuamua kukata kabisa mikorosho na kuamua kuanzisha kilimo kingine TOFAUTI na Mikorosho.. Baada ya kufanya nao mahojiano wengi wao walilalama kuhusu TOZO. Wanasema TOZO kuhusu uendeshaji wa korosho huwa kubwa Sana kitu amacho kinapelekea kutowanufaisha wakulima, na kuwanufaisha watu ambao hata kilimo cha korosho hata hawakijui. SOKO LA KOROSHO nalo linashuka Sana hvyo mkulima hula hasara kila mwaka akilinganisha na gharama zake za uendeshaji shamba. Haya ni malalamiko ya wakulima walioamua kubadilisha kilimo cha korosho na kuanza Aina ya vilimo vingine..

8.WAKULIMA

Tatizo lingine Linalosababisha kushuka uzalishaji ni wakulima wenyew.. Katika tafiti zangu pia nmegundua kuwa wakulima nao ni tatizo pia. Mkulima huwa na tabia ya ukaidi. Anaweza akapewa matumizi sahihi ya kiwatilifu fulani Lakini yeye akaleta ubishi usio na tija.,nakuamua kujiongeza kwa kuona kipimo alichoambiwa ni kidogo na kuhisi hakitafanya KAZI kwa Haraka. Hvyo huongeza kipimo mwisho wa siku hupelekea kuunguza zao au kusitisha kabisa uzaaji wa zao husika..

Hizo ni baadhi tu ya visababishi vya kushuka na kudholota kwa zao LA KOROSHO

Yapo mengi Sana Zaidi ya hayo yanayopelekea kushuka kwa zao hili.

Mwisho kabisa :- ukweli na uaminifu ndio utapelekea zao hili kupanda kupitia serikali, makampuni, mabwana shamba na wenyewe wakulima.. TOFAUTI na hivyo kilimo cha korosho baada ya miaka mbeleni hakitakuwepo na itabaki kuwa historia tu..

Read less
image
VITUNGUU SWAUMU
                UTANGULIZI

Vitunguu saumu ni zao ambalo lipo katika jamii ya vitunguu na hufanana sana na vitunguu maji, zao hili linatumika sana duniani kama kiungo cha chakula na wengine hutumia kama dawa.

ASILI YAKE
Vitunguu swaumu asili yake ni maeneo ya Mediterranean na China, Asia lakini pia usitawi katika nchi za kitropik kwa hapa tanzania ustawi katika mikoa ya singida,Arusha,Iringa na Mbeya. pia utumika kama kiungo cha chakula dawa kwa binadamu na wanyama pia na pia utumika kutengeneza mafuta pia harufu yake kali ufukuza wadudu waalibifiu shambani.
hivyo shamba la vitunguu swaumu haliwi na wadudu wa halibifu sana ukiringanisha na mazao mengine.

AINA ZA VITUNGUU SWAUMU
Vitunguu swaumu vipo vya aina mbalimbali nazo ni:=
i) Antichoke – Hii kwa mbali inaonekana kama ni nyekundu lakini sio iliyokolea
ii) Soft neck – Kwa rangi ni nyeupe inatumika sana kwasababu hachukua mda mfupi shambani
iii) Silver skin – Hivi vina rangi nzuri ya silver na mara nyingi hutumiwa na wasindikaji maana vinadumu mda mrefu bila kuharibika.

HALI YA HEWA & UDONGO
Vitunguu saumu hulimwa kiasi cha mita 1800 au zaidi kutoka usawa wa bahari na mvua kiasi cha mm 1000 au zaidi na joto kiasi udongo tifutifu na mnyevunyevu na usio tuamisha maji ndio unafaa kulima vitunguu saumu.

UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Shamba linapaswa kutayarishwa mapema kabisa, lima na akikisha udongo ni tifutifu na pia unaweza kutengeneza matuta kwaajili ya kupanda weka samadi shambani wiki 2 kabla ya kupanda.

UTAYALISHAJI WA MBEGU
Mbegu ya kitunguu swaumu ni ile punje (vikonyo) inayokuwa imebanguliwa kutoka kwenye kitunguu au tunguu iliyokomaa kabisa, kiasi cha kilo 300 – 500 hutumika kwa hekari moja na inatakiwa uchague mbegu isio na magonjwa au isio dhaifu.

UPANDAJI
Tabia ya mmea wa Vitunguu swaumu humea huanza kuota kipindi cha baridi ( miezi yenye baridi), kwa Tanzania kipindi ambacho hakuna joto ni miezi ya May mpaka August, Unachukua kitunguu swaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 5 na kati ya mistari ni sentimeta 20 na kushuka chini kiwe na wastani wa inchi 2.5 . Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kung’olewa kabisa. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu swaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu. Pandia TSP kilo 40 kwa eka au kilo 100 kwa hekta.

MBOLEA
Mbolea huwekwa baada ya palizi, tumia mbolea ya kukuzia CAN au UREA. CAN kiasi cha kilo 75 kwa eka au 190 kwa Hekta au UREA kiasi cha kilo 40 kwa eka na 100 kwa hekta na palilia mara mbili au zaidi ili kuweka shamba katika hali ya usafi.

UPALILIAJI
Kuwa na juhudi ya kupalilia ili kuipa uhuru mimea kumea vizuri na kulifanya shamba lako kuwa safi, Palizi ya kwanza ifanyike mapema mara tu magugu yanapo tokeza wakati vikonyo vimesha chipua na baada ya palizi ya kwanza ndipo weka mbolea. Unaweza kupulizia dawa yakuua magugu endapo vitunguu vimeshaota  kama vile Bromoxynil ambayo uua majani mapana na fusilade uua nyasi. Mmea unapoendelea kukua  na kutoa maua yaache majani yarefuke mpaka yajikunje, ndipo utayakata ili kuongeza uzalishaji.


MAGONJWA & WADUDU

MAGONJWA
Vitunguu swaumu havishambuliwi sana na magonjo, ila magongwa yake ni kama:=
i) Fusari muozo-unasababishwa na ukungu katika majani au miziz na pia unaweza kudhibiti kwa kuchoma masalia ya mimea baada ya kuvuna
ii) Kutu ya majani-mmea unakua na vinundu vya ukngu vyenye rangi ya kahawia kama kutu katika majani tumia dawa ya ukungu  kama fungaran nabayfidan na nordox ili kuzuia
iii) Kuoza kwa vitunguu-ukungu wa rangi ya blue ufunika vitunguu na usabibisha vitunguu kuoza na utokea gharan vuna kwa uangalifu ili kuepusha michubuko  na hakikisha store ni safi
iv) Baka jani-vidonda vidogo hutokeza katika majani na badae vinakua vikubwa epuka kumwagilia maji mengi kupita kiasi na tumia mzunguko wa mazao
v) Muozo shingo-shingo kuonyesha dalili ya majimaji weka mbolea ya ntrogen kama CAN,UREA na mwagilia maji ya kutosha hasa vinapo elekea kuvunwa.

WADUDU
Wadudu kama chawa wekundu nondo na funza  wanakata miche na mizizi tumia dawa ya karate,selecron,novthin,dursban hutumika kuuwa wadudu

UVUNAJI
Baada ya miezi 6-7 tokea kupanda ndio mda muafaka wa kuvuna vitunguu swaumu kwani vinakuwa vimekomaa na majani na mashina huonesha dalili ya kukauka, ndipo viache vitunguu shambani mpaka majani yanape kukauka kabisa  ng’oa kwa mkono au jembe na pia kua muangalifu ili kuepusha kuchubua vitunguu. Kiasi cha tani 4 – 7 zinaweza kuvunwa katika heka moja.

Http//wwww.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

Read less
image

Tuesday, 30 May 2023

Pima udongo katika shamba lako mwenyewe, fahamu njia za kutambua udongo wenye rutuba

NAMNA YA KUTAMBUA UDONGO WAKO



WhatsApp-Image-20160615.jpg




Kupima udongo kwa kutumia vidole



 Chukua sampuli ya udongo kwenye kiganja cha mkono kisha ondoa mizizi, changarawe kubwa kubwa na mabaki ya mimea.

 Kanda udongo kwenye kiganja chako. Kama udongo ni mkavu sana unaweza kuulainisha kwa maji kidogo

 Fikicha udongo kwa kutumia vidole na hakikisha kila kitu kimelainika (pima ugumu); Finyanga mpira (pima uwezo wa kuundwa); zungusha kutengeneza mnyoo kisha kandamiza kurudi chini (pima mnato na uwezo wa kupasuka/kupata ufa).


Udongo wa mfinyanzi:


Mwepesi na unanata sana. Ni rahisi kufinyanga mpira na haupasuki wala kupata ufa, unaweza kutengeneza. Udongo huu unaweza kuunda bonge/donge kubwa na likakauka.


Tifutifu:


Hujishika pamoja lakini hapasuka katika vijipande vidogodogo, chembe za mchanga haziwezi kushikika.


Mchanga:


Chembe za mchanga zinashikika na kuonekana. Udongo haunati na hauwezi kufinyangwa.


Namna ya kupima udongo kwa kutumia chupa ya plastiki.
Mahitaji

1. Chupa za plastiki tatu za saizi inayolingana, zenye mifuniko na zisizokuwa na rangi ili kuweza kuona vilivyomo ndani kwa urahisi.

2. Maji safi

3. Chumvi

Hatua
 Weka udongo ndani ya chupa hadi kufikia theluthi ya chupa.

 Ongeza maji mpaka kufikia theluthi mbili ya chupa.

 Weka chumvi kidogo kisha tikisa chupa kwa nguvu kwa muda wa dakika moja kisha ziache zitulie kwa saa moja.

 Baada ya lisaa limoja, tikisa chupa tena kisha ziache zitulie kwa muda wa masaa manne.

 Baada ya masaa manne udongo utakuwa umejigawa katika matabaka hivyo unaweza kuupima: Tabaka laini kabisa la juu ni mfinyanzi, linalofuatia ni mchangatope, linalofuatia ni mchanga na mwisho kabisa tabaka lenye chengachenga ni changarawe.

 Tafuta asilimia ya kila sehemu ndogo ya udongo (mfinyanzi, mchangatope, mchanga na changarawe) kwa kugawanya unene wa kila tabaka la udongo kwa jumla ya unene wa udongo wote kisha zidisha kwa mia moja (100%).

Snapshot.png


Aina za udongo
Changarawe (gravel): chembe zenye ukubwa wa zaidi ya 2 mm

Mchanga (sand): chembe zenye ukubwa wa zaidi ya 0.02 mm lakini zisizozidi 2 mm

Chembe za mchanga huchukua nafasi ndogo ukilinganisha na mchangatope au mfinyanzi. Uwezo wa kuhifadhi maji ni mdogo sana kwenye mchanga na hali ya utendaji wa kikemia ni ndogo.

Mchangatope (silt): chembe zilizo na ukubwa wa kati ya 0.02 mm na 0.002 mm

Chembe za mchangatope huchukua nafasi kubwa zaidi ya mchanga na zina uwezo mdogo kwenye hali ya utendaji wa kikemia. Mchangatope huathirika kwa urahisi na migandamizo ya vitu vizito hivyo kuathiri uwezo uingizaji wa hewa na mzunguko wa maji kwenye udongo.

Udongo wa mfinyanzi (clay): chembe zisizozidi 0.002 mm

Chembe za udongo wa mfinyanzi huchukuwa nafasi kubwa sana na zina hali kubwa sana ya utendaji wa kikemia. Virutubishi pamoja na maji hujishikisha kwenye huu udongo lakini havipatikani mara zote kwa mimea. Udongo wa mfinyanzi unauwezo wa kutuna na hufaa kuundia vitu mbalimbali kwa sababu ya asili yake ya kunata.

Mchanganyiko wa mchanga, mchangatope na udongo wa mfinyanzi huleta udongo tifutifu (loam) wenye rutuba. Udongo huu ni mzuri na hufaa kwenye kilimo.

Umuhimu wa mboji kwenye udongo
 Kusambaza virutubishi kama vile nitrojeni (N), fosforasi (P) na salfa (S) kwenye mimea ambayo inavihitaji.

 Kushikilia na kuhifadhi virutubishi hivyo kuzuia kuchujishwa/kuondoshwa kwa rutuba kutoba kwenye udongo.

 Husaidia kushikilia chembe za udongo pamoja hivyo kukinga dhidi ya mmomonyoko wa udongo.

 Huboresha uwezo wa udongo kupitisha hewa na kuhifadhi unyevunyevu kwenye udongo.

 Huboreha uwezo wa udongo kuhifadhi maji.

 Huvipa virutubisho viumbe hai viishivyo kwenye udongo.

Rangi ya udongo na kiasi cha rutuba kilichopo
Snapshot%25284%2529.png



Namna ya kuongeza kiasi cha rutuba kwenye udongo
WhatsApp-Image-20160615.jpg


 Tumia mboji au samadi iliyochanganya na mabaki ya mazao.

 Tumia mbolea za kijani

 Badilisha mzunguko wa mazao

 Hifadhi/tunza vijidudu viishivyo kwenye udongo

 Fanya kilimo mchanganyiko na miti

 Jitahidi kuhakikisha kuwa udongo umefunikwa wakati wote

 Punguza uwezekano wa mmomonyoko wa udongo


nimeeleza kwa ufupi namna ya kupima udongo wako lakini hapo ni mwanzo tuu kwani kuna vipimo vingine vinahitaji vifaa maalumu kama kupima Ph na unyevu katika udongo wako


ni muhimu kufahamu vizuri kuhusu udongo katika shamba lako ili wataalamu waweze kufanya design na kukushauri kuhusu matumizi ya maji katika kumwagilia na pia aina ya mazao unayotakiwa kulima katika udongo husika kwani ardhi ndio inabebe chakula cha mimea

WhatsApp /call 0683308173
Email address Shafii.ismail09@gmail.com 
UMUHIMU WA MTI WA MPERA NA MATUNDA YAKE KIAFYA


UMUHIMU WA MTI WA MPERA NA MATUNDA YAKE KIAFYA

MTI wa mpera ni miongoni mwa miti ya matunda inayofahamika na wengi hapa nchini. Mti huu hutoa matunda yanayofahamika kama mapera. Asili ya mti huu ni Amerika ya Kati na Kusini licha ya kuwa siku hizi unapatikana sehemu mbalimbali nchini na duniani kote.

Mmea huo kama ilivyo mimea mingine ya matunda, hustawi zaidi katika hali ya hewa ya kitropiki. Hapa nchini Tanzania mti huu unasadikika uliletwa na wakoloni waliotoka mashariki ya mbali waliokuja Afrika kwa madhumuni mbalimbali ikiwemo suala la kueneza dini ya Kiislamu na Kikristo.

Mapera ni miongoni mwa matunda yenye kiwango kizuri cha vitamin C pamoja na vitamin A na inaelezwa kuwa kiwango cha vitamin C kinachopatikana ndani ya pera ni mara nne ya kiwango cha vitamin hiyo kinachopatikana kwenye chungwa.

Pia mapera yamesheheni virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitamin B2, E na K pamoja na madini ya chuma, ‘copper’, ‘potassium’ na ‘manganese.’

Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kuchapishwa na Jarida la Journal of Human Hypertension mwaka 1993 ulieleza kuwa tunda aina ya pera hupunguza kiwango cha msukumo mkubwa wa damu ndani ya mwili yaani 'High Blood Pressure' hii ni kwa sababu ya madini ya potassium na vitamin C ambayo husaidia kuweka sawa msukumo wa damu ndani ya mwili.

Faida haziishii kwenye tunda pekee, bali hata majani ya mti wake yanapoandaliwa vizuri huweza kuwa tiba ya magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na malaria. Majani ya mpera yanapoandaliwa kama chai, yaani yakichemshwa husaidia kuondosha sumu ndani ya mwili 'cholesterol' jambo ambalo husaidia kulinda afya ya moyo wako pia.

Majani hayo hayo ya mpera pia huwasaidia wale wenye matatizo ya kuharisha, ili kukabiliana na tatizo hilo mgonjwa wa kuhara huweza kuandaliwa maji yatokanayo na majani ya mpera ambayo yamechemshwa na kunywa kikombe kimoja asubuhi na jioni.

Vilevile majani ya mpera husaidia kutibu tatizo la vidonda vya tumbo, huku likiwa na virutubisho vingi ambavyo husaidia kuimarisha fizi na kuongeza vitamin B na A mwilini.

Majani ya mpera yenye uzito wa kilo moja yanapopondwa na kisha mgonjwa akanywa lita moja ndani ya siku nzima husaidia kukinga seli za mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Majani mateke ya mti huo yanapofungwa shingoni kwa mwenye tezi huweza kuponyesha tatizo hilo pia na mwenye jipu akifunga sehemu husika hulifanya jipu kuiva kwa haraka.

Pamoja na majani hayo kuwa msaada wa kutibu maradhi mbalimbali , halikadhalika juisi ya mapera nayo husaidia sana kutibu mgolo au bawasiri, figo na hata kuondoa mafuta katika moyo.

Kimsingi mti wa mpera karibu kila sehemu yake ni tiba kwani hata mizizi yake inapochemshwa na kutumia kwa kunywa huenda kuwasaidia wanawake wenye matatizo ya hedhi au wenye matatizo ya kutokwa na maji yenye harufu mbaya sehemu zao za siri.

Sanjari na hayo, watoto wadogo wenye matatizo ya kutopata choo zaidi ya siku mbili, wakinyweshwa maji ya majani hayo baada ya kuchemshwa huwasaidia kuondokana na shida hiyo, lakini ni vyema kuwasiliana na wataalam wa tiba asili kabla ya kuamua kutumia majani hayo kama tiba kwa mtoto.
WhatsApp /call 0683308173
Email address Shafii.ismail09@gmail.com 
KIJUE KILIMO CHA MAHARAGE
KILIMO BORA CHA MAHARAGE

KILIMO BORA CHA MAHARAGE : Maharage ni zao jamii ya mikunde ambalo hulimwa kwa ajili ya kuliwa kama mboga au futari. Pia majani yake huliwa kama chakula cha mifugo na binadamu pia. Maharage hulimwa kwa kwa wingi Mbeya, kigoma, arusha, moshi, morogoro na mikoa mingineyo.

 

HALI YA HEWA

Hustawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 1000 hadi 2000 kutoka katika usawa wa bahari . Pia yanaweza kulimwa pungufu ya mita 1000 au zaidi ya mita 2000 kutoka usawa wa bahari.

Maharage huhitaji mvua ya kutosha katika kipindi cha upandaji na ukuaji pia. Maharage pia Huitaji unyevu kidogo kipindi cha kuweka maua na ukavu kipindi cha kukomaa na kukauka vitumba.

 

AINA ZA MBEGU BORA ZA MAHARAGE

Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za maharage kama vile canadian wonder, uyole, SUA, ilonga na lyamungo.

 

UPANDAJI

Maharage hupandwa mwishoni mwa msimu wa mvua kuepusha kunyeshewa kipindi cha uekaji maua. Yanawezwa kupandwa mwezi Februari, machi, aprili inategemea mvua katika eneo lako zinaisha mwezi gani.

Fukia mbegu zako katika shimo kwa vipimo vya sm 2.5 hadi 4 katika ardhi kutegemea na aina ya udongo shambani kwako.

UPANDAJI WA MAHARAGE
UPANDAJI WA MAHARAGE

 

 

NAFASI YA UPANDAJI

Maharage yapandwe kwa nafasi ya sentimeta 40-60 mstari hadi mstari na sentimeta 8 -15 shina hadi shina

 

MBOLEA

Unaweza kupanda katika shamba lililotawanywa mbolea ya samadi.

Pia uanweza kwa uzuri zaidi kupandia mbolea za viwandani kama vile TSP  kwa kiasi cha kg 50 -100 kwa ekari.

Wakati wa mmea kuanza kuweka maua unaweza kutumia mbolea ya N.P.K au SA au Kwa Kiasi Kidogo CAN au UREA

Angalizo Mbolea hizi zikizidi maharage huwa na majani mengi kuliko maua na kusababisha mavuno kuwa machache.

 

UPALILIAJI

Upaliliaji inabidi ufanyike mapema mara tuu maharage yanapoota na mara baada ya shamba kuwa na magugu.

Palizi ya kwanza inaweza kufanyika Kati ya siku 8-12 baada ya mmea kuota na palizi ya pili ifanyike siku ya 20- 30 baada ya palizi ya kwanza. Kufanya hivi husaidia kuyalinda maua ya maharage yako yasipukutike wakati wa palizi hakikisha unaepuka palizi kipindi cha uwekaji maua.

 

WADUDU

Funza wa maharage ni wadudu wanaoshambulia mimea michanga ya maharage. Funza wa maharage hawa huweza kusababisha uharibifu hadi kufikia asilimia 100 kufuatana na hali ya hewa-unyevu kidogo, rutuba kidogo, kuwepo kwa maotea ya aina ya maharage na magonjwa kwenye udongo, kurudia kupanda zao la maharage kila msimu na aina ya maharage.

FUNZA WA MAHARAGE
FUNZA WA MAHARAGE

 

NJIA NZURI YA KUDHIBITI FUNZA WA MAHARAGE NI :-

  1. Kupanda mapema
  2. Kupakaza mbegu dawa kama endosufan, Acephate, Murtano kabla ya kuoanda mbegu ardhini. Kufanya hivi kutasaidia  kuzuia funza wa maharage na visababishi vya kuozesha mizizi.

Pia maharage yanaweza kushambuliwa na wadudu mbalimbali kama vile nzi weupe wa maharage na wengineo ambao wanweza kuzuiwa kwa kutumia dawa mbalimbali za wadudu

 

MAGONJWA

Magonjwa maarufu ni adui katika ukuaji maharage, madoa pembe, kutu, magonjwa yanayosababishwa na bacteria na virusi. Mbegu iliyoambukizwa, udongo na takataka za maharage ni vyanzo vikubwa vya uambukizaji kwa magonjwa yote isipokuwa ugonjwa wa kutu ya majani.

MAGONJWA YA MAHARAGE
MAGONJWA YA MAHARAGE

 

 

UVUNAJI

Maharage huvunwa mara tu yanaponza kukauka na kabla vitumba havijapasuka. Ng’oa mashina ya maharage na usupige kuyaondoa katika vitumba vyake.

Katika ekari moja unaweza kupata Kg 600 hadi 1200 za maharage

 

KUHIFADHI

MAHARAGE
MAHARAGE

Baada ya kuyapiga na kupeta kuondoa uchafu yaanike juani kwa siku kazaa kuhakikisha yamekauka na hayana unyevu unaoweza kusababisha yapate fangasi.

Yahifadhi katika magunia, kama yatakaa muda mrefu bila kuliwa basi hakikisha unayahifadhi kwa kutumia dawa za kuulia wadudu kama vile Shumba, Kama vile ACTELLIC DUST au MALATHION. Au Tumia mifuko maalum ya kuhifadhia nafaka. Mifuko hii huwa na maalumu ambayo husaidia kuzuia wadudu waalibifu

WhatsApp /call 0683308173

Email address Shafii.ismail09@gmail.com 

kiwavi ni nini????

 Kiwavi ni hatua ya ukuaji wa mdudu wa oda ya Lepidoptera (wadudu kama vipepeo na nondo). Kwa kawaida hula majani. Wakitokea kwa wingi, k.m. viwavijeshi, wanaweza kuharibu mimea na hasa mashamba. Hivyo ni adui wakubwa wa wakulima.

Kipepeo na hali za kiwavi cha Schizura concinna.
Kiwavi cha hatua ya tano cha Opodiphthera eucalypti.

Jinsi ilivyo kwa wadudu wengi, maisha ya kiwavi huanza kama yai. Inatoka kwa umbo la kiwavi. Baada ya muda kiwavi huwa bundo. Ndani ya bundo hugeuka kuwa kipepeo anayetoka na kutaga mayai tena. Mzunguko huo kwa jumla ni metamofosisi.


WhatsApp /call. 0683308173

Email address. Shafii.ismail09@gmail.com

Monday, 29 May 2023

POWER TILLER

 8. POWER TILLER


Power tiller kwa jina jingine inaitwa walking tractor, inafanya kazi kama tractor tu hebu rejea kazi za tractor hapo juu isipokuwa power tiller inafanya kazi ndogo ndogo sio kama tractor.
power tiller.jpg

fig no 8 walking tractor, power tiller

HITIMISHO
Kuna mashine nyingi sana ambazo zinatumika katika kilimo na sijazitaja, nimetaja vifaa vya msingi vya shambani kwanza, kuna vifaa kama vile matela ya matrekta , machine za kupukuchua mahindi, kukoboa mpunga na nyingine nyingi. Kwa leo ninaishia hapa naomba uwe karibu na uzi huu nitakuwa nina update mara kwa mara bila kusahau kwa ushauri au manunuzi ya vifaa mbalimbali piga simu 0683308173
Email shafii.ismail09@gmail.com
COMBINE HARVESTER

 7. COMBINE HARVESTER

Hii ni machine ambayo inafanya kazi ya kuvuna, inaitwa combine harvester kwa sababu inafanya kazi zaidi ya moja katika kuvuna, kwa mfano katika kuvuna mahindi itakata mahindi inayatoa maganda mahindi halafu inayapukuchua kwa wakati mmoja. Combine harvester inaweza ikawa ni machine maalamu kama ilivyo kwenye picha, hapo chini au inaweza ikawa kwa mfumo wa implement(yaani kama kifaa chenye uwezo wa kuvuna lakini kinafungwa kwenye tractor, kama unakumbuka mara ya kwanza kabisa nilikuambia kuwa tractor lina linafanya kazi ya kuvuna)
combine harvester.jpg