Okoa fedha na linda afya za walaji kwa kutumia viuadudu vya asili kudhibiti wadudu shambani kwako.
Fuata hatua zifuatazo kutengeneza kiuadudu kwa kutumia mbegu za mti wa mwarobaini.
Kwanza tafuta mwarobaini wenye matunda ambayo yana rangi ya kijani na manjano na kisha vuna matunda yenye rangi ya majano hayo ndiyo matunda yaliyokomaa au kuiva.
Vuna matunda hayo na yaanike kwenye jua kwa takriban siku 3 hadi 4 ili yakauke.
Hakikisha matunda yanageuka na kuwa na rangi ya kahawia.
Ponda ponda hayo matunda ili kutenganisha ganda la juu na mbegu bila kuvunja mbegu ya ndani.
Kisha pepeta ili kutenganisha maganda na mbegu au kiini cha ndani.
Baada ya hapo chambua mbegu nzuri na zilizokomaa unashauriwa kuchagua zile zenye rangi nyeusi zinafaa zaidi zile zenye rangi nyeupe unashauriwa kuziacha.
Weka mbegu ulizo chagua kwenye chombo kisha ziponde mpaka ziwe unga mlaini
Chukua unga wako na changanya na maji safi.
Uwiano mzuri wa uchanganyaji ni gramu 350 za unga wa mbegu za mwarobaini kwa lita 10 za maji safi.
Acha mchanganyiko utulie kwa masaa 24 kabla ya kutumika.
Chuja mchanganyiko huo kuondoa chembe ndogo zinazoweza kuziba Kichujio cha kinyunyizi au solo
Baada ya hapo kiuadudu chako kitakua tayari kwa matumizi.
Kinyunyizi chenye ujazo wa lita 15 kinapaswa kitumike kwenye eneo la takribani mita za mraba 400
Mawasiliano...
Whatsapp/call 0683308173
EMAIL. shafii.ismail09@gmail.com
website. Http//www.kilimoniuhai.blogspot.com
0 comments: