Sunday, 30 July 2023

Kilimo cha maboga

 Email address shafii.ismail09@gmail.com

WhatsApp /call 0683308173

Website http//www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

MABOGA

Boga ni zao ambalo mmea wake unakuwa kwa kutambaa na ni la mviringo, ngozi yake ni nyororo na rangi yake ni ya njano inayoelekea kwenye rangi ya chungwa au rangi ya kijani. Katikati ya boga kuna mbegu na massa, Boga lipo katika jamii ya Cucurbita pepo.


Asili yake

Asili ya boga ni Amerika kaskazini, maboga yamekuwa yakipandwa kwaajili ya biashara na kwaajili ya chakula. Kwa sasa maboga yamekuwa yakilimwa maeneo mbalimbali duniani, Antarctika pekee ndiko maboga hayawezi kustawi. Mataifa yanayozalisha maboga kwa wingi ni Marekani (USA), Canada, Mexico, India, and China.


Hali ya hewa & udongo

Maboga yanahitaji joto la wastani kutoka kwenye jua, pia eneo ambalo halituamishi maji udongo wake uwe na pH kati ya 6.0 – 6.8. Pia udongo uwe na joto inchi tatu (sm 7.6) kushuka chini angalau nyuzi 60 °F (15.5 °C), maboga yatadhoofika kama maji yatakosekana.


Utayarishaji wa shamba

Shamba litayalishwe kwa umakini bila kuwa na sehemu ya kutuamisha maji maana mmea wa maboga na maboga yenyewe hutambaa chini, tumia jembe la ng’ombe, trekta, jembe la mkono au pawatila, changanyia mbolea za asili (samadi au mboji) na udongo ili kurutubisha shamba.


Utayarishaji wa mbegu

Mbegu za maboga zinatoka ndani ya maboga, kuna mbegu zilizoboreshwa (za kisasa) na za asili, andaa mbegu mapema wiki moja au mbili kabla ya kupanda.


Upandaji

Maboga hupandwa kwa kufukia mbegu sentimita 1 au 2 chini ya udongo , panda mbegu 2 kila shimo. Pia panda umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 – 2 kutoka mstari hadi mstari.


Matandazo (mulches)

Kwasababu ni zao linalotambaa basi lazima tuangalie namna ya kutandaza, weka nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika ardhi. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.


Mbolea

Katika matumizi ya mbolea yanatofautiana kutokana na mbegu, Lakini tumia mbolea za asili (samadi au mboji) ili kuongeza rutuba kwenye udongo, ukihitaji kutumia mbolea za viwandani weka kiasi sana, labda eneo hilo kama hakuna rutuba, mbolea ya NPK inaweza tumia.


Upaliliaji & unyevu

Palilia shamba nyasi zinapoanza kuota, pia safisha shamba ili kuondoa wadudu. Shamba la maboga linatakiwa liwe na unyevunyevu kila mara ili maboga yaweze kustawi vizuri yasidumae.


Uvunaji

Maboga hukomaa baada ya siku 95 mpaka 120, ili kujua kuwa boga lako limekomaa unaangalia kikonyo, kikonyo cha boga kinapoteza maji na kinaanza kuwa kikavu.



Saturday, 29 July 2023

Kilimo cha viazi vitamu

 Kilimo-cha-viazi-vitamu

Email shafii.ismail09@gmail.com 

WhatsApp /call 0683308173 

Website http//www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com


KILIMO CHA VIAZI VITAMU 

Zao hili hustawi maeneo mengi Nchini Tanzania. Viazi hustawi vizuri katika maeneo ya tambarare yenye udongo tifutifu, unaoruhusu maji kupenya kwa urahisi. Udongo wa mfinyazi na wenye kokoto nyingi haufai kwani huzuia mizizi kupenya na kupanuka.



Utangulizi
Kilimo cha Viazi Vitamu ni muhimu sana kwani viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi katika jamii ya ki-Tanzania. Zao hili ni moja kati ya mazao ya kinga ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame. Viazi vitamu asilia yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Morogoro, Kagera, Arusha na Ruvuma.

Matumizi
Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa katika njia mbalimbali kama vichembe, na Matobolwa. Pia Unga wa viazi vitamu hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati, tambi na Juice. Majani ya viazi huliwa kama mboga (matembele) pia hutumika katika kutayarisha mboji.

Aina
Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni. Hapa nchini Tanzania aina zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega, Karoti C, Mwananjemu, Ali mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli, Sinia, Vumilia na Polista.

Uzalishaji
Zao hili hustawi maeneo mengi Nchini Tanzania. Kilimo cha Viazi Vitamu kinakubali vizuri zaidi katika maeneo ya tambarare yenye udongo tifutifu, unaoruhusu maji kupenya kwa urahisi. Udongo wa mfinyazi na wenye kokoto nyingi haufai kwani huzuia mizizi kupenya na kupanuka. Shamba jipya litayarishwe vizuri kwa kufyeka vichaka na kung’oa visiki. Majani yafukiwe wakati wa kutengeneza matuta ili kuongeza rutuba ya udongo.

Kupanda-viazi-vitamu


Viazi vipandwe kwa kutumia marando (mashina ya viazi) yenye urefu wa sentimita 30 kwa mavuno bora. Inashauriwa kutumia sehemu ya juu ya shina kwa mavuno zaidi. Marando yapandwe katika umbali wa sentimita 25 hadi 30 kutoka mmea hadi mmea na sentimita 60 hadi 75 kutoka tuta hadi tuta. Viazi pia vyaweza kupandwa kwa kutumia viazi vyenye afya vyenye uzito wa kati ya gramu 20 hadi 30. Hata hivyo inashauriwa kutumia marando ili kupata mavuno zaidi na kuepuka kuenea kwa magonjwa.

Kutunza shamba
Ni muhimu kupalilia shamba katika miezi miwili ya mwanzo ili kuupa mmea nguvu ya kutambaa vizuri. Baada ya muda huo, viazi huweza kufunika ardhi na hivyo huzuia uotaji wa magugu. Mashambulizi ya wadudu kama vile kipepeo, mbawa kavu, fukusi na minyoo fundo ni miongoni mwa changamoto zinazokikabili kilimo cha viazi vitamu. Pia hushambuliwa na magonjwa yakiwemo magonjwa yanayotokana na virusi kama Sweet Potato Chlorotic Stunt virus (SPCSV). Magonjwa na wadudu yaweza kudhibitiwa kwa kuzingatia usafi wa shamba, kubadilisha mazao, na kuzingatia udhibiti sango.

Uvunaji
Uzuri wa kilimo cha Viazi vitamu ni kwamba huchukua mda mfupi sana kukomaa, hivyo kumlipa mkulima mapema kabisa. Kwa kawaida huwa tayari kuvunwa miezi mitatu hadi minne tangu kupandwa kutegemeana na hali ya hewa. Viazi vinaweza kuvunwa kidogo kidogo kwa kutumia mikono, vijiti, jembe, au rato kadri vinavyohitajika. Aidha inashauriwa viazi visiachwe ardhini muda mrefu bila kuvunwa kwani vitakomaa sana na kuwa na nyuzi, na hivyo kuharibu ubora wake. Pia kuacha viazi muda mrefu hukaribisha mashambulizi ya wadudu kama fukusi na kuoza. Kwa maeneo makubwa zaidi, inashauriwa kutumia mashine ya kukokotwa na ng’ombe. Uvunaji ufanywe kwa uangalifu ili kuhakikisha viazi visikatwekatwe wala kuchubuliwa wakati wa kuvuna. 

Uvunaji-viazi-vitamu


Mavuno ya viazi hutofautiana kulingana na aina, hali ya hewa, na udongo. Mavuno ya viazi yanakadiriwa kufikia tani 20 kwa hekta. 

Tuesday, 25 July 2023

KITALU CHA MBOGA MBOGA

 Email shafii.ismail09@gmail.com 

 WhatsApp/call  0683308173

Website http//www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

 Kitalu ni nini?

Kitalu ni sehemu ambayo miche huoteshwa na kutunzwa kabla ya kupandikiza bustanini / shambani.

Ni muhimu kujua jinsi ya kuandaa na kutunza kitalu cha miche ya mboga mboga kwa sababumazao mengi ya mbogamboga huhitaji kuanzia kitaluni ili yaweze kufanya vizuri shambani / bustanini.

Baadhi ya mazao ya mbogamboga yanayo hitaji kuanzia kitaluni ni kama vile nyanyapilipili hoho,vitunguu, kabichi, nanasimatango, n.k.

Makala hii ambayo naamini itakuwezesha kujua nini cha kufanya ili ukuze miche bora utakayopandikiza kwenye shamba lako.

 

Aina za Vitalu vya miche ya Mbogamboga

Kuna aina tofauti za vitalu ambavyo vinaweza kutumika kukuzia miche ya mboga. Njia inayotumika na wakulima wengi wa Tanzania ni ile ya  (1) kutumia udongo wa asili, yaani kuandaa tuta / jaruba la kitalu karibu na shamba / bustani. Vilevile kuna kitalu ambacho huanzia katika (2) tuta la mchanga (ulioletwa) au matrei ya plastikina baadae miche kuhamishiwa katika viriba vyenye udongo wenye rutuba au matuta. Kitalu cha kwenye viriba hutumika sana katika kuzalisha miche ya mbogamboga kwa ajili ya kuuza.

Faida za kukuza miche Kitaluni

Kitalu ni muhimu katika kilimo cha mboga mboga kwa sababu zifuatazo;

  1. Ni rahisi kutunza na kuiangalia miche michanga kwa uangalifu zaidi inapokuwa kitaluni kuliko inapokuwa shambani.
  2. Kupanda mbegu kwenye kitalu humpatia mkulima nafasi ya kuchagua miche  mizuri yenye afya kwa ajili ya bustani yake kuliko pale anapopanda mbegu moja kwa moja shambani.
  3. Kitalu husaidia kuepuka matatizo kama vile ya mbegu kushindwa kuota ambayo husababisha shamba kuwa na mashimo tupu yasiyo na mimea.
  4. Kitalu hutumia sehemu ndogo kutunza miche ambayo huweza kupandikizwa katika eneo kubwa.

UCHAGUZI WA ENEO LA KITALU

Ni muhimu kuchagua eneo sahihi kwa ajili ya kuandaa kitalu cha mboga ili kurahisisha matunzo ya miche katika kitalu. Eneo kwa ajili ya kuandaa kitalu inashauriwa liwe na tabia zifuatazo:

  1. Eneo liwe na urahisi wa kupata maji ili kurahisisha umwagiliaji wa miche kitaluni.
  2. Eneo lisiwe tambarare sana au lenye mwinuko mkali.
  3. Eneo liwe na udongo mzuri wenye rutuba na usiotuamisha maji.
  4. Eneo liwe na mwanga wa jua wa kutosha.
  5. Eneo lisiwe na historia ya mashambulizi ya magonjwa na wadudu wanaoshambulia miche michanga au wanyama waharibifu kama vile panya tumbili n.k.
  6. Eneo lisiwe mbali sana na shamba kurahisisha uhamishaji wa miche kutoka kitaluni kwenda shambani wakati wa kupandikiza.

JINSI YA KUANDAA KITALU

Zifuatazo ni hatua za Kuandaa Kitalu cha miche ya mbogamboga

  • Kusafisha eneo na kukatua

Safisha eneo la kuandalia kitalu kwa kufyeka vichaka na kuondoa magugu kisha katua udongo wa kutosha mita za mraba 10.

 

  • Kuchoma udongo

Choma udongo wa kitalu kwa muda wa dakika 40 hadi saa moja katika pipa la bati au nyunyizia dawa katika udongo kuua vimelea na wadudu walio katika udongo. Vilevile unaweza kuchoma udongo kwa kutumia plastiki maalum jeusi (plastic mulch) au kuchoma nyasi juu ya udongo wa kitalu.

 

  • Urutubishaji wa udongo

Rutubisha udongo kwa kuchanganya na samadi iliyoiva vizuri kiasi cha debe mbili. Ukikosa mbolea ya samadi unaweza kutumia mbolea ya kupandia aina ya DAP kwa kuweka gramu 200 ambazo unaweza kukadilia kwa kuweka maganda nane ya kiberiti yaliyo jaa mbolea. Inapendekezwa zaidi kutumia mbolea za asili kama samadi katika kitalu kuliko mbolea za viwandani. Vilevile kuharakisha ukuaji unaweza kuyunyizia mbolea ya maji aina yabooster siku kumi na nne tangu mbegu kuota.

 

  • Kutengeneza Tuta

Tengeneza tuta la upana wa mita 1, urefu wa mita 10 hadi 12 lililoinuliwa katika kimo cha sentimita 15 na kulisawazisha vizuri. Hakikisha upana wa tuta ni mita 1 na si vinginevyo ili kurahisisha uhudumiaji.

 

  • Kupanda / Kusia Mbegu Kitaluni

Kuna njia mbili za kusia mbegu kitaluni, nazo ni kama zifuatazo:

(i) Kupanda kwa mstari

Kupanda mbegu kwa mstari chora vifereji vyenye kina cha sm 2 mpaka 3 juu ya tuta kwa kutumia kijiti au kidole cha mkono kukata urefu wa tuta kwa nafasi ya sm 10 au sm 15 kutoka kifereji hadi kifereji kisha sia mbegu kwa kuzisambaza katika vifereji na fukia kwa udongo mwepesi.

(ii) Kupanda kwa kutawanya

Njia hii hutumika hasa kwa mbegu ambazo ni ndogo sana kama vile mbegu za mchicha ambapo mbegu huchanganywa na mchanga katika uwiano wa 1:4 kabla ya kutawanya katika tuta. Kwa mfano kikombe kimoja cha mbegu kitachanganywa na vikombe vinne vya mchanga. Kipimo chochote utakachotumia hakikisha kinafuta uwiano huu ili kuwa na mchanganyiko mzuri wa mbegu katika tuta.

  • Kuweka matandazo (Mulching)

Baada ya kutengeneza tuta na kusia mbegu weka matandazo ya nyasi kwa kuyatandaza katika tuta kisha mwagilia maji ya kutosha.

Zingatia: Idadi ya vitalu itategemea idadi ya miche unayotaka kuwa kutokana na ukubwa wa eneo unalotaka kupandikiza.


Monday, 24 July 2023

kilimo Cha strowbery

 

Email address shafii.ismail09@gmail.com 

WhatsApp number /call 0683308173 

Website http//www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

Utangulizi

strawberry (fukasidi) hustawi katika maeneo yenye joto la wastani, na hukua kwa haraka zaidi na uzalishaji kuongezeka linapolimwa kisasa zaidi, Hasa katika Green house. Zao hili hukua vizuri katika mwinuko wa mita 1500 na zaidi kutoka usawa wa bahari. Zao hili hata Tanzania hustawi zaidi katika mikoa mingi kama Morogoro,mbeya,iringa, Arusha, Kilimanjaro, na Pia hufanya vizuri katika mikoa ya Pwani endapo utalima kisasa zaidi na kufuata maelekezo ya kitaalamu(Under controlled condition)


AINA YA STRAWBERRY


Aina kuu ni Fragaria genus


.chandler-strawberries.jpg


Na hapo kwenye Fragaria genus utakutana na;


1. Chandler,

2. Domanil

3. pajaro

4. Douglas

5.Tioga selva

6. Rabunda

7.Tri-Star

8.Tribute


Kila aima ina sifa zake nzuri na mbaya zake pia na ziko za ukanda wa joto sa a na ukanda wa Baridi sana.


KUPATA KUJUA KILA AINA NA SIFA ZAKE

MATUMIZI


Strawberry ina matumizi mengi sana nitataja machache.


1. Kutengenezea Icecream- Mahoteli makubwa huanunua kwa ajili hiyo ya Icecream.


2. Ftesh Juice- Wanunuzi ni Mahoteli na majumbani.


3. Processed Juice- Hii ni juice iliyo packiwa


4. Yogurt- Viwanda vya kusindika maziwa wanatumia sana na ndo wanunuzi wakuu wa haya matunda.


5. Watengeneza keki- Kudecorate keki


6.Decoration kama maua ya kupamboa ukumbini.


7. Manukato


8. Kuliwa kama Freshi fruit


9. Jam


10.Sauces


Kupanda

1.NJIA YA MABOMBA


Ili kuwa na mazao bora ambayo yatakuwezesha kupata soko la uhakika, inashauriwa kuzalisha kwenye nyumba maalumu ya kuzalishia mazao (green house).


Katika upandaji wa strawberry kwenye green house Utahitajika kuwa na Mabomba yenye matundu(Plastic Pipe)


Matundu katika bomba hilo yawe na umbali wa inchi 1.

2. Ni vyema matundu hayo yakawa zigzag, ili kuruhusu mimea utakayoipanda kukua vizuri bila kusongamana


Tandika karatasi la nylon sakafuni ili kuwezesha maji utakayotumia kunyeshea kurudi kwenye bwawa au

sehemu ya kuhifadhia.


4.Ning’iniza mabomba hayo kwa kutumia waya.


Jaza kokote, yenye mapande makubwa kiasi.

6 .Panda miche kwenye kila tundu kwa uangalifu ili mizizi isikatwe na kokoto zinazoshikilia mmea


2.NJIA YA KITALU CHA NGAZI


umwagiliaji

Mimea ya strawberry inahitaji maji kwa kiasi kikubwa sana. Hii inamaanisha kuwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri


 umwagiliaji matone

wa umwagiliaji kabla ya kuanza kilimo cha zao hili. Unapaswa kumwagilia mara nne kwa siku, kila baada ya saa nne unapaswa kumwagilia kwa robo saa. Hii itawezesha mimea yote kupata maji ya kutosha. Endapo stroberi haitapata maji ya kutosha, uzalishaji wake pia utakuwa ni hafifu sana, kwani maua hayatachanua ipasavyo na hata matunda kukomaa inakuwa ni shida.


Wadudu na magonjwa

WADUDU


Spider (two spotted) mite


Cluster caterpillar

Heliothis

Looper

Rutherglen bug

Cutworm

Aphids

Queensland fruit fly

MAGONJWA


   Lethal yellows

Mmea ulioathirika unaonyesha dalili zifuatazo;


Majani yaliyokomaa yanakuwa na rangi ya dhambarau na yanajinyonganyonga kwa upande wa juu na kusababisha kuangua chini.


Majani chipukizi yanakuwa na rangi ya njano katika kingo za jani na kupelekea kudumaa kwa kikonyo cha jani. Huu ugonjwa unapunguza nafasi ya jani kushindwa kujitengenezea chakula chake na hivyo mmea kudumaa na kupelekea kufa kwa mmea.


Mnyauko fusari (fusarium wilt)

Huu ugonjwa huunezwa na mbegu zenye huu ugonjwa na husambazwa na vimelea vya fangasi ambavyo vipo kwenye udongo.


Ugonjwa huu hujitokeza Zaidi kwenye kipindi cha kiangazi na hushambulia sehemu za mirija yam mea ya kupitishia chakula hivyo mmea hukosa chakula na maji na hatimaye unyauka na kufa. Na shina la mmea ukipasua ndani unakuta lina rangi ya kahawia.


Kudhibiti


Tumia mbegu safi na bora.

Tumia dawa ya kuua wadudu na magonjwa ili kupata mazao mengi na yenye ubora.

Choma masalia ya mazao ili kudhibiti uenezaji wa ugonjwa

Chagua mbegu ambayo ina uwezo wa kuhimili magonjwa.


Friday, 21 July 2023

KILIMO CHA MBAAZI



Email 

 shafii.ismail09@gmail.com 

WhatsApp /call 0683308173 

Website http//www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com




Mbaazi ni zao la chakula ambalo pia linaweza kulimwa kama zao la biashara kutokana na kuwa na soko zuri. Mbaazi ina kiasi kikubwa cha protini. Mbaazi inaweza kutoa mavuno ya tani 6 hadi 8 kwa hekta

MAHITAJI MUHIMU YA MBAAZI.1. Mbaazi zinafaa kulimwa katika maeneo ya ukanda wa chini kutoka usawa wa bahari na pia hata sehemu za nyanda za juu nazo zinafaa kulimwa zao hili. 
2. Ni zao linalostahimili ukame na hili linalifanya kulimwa hata katika maeneo yanayopata mvua za wastani na yale yanayopata mvua kwa kiasi kidogo.
3. Mbaazi hukua vizuri katika maeneo yenye wastani wa mua wa mm 400-1000 kwa mwaka,katika maeneo yenye mvua zaidi ya mm 1000 kwa waka hustawi ila ni rahisi kupta ugonjwa wa mnyauko.

4. Mbaazi hustawi vizuri katika hali ya joto ya nyuzi 18-30 C. Pia kama hali ya udongo na unyevu ni nzuri  zinaweza kukua vizuri katika hata katika 35 C.
UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA MBAAZI
Mbaazi zinastawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia linaweza kulimwa katika udongo wenye asili ya mfinyanzi katika maeneo yanayopata mvua kwa kiasi kidogo. Hustawi vizuri katika udongo wenye pH 5-7, Pia pH 4.5 - 8 zinaweza kulimwa

AINA KUU ZA MIMEA YA  MBAAZI
Kuna aina kuu tatu za mimea ya mbaazi
Mbaazi za muda mrefu
: Hii ni mbaazi ambazo zinawezwa kuvunwa katika misimu zaidi ya miwili.Huchukua muda mrefu kukua hadi kuvunwa kwa mbaazi zake.Baada ya mbaazi kuvunwa Mbaazi hukatwa nusu yake na kuruhusu Machipukizi yake kukua na kuvunwa tena msimu unaofuata na zoezi hili hufanyika ziadi ya msimu mmoja.Huchukua Siku 180 hadi 270 kupandwa hadi kuvunwa.

Mbaazi za Muda wa kati; Hizi hulimwa kwa msimu mmoja ila huchukua mda wa kati katika kukomaa kwake.huchukua siku 140 hadi 180.

Mbaazi za muda MfupiHizi hulimwa kwa msimu mmoja na baada ya kuvunwa mimea yake hukatwa na kung'olewa na kupandwa mbegu mpya msimu unaofuata.mbegu hizi huchukua siku 120 hadi 140.

MAANDALIZI YA SHAMBA
Andaa shamba lako mapema kadri utakavyoweza kulima kulinga na aina ya kilimo unachotumia, hakikisha umeondoa magugu shambani na uchafu mwingine ambao unaweza kuinyima mimea ya mibaazi kukua vizuri.

UPANDAJI.
Mbaazi za Muda Mirefu
; Panda kwa mistari kwa umbali/ nafasi ya sentimeta 150 kwa 100.(Sentimeta 150 Mstari na mstari na sentimeta 100 Shina hadi shina katika mstari)
Mbaazi za Muda wa Kati; Mbaazi.Panda kwa mstari nafasi ya sentimeta 100  kwa 60

Mbaazi za Muda  Mifupi;Panda kwa mstari  kwa umbali/ nafasi ya sentimeta 90 kwa sentimeta 60

ANGALIZO:
Maaneo ya Pwani ambayo yanarutuba kwa wingi na joto la kutosha mimea inakuwa kwa kasi na ili upate mavuno bora lazima uhakikishe mimea yako unaipa nafasi ya kutosha,Hivyo uwe makini na nafasi za mimea yako uanapopanda shambani.

MATUMIZI YA MBOLEA.Mara nyingi zao la mbaazi halihitaji matumizi ya mbolea na samadi. Ijapokuwa Hustawi zaidi katika shamba lenye rutuba ya kutosha.

PALIZIMimea ya mibaazi huitaji kupaliliwa mapema ili kufanya ikue katika hali ya afya bora na kusaidia kuongeza mavuno yako.

WADUDU WANAOSHAMBULIA MIBAAZI NA MBAAZIMbaazi ni mojawapo ya mazao ambayo hayashambuliwi sana na wadudu japokuwa wapo wadudu ambao kuna maeneo mengine hushambulia kwa kiasi kikubwa mbaazi nao ni funza wa tumba na wadudu wapekechaji wa mbaazi. Zuia wadudu hawa kwa dawa za wadudu kama ATTAKAN-C,Karate au dawa nyingine za wadudu.

MAGONJWA YA MBAAZI
Ugonjwa mkuu unaoshambulia mbaazi ni mnyauko wa fusaria ( fusarium wilt).Ambao husababisha shina la mbaazi kuwa na rangi nyeusi,ugoro au kahawia.ugonjwa huu huzuia mfumo wa usafirishaji wa mmea.
Zuia ugonjwa huu kwa kuzungusha mazao shambani kila baada ya msimu kuisha.usipande kila msimu mbaazi tuu.Kila msimu badilisha zao.

UVUNAJI WA MBAAZIMbaazi zikishakomaa na kuanza kukauka zivunwe mapema kwa kukatwa matawi yenye mbaazi na kukaushwa zaidi kisha Mbaazi zitenganishwe kwa mikono au kwa kupigwa hayo matawi  taratibu  baada ya kukaushwa sana..
Mbolea ya asili (mboji)


Email address shafii.ismail09@gmail.com 

WhatsApp /call 0683308173 

Website http//www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

MBOJI 

 Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama (matamahuruku) ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji.

Vipande vya vitu au sehemu za viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini itachukua muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba yake kupotea.

Lakini kama muda ukitengwa ili kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri na ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na jikoni yanatumika katika kutengenezea mboji.

  • Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa shambani. Mboji huchemka hata kiasi cha kuua magonjwa ya mimea na mbegu za magugu.
  • Majani makavu ya ndizi ni mazuri kwa kutunza vifaa vya mbolea na kuweka ukavu. Hali hii huwa huzuia kupotea kwa maji kabla ya kujenga lundo la mboji na wakati mbolea inapokuwa inaiva.

Vifaa visivyofaa kuwekwa kwenye mboji

  • Sehemu za mimea ambazo zimenyunyiziwa dawa ya kuwaua wadudu (viuatilifu) na kwekwe juzijuzi (Pesticide/herbicides).
  • Vipande vya nyama kwa sababu vinavutia panya na wadudu wengine.

Sehemu nyingi za Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama (matamahuruku)) ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa huku ni tofauti kabisa na zile sehemu zilizowekwa. Mboji iliyoiva hubadilika rangi na kuwa ya hudhurungi, tifutifu na hunukia vizuri.

MUHIMU

Samadi kutoka kwa mifugo na mabaki ya mimea ni nzuri sana katika kutengeneza mbolea hai.

Namna ya kutengeneza mboji ya mimea Kusanya vitu na vifaa vinavyohitajika katika utengenezaji wa mboji ambayo ni;

  • Majani mengi mabichi/kijani na makavu. Majani jamii ya mikunde ni mazuri sana kwani hutengeneza kirutubishi cha naitrojeni (N) kwa wingi.
  • Mabua ya mahindi au vitawi vya miti.
  • Udongo wa kawaida wa juu.
  • Samadi, mbolea yoyote ya wanyama au mboji ya zamani .
  • Majivu au vumbi la mkaa.
  • Maji

Hatua

  1. Chagua sehemu karibu na eneo ambalo mboji itaenda kutumika na ambapo kuna hifadhi ya kutosha kukinga dhidi ya upepo, jua na mvua.
  2. Katakata majani yawe madogo madogo ili yaweze kuoza haraka. Tengeneza msingi kama mita sita (6) urefu na upana wake mita 2 kwa kutumia majani magumu kama matawi/vijiti. Hii itahakikisha maji yanatiririka na hewa ina zunguka vizuri. Hakikisha kuna nafasi ya kutosha kufanyia kazi kwenye biwi bila kulikanyaga.
  3. Weka sentimita 10 ya majani ambayo hayaozi haraka kwa mfano mabua vya mahindi au mimea mibichi/kijani.
  4. Weka sentimita 10 ya vifaa ambavyo huoza haraka kwa mfano maganda ya mboga na matunda.
  5. Weka sentimita 2 ya samadi(mbolea-hai ya wanyama), mabaki ya mbolea ya zamani kama yaweza kupatikana.
  6. Weka udongo wa juu sentimita 10 kutoka kwenye shamba ambalo hulimwa.
  7. Majivu na mkojo vyaweza kunyunyuziwa juu ili kufanya biwi/lundo kuoza haraka
  8. Nyunyizia maji kwenye biwi mpaka lilowe.
  9. Rudia mpangilio huu kuanzia namba nne (4) mpaka lundo lifike mita moja (1.m) hadi moja na nusu (1.5m) kwenda juu isipokuwa vijiti/matawi ya kwanza.

Zingatia

  • Biwi/lundo cha mboji linatakiwa lifunukwe ili kupunguza/kuzuia mvuke ama mvua nyingi ambayo hubeba rutuba kutoka kwenye mbolea. Weka gunia, nyasi ama matawi ya ndizi yaliyokauka.
  • Kila tabaka/kunjo/safu yafaa kupangwa kuanzia kwenye ukingo ili lundo la mbolea lisiporomoke.
  • Namna nyigine ya kuzuia lundo kuporomoka ni kwa kuweka vipande vya mbao kando ya biwi. Wavu wa nyuzi za chuma utafanya biwi kukauka.
  • Katika sehemu zenye ukavu mwingi. Mianzi iliyo na mashimo husaidia kufanya hewa kuingia na kuzunguka kwa urahisi.