Email shafii.ismail09@gmail.com
WhatsApp /call 0683308173
Website http//www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com
Minyoo fundo ni wadudu wadogo wasioonekana kwa macho. Huishi kwenye udongo na au mizizi. Vifundo huonekana kwenye mizizi ambavyo huzuia mtiririrko wa maji na virutubisho kwenye mmea. Hali hii husababisha mimea kunyauka, hususani wakati wa kiangazi. Mimea hudumaa, kubadilika rangi kuwa njano na kushindwa kuchukua virutubisho ardhini, hatimaye kuwa na matunda machache.
Habari tangulizi
Minyoo fundo huishi tu kwenye udongo au na mizizi ya mmea. Vifundo vyake hukwamisha mtiririko wa maji na virutubisho kwenye mmea.Hata hivyo ni rahisi kuzuia kuliko kuponya mimea iliyoathirika.
Usimamizi
- Pandikiza miche yenye afya isiyoshambuliwa na minyoo fundo.
- Panda mbegu kinzani dhidi ya minyoo fundo (mfano. Tengeru 97; Cal-J, Kentom, Meru, Roma VFN).
- Tumia kilimo mzunguko kwa mazao yasiyoshambuliwa na minyoo fundo (mfano, bangi mwitu, Marejea, jamii ya kabichi, mtama). Angalizo: bangi mwitu hunaweza kuvuta Vithiripi.
- Wakati wa kuandaa kitalu, choma moto juu ya kitalu au mwaga maji yenye moto juu ya kitalu ili kuangamiza minyoo fundo kama ilikuwa kwenye udondo. Au ondoa udongo wa juu kisha weka mbolea ya komposti.
- Badilisha eneo la kitalu kila msimu.
- Tumia kiasi cha kutosha cha mbolea za asili.
- Tifua shamba wakati wa kiangazi ili minyoo fundo ikaushwe na jua.
- Katakata bangi mwitu sambaza shambani kisha tifulia chini. Angalizo: Mbangi mwitu hupunguza kuota kwa mbegu kitaluni.
- Panda mazao yasiyoshambuliwa na minyoo fundo kwa mzunguko wa miaka miwili hadi mitatu. (mfano: bangi mwitu, marejea na mazao jamii ya kabichi).
- Matumizi ya mwarubaini hupunguza idadi ya minyoo fundo shambani (1 kg / 10 m2).
- Viuatilifu vya kudhibiti minyoo fundo vina sumu kali, hivyo ni hatari kwa wakulima, walaji na mazingira.
- Viuatilifu vya kufukiza kwenye udongo haviruhusiwi katika kilimo husishi.
0 comments: