Mchungwa ni jamii ya mlimao, lakin hustawi zaidi ukandawa pwani wenye joto kiasi, mvua zaidi na udongo wenye rutuba. Hapa Tanzania mikoa kama Pwani, Dar es salaam, Morogoro, Mtwara,Tanga , na Lindi kinafanyika kilimo hiki. Ulaji wa tunda la mchungwa huongeza vitamini kwenye mwili wa binadamu.
Hali ya hewa.
Matunda mengi aina ya citrus kama machungwa unatakiwa kukuza maeneo yenye joto la nyuzi joto 15 5c - 29c.
Kuandaa mbegu.
Ili kupata mbegu za mchungwa unatakiwa kukusanya mbegu za mlimao kutoka katika malimao yaliyokomaa na inatakiwa yawe yameiva katika mti, kinachofuata ni kausha mbegu zake na baada hapo toa ganda la nje ili ziweze kuota vizuri.
Kuandaa kitalu.
Tengeneza kitalu chako vizuri kwa kutumia jembe, kisha changanya na mbolea za mboji au samadi baada ya kukauka vema mwaga mbegu zako na uzifukie kwa udongo kiasi cha nusu sentimita, kisha mwagia maji kila siku na baada ya wiki 3 – 6 mbegu zitaanza kichipua, baada ya miche kufikia kiasi cha sentimita 3 – 5, miche ihamishwe kwenye viroba zenye udongo wenye mbolea ya kutosha na viwekwe kwenye kivuli kiasi.
Kuunga miche.
Miche ikifikia urefu wastani wa sentimita 30 – 45 huungwa ili kupata michungwa. Kwa Tanzania kuna aina mbili kuu za michungwa ambazo ni Jaffer na Valencia.
Jaffer ni rahisi kuunga sababu vikonyo vyake ni vikubwa na viko wazi kwenye miti, miti yake ni mikubwa na inazaa sana lakini huathirika sana na jua likiwa kali na matunda yake huanguka, pia machungwa yake hukua kwa haraka sana ila soko likiwa baya huishia shambani kwa kuanguka.
Vlencia ni miti ya wastani , vikonyo havipo wazi kwa hiyo huwapa kazi waungaji (hawaipendi) ina uzao wa wastani na inakaribia ukame na matunda yake hayaivi haraka.
Upandaji.
Andaa shamba lako kwa kuchimba mashimo,weka mbolea na subiri msimu wa mvua, miche ipandwe mara tu baada ya mvua za kwanza kunyesha.
umbali wa kupanda miche ya machungwa iwe ni mita 8 * 8 kwa Jaffer na mita 5 * 8 kwa Valencia.
Palizi ifanyike si chini ya mara 2 – 4 kwa mwaka na miche ikifikisha miaka 3 unaweza ukasafishia miaka mitatu unaweza ukasafishia visahani na kufyeka sehemu nyingine. Kwenye mbolea weka samadi iliyoiva debe moja hadi mbili kwa shimo, changanya mbolea na udongo wa kwanza kutoka shimoni.
Uzao.
Kuanzia miaka mitatu miche itaanza kutoa maua na kuzaa na huchanganya kuzaa baada ya miaka mitano, miche huendelea kuzaa hadi kufikia miaka mitano 25 – 30 tangu kupandwa.
Magonjwa na wadudu katika michungwa.
Magonjwa.
1.Vidonda katika shina .
Huletwa na aina fulani ya ukungu. Dalili za ugonjwa huu nikutokea sehemu ya shina ambayo hubadilika rangi.
Dalili; Huongezeka ukubwa na baadae kutoa utomvu.
Kudhibitisha; Hutokea sana sehemu iliyo na udongo ambao huatamisha maji.
Husababishwa na virusi ambavyo husambazwa na chawa weusi.
Dalili; Sehemu ya shina hunyauka na ndani yake hutokea mipasuko pasuko,kasha mmea hudhoofika polepole na kutoa matunda madogo madogo, na majani hubadilika ghafla na kuwa ya njano.
3.Ugonjwa wa kutobadilika rangi kwa machungwa yanapokomaa.
Hutokea hasa kwenye sehemu za miinuko ya kati na kusambazwa na vidudu viitwavyo psyllids, na vile vile kwa kuchukua vikonyo na kubebeshea kutoka kwenye miti inayoonyesha dalili za ugonjwa.
Dalili; Hutokea mabaka ya njano kwenye majani, pia matunda huwa ya ukali nay a njano sana.
KUZUIA:
Sehemu ambazo ugonjwa unaweza kutokea angalia wadudu kama chawa. Hakikisha wadudu hawa hawashambulii miche kwenye kitalu. Wakiwepo, majani huonyesha kujikunja kwa kuweka mafundo sehemu ya juu. Vilevile epuka kuchukua vikonyo kutoka kwenye miti yenye dalili za ugonjwa huu.
WADUDU:
i. Wadudu mafuta (aphids).
Hawa ni wadudu weusi ambao hukaa kwenye majani ya mimea wakizaliana na kufyonza virutubisho vya mmea, nah ii pia husababisha mmea kudumaa na kutoa mazao duni.
Kuzuia:
Tumia kiuwa wadudu (insectside).
ii. Nzi weupe (white fly).
Hawa ni wadudu ambao hukaa kwenye majani ya mimea wakizaliana na kufyonza virutubisho vya mmea, na hii husababisha mmea kudumaa na kutoa mazao duni.
Kuzuia:
Njia ya kiusalama zaidi ni kwa kupandisha shambani wadudu aina ya Cales noacki ambao huwala hawa nzi weupe na kuzuia kusambaa kwao.
Kuvuna
Machungwa huvunwa kwa njia ya mikono au kwa kutumia kikapu cha kuvunia na baada ya miezi 3 – 4 huwa tayari kuvunwa.
Hifadhi
Machungwa huhifadhiwa kwenye ghala safi lenye kuruhusu hewa. Ghala lijengwe nje ili kuruhusu hewa safi ili yasioze.
Email shafii.ismail09@gmail.com
WhatsApp /call 0683308173
0 comments: