Wakulima wengi wamekuwa wakisumbuka saana huhusiana na Tatizo hili. Na mara nyingi tumekuwa tukipigiwa simu kuulizwa tu kuhusiana na tatizo hili.
Hivyo ili kusaidia wakulima wote nchini; makala hii ambayo ni elimishi na yakitaalamu itafafanuwa kiufupi kuhusiana na tatizo hili na kubainisha namna ya kukabiliana nalo.
Habari Mpendwa msomaji wa makàla zetu za kilimo ni uhai tuko hapa kupeana elimu ya kilimo kwa ujumla
Mara nyingi kujikunja kwa majani ya mmea wa nyanya (kujikunja kuelekea juu au chini) husababishwa na Hali ya mazingira, kemikali, wadudu na magonjwa.
KUJIKUNJA KUNAKOSABABISHWA NA HALI YA KIMAZINGIRA.
Hii ni hutokea mara nyingi saana kwenye zao la nyanya na pilipili Hoho; husababishwa na Joto kali na umwagiliaji usio yakinifu.
Mkulima hapaswi kutishika/kupata hofu kutokana na hali hii kwasababu haidhuru wala kuathiri mavuno.
Hali hii Huendelea kwa siku kadhaa na hukoma mara tu Hali ya hewa inapokaa sawa.
Mmea hukunja majani yake (Leaf roll) ili kupunguza uso wa majani (leaf surface) kukabiliana na hali ya upungufu wa maji.
USHAURI: Mkulima ahakikishe anamwagilia maji ya kutosha na kulainisha udongo ili maji yafike kwenye mizizi yote.
Kujikunja kunakosababishwa na mazingira ya joto au upungufu wa maji |
Kujikunja kunakosababishwa na mazingira ya Joto au upungufu wa maji |
KUJIKUNJA KUNAKOSABABISHWA NA WADUDU NA MAGONJWA.
Uwepo wa wadudu waharibifu wanaofyonza kwenye majani kama vile kimamba, Vithiripi na vipepeo weupe, husababisha kueneza magonjwa ya virusi.
Magonjwa ya virusi hayana tiba Mara yanapoingia na yanaathiri mavuno kwa kiwango kikubwa.
Majani yalioathiriwa na virusi kujikunja kwake ni tofauti na kujikunja kwa majani kulikosababishwa na mazingira.
Kujikunja kwake huambatana na uvimbe uvimbe mdogo mdogo kwenye majani (leaf curling)
Pia kwenye Ugonjwa wa batobato (Tomato mosaic Virus) mishipa ya jani la Nyanya (leaf veins) kwa chini huwa na rangi ya zambarau (purple) kwa mbali.
Ugonjwa mwengine wa virusi (Tomato yellow leaf curl virus- TYLV) ambao huwa na dalili ya uwepo wa rangi ya umanjano kwenye majani.
Tomato yellow leaf curl virus |
Tomato mosaic virus |
Dhibiti wadudu wasumbufu na waharibifu kwa kutumia viuatilifu sahihi mara tu ugunduapo uwepo wao.
Tumia Dudumectin, Duduacelamectin, Snowthunder, au liberate kuwadhibiti wadudu waharibifu
.
Na tatizo hili sio kwa nyanya tu hukumba Hadi mazao mengine ,kama bamia,bilinganya, maharage,kunde.
Mawasiliano
Whatsapp/call 0683308173
Whatsapp/call 0683308173
EMAIL. shafii.ismail09@gmail.com
website. Http//www.kilimoniuhai.blogspot.com
0 comments: