Sunday, 9 July 2023

Kilimo cha chainizi

 Email Shafii.ismail09@gmail.com 

WhatsApp /call 0683308173 

Website http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

Spinachi ni moja kati ya mazao ya mbogamboga inayo limwa sana nchini Tanzania na asili yake ni china na ndo maaana huwa tunaiita chinese na badae likasambaa katika nchi mbalimbali ikiwemo na Tanzania.

Mboga hii huwa haina msimu, hivyo mkulima anaweza kulima muda wowote ambao anataka, na hii itategemea upatikanaji wa maji wa maji kwa wingi. Kwani mboga hii huhitaji maji kwa wingi katika hatua za awali.

Hali ya hewa inaoyofaa kwa kilimo hiki ni.
Jotolidi; Chinese au  linastawi na kukua vizuri kwenye maeneo yenye jotolidi 18 °c hadi 27° c.

Unyevunyevu; chinese  ni zao linalo tegemea umwagiliaji kama ambavyo nimekwisha eleza hapo awali hivyo linaitaji maji mengi wakati wa ukuaji.

Udongo; chinese cabbage linakua vizuri kwenye udongo wa kichanga na wenye unyevunyevu wa kutosha PH; 5.5 hadi 7.6

Namna ya kuandaa shamba.
Udongo unatakiwa utifuliwe vizuri kabla ya kupanda unaweza kutumia jembe la mkono au machaku na chisel na andaa shamba wiki 6 kabla ya kupanda.

Uandaaji wa kitalu.
Kitalu kinatakiwa kiwe na upana wa mita 1 yani sentimita 100 na urefu wa mita 5 yani sentimita 500. Kitalu kitifuliwe vizuri na kiwe na kingo ili kuzuia maji kutoka nje ya kitalu. kisha panda mbegu kwenye kitalu kwa sm 15 hadi 20 mstari hadi msitari na panda mbegu sm 2 kati ya mbegu na mbegu na fukia sm 1 hadi 2.

Kupanda
Kwa kupanda moja kwa moja chimba udongo sm 2 hadi 3 kwa kutumia jembe la mkono na panda nafasi ya 30 mstari hadi mstari na 30 mbegu hadi mbegu na fukia sm1 hadi 2.
Na kwakupandikiza hamisha miche inapo fikia urefu was sm 5 na chagua miche yenye afya na isiwe na magonjwa.

Mbolea.
Kama unatumia mbolea ya ng’ombe, kuku na nguruwe tumia ndoo katika kila kitalu chenye mita 5
Na pia weka mbolea ya kukuzia UREA gram 50 kwa kila kitalu chenye mita 5 pale mmea unapofikia majani matano.

Palizi
Tumia jembe la mkono kupalilia magugu pale yanapo jitokeza.

Magonjwa na wadudu waharibifu
Pale utakapohisi majani ya mboga hizi yameanza kubadikika, ikiwa ni ishara ya kushambuliwa na wadudu, tafadhari unashauriwa uweze kutumia chemicali za kuua wadudu kama vile ninja, supercorn, wilcron na perfecron na pia hakikisha kila wakati unakumbuka kuondoa  magugu pamoja na mimea yenye wadudu na pia weka shamba safi wakati.

Lakini kama utatokea ugonjwa wa Kuoza kwa mizizi unachotakiwa kufanya kuondoa mazao yaliyo athilika na ugonjwa huo.

Kuvuna
Chinese ukomaa baada ya miezi 2 hadi 4 inategemea na aina mbegu uliyopanda, au muda mwingine hutegemea na hali ya hewa pia.

Kumbuka;
Wakati wa kuvuna unang’oa kwa mkono au unaweza kutumia kisu kukata kuanzia chini kabisa ya shina ili kuruhusu majani mengine ya mboga kukomaa.

Saturday, 8 July 2023

Kilimo cha cabbage

 Email Shafii.ismail09@gmail.com 

WhatsApp /call 0683308173 

Website http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

CABBAGES 


 Zao la kabichi hulimwa katika mikoa ya Morogoro, Arusha,Tanga, Iringa, Kilimanjaro na Mbeya. Kama mboga zao la kabichi lina viini lishe kama chokaa, protini, kambakamba na maji kwa wingi. Hutumika kutengeneza kachumbari, pia kuchanganywa na nyama au maharage.
HALI YA HEWA
Zao la kabichi hupendelea: hali ya ubaridi Mwinuko: Kuanzia mita 1200 hadi 1900 kutoka usawa wa bahari. Udongo uwe; Tifutifu,  Rutuba nyingi na Unaohifadhi unyevu kwa muda mrefu, Usiotuamisha maji , Usio na chumvichumvi nyingi. Kama hauna rutuba ya kutosha ongeza mbolea ya samadi au mbolea vunde. 
 AINA ZA KABICHI
 Early Jersey Wakefield:  Umbo lilochongoka kidogo, Hufunga vizuri,  Uzito ni kati ya kilo 1.5 hadi 2.0,  Hukomaa mapema siku 90 – 100 tangu kupandikiza. · Copenhagen Market: Vichwa vya mviringo na hupasuka kirahisi . Hukomaa mapema, siku 90 – 100 tangu kupandikiza ·
 Prize Drumhead: Vichwa vikubwa (kilo 2- 2.5), Vichwa ni bapa, huchelewa kukomaa (siku 110 – 120) - Huvumulia hali ya jua kali, Pia vichwa hupasuka. · Oxheart: - Vichwa vidogo huchongoka kama moyo,  Hupendwa sana na walaji,  Ladha yake ni tamu, hukomaa mapema, Hazina tabia ya kupasuka.  Glory of Enkhuizen: - Vichwa vya mviringo, Huvumilia hali ya jua kali,  Huchelewa kukomaa (siku 110 – 120)  na  Ina tabia ya kupasuka.
KUOTESHA MBEGU
Mbegu za kabichi huoteshwa kitaluni na baadaye huhamishiwa shambani. Andaa kitalu vizuri na weka mbolea za asili zilizooza vizuri kwa kiasi cha ndoo 5 – 10 za ujazo wa kilo 20 kwenye eneo la mita za mraba 10. Changanya na udongo kisha lainisha udongo kwa kuvunja mabonge makubwa kwa kutumia reki. Tengeneza tuta lililoinuka kwa sentimita 25 na lenye upana wa mita 1.
Mwagilia maji kwenye tuta siku moja kabla ya kusia mbegu. Kiasi cha mbegu zinazohitajika ni gramu 1 kwenye eneo la mita 1 ya mraba hivyo hekta 1 huhitaji gramu 200 – 300. Sia katika umbali wa sentimita 15 toka mstari hadi mstari na kina cha nusu sentimita.Funika mbegu na udongo laini kasha tandaza nyasi kazu ili kuhifadhi unyevu.Mwagilia maji kila siku asubuhi na jioni mpaka mbegu ziote, huota kwa muda wa siku 5 – 10.
KUTAYARISHA SHAMBA
Shamba litayarishwe mwezi mmoja kabla ya kupandikiza.
·        Katua ardhi kwa kina cha sentimita 30
·        Lainisha udongo na tengeneza matuta  kisha weka mbolea za asili kwa kiasi cha ndoo 2 kwa kila hatua moja au Mbolea iwekwe kwa kila shimo kwa kiasi cha kilo kwa shimo.
·         Mbolea ya N.P.K. 5:15:5 yaweza kuwekwa kwa kiasi cha kijiko 1 cha chai chenye gramu 5 kwa kila shimo.
KUPANDIKIZA MICHE

 Miche huwa tayari kupandikizwa shambani baada ya wiki 3 – 5 tangu kusia mbegu . Miche huwa na urefu wa sentimita 15 – 20. Ng’oa miche kwa uangalifu na pandikiza kama ilivyokuwa kitaluni na hakikisha mizizi haipindi wakati wa kupandikiza. Nafasi ya kupandikiza: Hutegemea aina ya kabichi – zenye vichwa vikubwa (Drumhead) ni sentimita 60 kutoka mche hadi mche na sentimita 75 toka mstari hadi mstari. – Zenye vichwa vidogo (Oxheart) ni sentimita 40 – 50 kutoka mche hadi mche na sentimita 60 toka mstari hadi mstari. – Umbali toka tuta moja na jingine ni sentimita 60. – Muda mzuri wa kuotesha ni asubuhi au jioni – Baada ya kupandikiza weka matandazo kama vile nyasi kavu ili kuhifadhi unyevu na kuzuia magugu kuota kwa urahisi. 
 PALIZI
 Zao la kabichi halina mizizi ya kina kirefu hivyo wakati wa palizi ni muhimu kuwa mwangalifu kwa kupalilia juu juu ili kuepuka kukata mizizi. Kuongeza matandazo husaidia kupunguza palizi a mara kwa mara.
UMWAGILIAJI
 Kabichi hustawi vizuri zaidi iwapo kuna maji ya kutosha kwenye udongo. Mwagilia mara mbili au zaidi kwa wiki kutegemea hali ya hewa na aina ya udongo. Kabichi ambazo hazikupata maji ya kutosha huchelewa kufunga na huwa na vichwa vidogo. Zikikosa maji kwa muda mrefu na zikapata maji mengi ghafla, vichwa hupasuka. 
 MBOLEA
Mbolea ya kukuzia (S/A) huwekwa baada ya 4 – 6 baada ya kupandikiza miche na kabla ya vichwa havijaanza kufunga. Kiasi cha kilo 80 huhitajika kwa eka moja. - Kilo 40 ziwekwe baada ya wiki 4 – 6 na kilo 40 ziwekwe tena baada ya mwezi mmoja . Mche mmoja huhitaji kiasi cha kidogo cha gramu 5. Mbolea iwekwe kuzunguka shina umbali wa sentmita 10 – 15 kutoka kwenye shina. Muhimu: Epuka kuweka mbolea nyingi, kwani husababisha vichwa visifunge vizuri (kabichi zinakuwa nyepesi) 
 KUBADILISHA MAZAO
 Kabichi nizao linalotumia virutubisho vingi kulinganisha na mboga nyingine,hivyo kabla ya kuotesha kabichi panda mazao jamii ya mikunde ili kuongeza rutuba. Baada ya kuvuna kabichi otesha mazao yanayotumia chakula kidogo kama vile karoti, radishi au lettuce. Kubadilisha mazao pia hupunguza kuenea kwa wadudu waharibifu na magonjwa. 
KUVUNA
 
 Kabichi hukomaa katika siku 60 mpaka 210 tangu kupandikiza miche. Hata hivyo muda wa kukomaa hutegemea aina ya kabichi. Uvunaji hufanyika kwa kukata shina sentimita 2 – 3 kutoka kwenye kichwa kwa kutumia kisu. Ondoa majani ya nje na acha majani 2 au 3 ya kijani kwa ajili ya kuzuia kabichi zisikwaruzike na kuoza wakati wa kusafirisha. Punguza urefu wa majani ili kurahisisha ufungaji. Ni muhimu uvunaji ufanyike asubuhi au jioni. Ondoa kabichi zilizooza au kuharibika wakati wa kuvuna, kisha panga zilizobaki kufuata daraja kama vile ndogo, za kati na kubwa. Mavuno: Kiasi cha tani 40 au zaidi za kabichi hupatikana kwa hekta moja kama zao limetunzwa vizuri.
HIFADHI
Kabichi ni zao linaloharibika kwa haraka, hivyo halina budi kutumika mapema iwezekanavyo baada ya kuvuna. Kabichi kwa ajili ya kuuzwa zisafirishwe mara moja kwa walaji. Kama usafiri ni mgumu, zihifadhiwe kwenye sehemu yenye ubaridi na hewa ya kutosha. Wakati wa kusafirisha, ziwekwe kwenye matenga au visanduku vya mbao vilivyo na matundu yanayoingiza hewa ya kutosha. leo tuishie hapa unaweza kuandika chochote au kutoa ushauri

Tuesday, 4 July 2023

VIUATILIFU

 VIUATIIFU:


Viuatilifu ni kemikali maalumu zilizotengenezwa kwa lengo la kuua au kudhuru visumbufu lengwa katika viumbe hai husika


Kemikali yeyote yaweza kuua au kudhuru hivyo chukua tahadhari sana unapotumia viatilifu hivyo kwani madhara ya sumu ya kemikali yanapungua au kuongezeka kutegemeana na wingi wa dozi ya kemikali.


Kwa Mfano

Hata kemikali (Madawa) tunazotumia binaadamu kutibu magonjwa mbalimbali mfano dawa za kutibu malaria, minyoo au typhoid, etc ni nzuri kama ukifuata masharti (ya dozi na wakati sahihi wa kutumia) lakini ukizitumia vibaya (kuoverdoze) zaweza kukudhuru kutegemea na wingi wa kemikali ulio consume.


Maana ya visumbufu

Ni viumbe hai (mfano Wadudu, mimea-magugu, wadudu, ndege, chawa etc) , vinavyoathiri ubora, wingi wa mavuno au uhai wa kiumbe hai kusudiwa (mimea-Mahindi, nyanya, vitunguu)


KUMBUKA ZIPO AINA NYINGI SANA ZA VIUATILIFU KUTEGEMEA NA AINA YA KISUMBUFU LENGWA


Mifano 1.Viua dudu(Insecticides),-Mfano wa kiua tilifu- Dursban, Phyrinex, duduall,Belt 2.Viuakuvu(Funguicides),mfano -Blue Copper,-cobox,-Kocide, Ridomil Gold,Ivory, Ebony 72WP 3. Viuagugu(Herbicides)-Mfano Roundup, Mo-Round, Paraquat 4. Viua Minyoo(Nematicides),Mfano-Furadan-Basamid, 5. Viuakupe(Acaricides)- Mfano-Tactix, 6. Viuandege(Avicides)-Mfano-Bombs,-Methicarb, 7. Vifukizi (Fumigants) Phostoxin tablet


ATHARI ZA SUMU KATIKA VIUMBE HAI A) Usumu (Toxicity) na Madhara (Hazard)


Usumu; Ni uwezo wa kusababisha madhara( Hutegemea aina ya kemikali iliyotumika

Madhara: Uwezekano wa sumu kudhuru au kusababisha matatizo hasa ya kiafya Kwa hiyo: Madhara=Usumu x Eneo la Mwili x Muda.


Matatizo ya Viuatilifu tunavyovitumia

1. Husababisha Usugu(Resistance)

2. Huua Viumbe visivyolengwa(Non target)

3. Mabaki (Residues)

4. Uchafuzi wa Mazingira(Pollution)

5. Madhara ya kiafya

6. Kuzaliwa kwa visumbufu vipya Maeneo ambayo sumu huingilia mwilini,

i)Mdomoni-kwa njia ya kujiua, kunywa, kuweka katika cupa yenye sumu kwa bahati mbaya.

ii)Kupitia ngozi (Dermal)-kwa njia ya mivujo (Spills), kujigusa na mazao, unyunyizaji,

iii) Kupumua-hewa(Inhalation)

iv) Kupitia mikwaruzo au michubuko

● Eneo la kichwa- (43%)

●Mikono-Kiganja (4%)

●Mikono (eneo la kichwa)-(3%)

●Tumbo-(7%)


●Chini ya tumbo-(38%)

● Miguu – (5%) Madhara yasababishwayo na sumu

-Madhara ya muda mfupi (ACUTE) , mfano, ngozi kuwasha, kusikia -kizunguzungu,kutapika, kichefuchefu, uchovu, Kichwa kuuma

XX-UKIWA MAKINI WAKATI UNAPOTOKA KUPIGA DAWA MASHAMBANI KAMA HUKUVAA VIFAA VYA KUJILINDA UTAKUWA UMEKUTANA NA BAADHI YA MADHARA NILIYOYAELEZA HAPO JUU

-Madhara ya Muda Mrefu (CHRONIC) -Upofu, Kansa ya Ngozi, Mtindio wa ubongo, kifo

Madhara ya Sumu kwa Muda mrefu, huweza kusababishwa na

-Kutumia Kemikali(Sumu) mara nyingi

-Kupata sumu kupitia vyakula na hewa

-Vumbi lenye mabaki (Community exposure) Madhara ya Sumu (WHO STANDARD)

Ni muhimu sana kujua ni aina gani ya dawa umenunua (hasa kujua umenunua sumu yenye ukali kiasi gani).


BAADHI YA MAMBO MUHIMU YA KUKAGUA KABLA HUJANUNUA DAWA YOYOTE DUKANI


 


1. Kopo lolote la dawa iliyosajiliwa tanzania lazima iwe na Namba ya uthibitisho wa TPRI

2. Lazima iwe na kibandiko cha kuonyesha imetengenezwa lini na itaisha nguvu lini,pia katika hicho kibandiko lazima hiyo dawa iseme ndani yake ipo na KIAMBATA GANI (Chemical ingredient)

3. Pia lazima ieleze jinsi ya kutumia dozi (Uwiano wa dawa :Maji, ie mls 20-Dawa:ml20-Maji

4. KOPO LOLOTE LA KIUATILIFU LAZIMA LIWE NA UFITO SALAMA, CHINI KARIBU NA KITAKO CHA KOPO (CHUNGUZA KWA MAKINI), UTAKUTA AIZA KUNA UFITO RANGI 1. NYEKUNDU,AU 2. NJANO, AU 3. BLUU, AU 4. KIJANI


KUMBUKA; Viutailifu vingi/ Sumu nyingi sana tutumiazo mashambani zilizo katika daraja la kwanza (Kibandiko chenye ufito mwekundu) mpaka la pili (Ufito wa njano), maranyingi ukizipiga wakati mimea iko na maua au matunda machanga sana ukizidisha zaidi ya mls 10-15 kwa maji lita 20 LAZIMA Maua au matunda yatapukutika maana ni sumu kali sana , hivyo zinahitaji dozi kidogo sana kati ya mls 5 hadi 10 tu kwa maji lita 20.


TAHADHARI ZA KUCHUKUA PUNDE UNAPOTAKA KUTUMIA VIUATILIFU HIVI MASHAMBANI


1. Soma kibandiko vizuri ukielewe, na nunua dawa sahihi kwa kisumbufu sahihi


2.  Puliza dawa hizi au asubuhi sana au jioni, usipulize mchana


3. Kabla ya kupuliza angalia sana uelekeo wa upepo


4. Hakikisha bomba lako (Knapsack-Sprayer liko salama-halivujishi kimiminika


5. Hakikisha unamavazi maalumu ya kuingilia shambani, na unapomaliza kupiga dawa vua mavazi hayo


6.Hakikisha unabuti/viatu maaalumu vya kuvaaa punde uingiapo shambani-USICHOMEKEE SURUALI NDANI YA BUTI, BALI SURUALI IFUNIKE BUTI, ILI DAWA IKILEAK IPITILIZE CHINI , ILA UKICHOMEKEA MEANS DAWA IKILEAK ITAINGIA DAWA YA VIATU/BUTI NA HAITATOKA-ITAKUDHURU


7.EPUKA KUNUNUA DAWA ZILIZOKWISHA MUDA WAKE, AU DAWA ZA KUPIMA, MAANA IKITOKEA BAHATI MBAYA DAWA HIZO ZA KUPIMA ZIMEKUPA MADHARA DOCTOR WATASHINDWA KUJUA DAWA GANI HASA IMEKUDHURU. INATAKAIWA UKIDHURIKA NA DAWA HIZI ZA KILIMO UKIPELEKWA HOSPITAL UENDE NA KOPO LA ILE DAWA, ILI ADOCTOR WAJUE ANTIDOTE GANI WAKUPE KWA HARAKA, WAKATI MATIBABU RASMI YAKIFUTA KUWA MAKINI UNAPOTAKA KUNUNUA DAWA, JARI SANA CHEMICAL INGREDIENT (USIFUATE MAJINA YA KIBIASHARA-TRADE NAME).


Mifano


1.Kuna dawa za wadudu mfano-Dursban, Twigaphos, Subachio, Royalnex, Propyrifos, Resguard nk. etc zote ni aina moja za dawa, ZINAKIMABTA KIMOJA TU CHA Chlorpyrifos, HIVYO STICK KATIKA CHEMICAL NAME

-Haya yote..Dursban, Twigaphos, Subachio, Royalnex, Propyrifos, Resguard NI MAJINA YA KIBISHARA TU YANABADILIKA WAKATI WOWOTE, KIKUBWA NI KUJUA NI NINI KIMO NDANI YA HILO KOPO??Yaani Dhamana/Guarentee/Kiambato Aminifu ni kipi??

xx-ACHA KUKALILI MAJINA YA KIBIASHARA JITAHIDI KUELEWA NI KIAMBATA GANI/DAWA GANI IMO NDANI.


2. Kuna makopo ya dawa yameandikwa, Ascotin 0.15EC, Nimbecidine 0.03%... zote ndani yakeni dawa moja maana zina kiambata cha Azadirachtin, lakini kama hujui unaweza kudhani ni dawa tofauti


3.mfano mwingine ni wa makopo yaliaonadikwa, Avaunt 150EC, Mavuno 25 EC, zote ni aina moja maana zinakiambata kimoja cha Indoxacarb


HIVYO USIPOKUWA MAKINI UNAWEZA KUNUNUA MAKOPO YA DAWA HATA 3 KUMBE ZOTE NI AINA MOJA TU (VIAMBATA VILIVYOMO VINAFANANA)-KUWA MAKINI


MBOLEA

 Email Shafii.ismail09@gmail.com 

WhatsApp /call 0683308173 

Website http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

MBOLEA

Mbolea kwa maana ya kueleweka kwa haraka ni kitu chochote kinacho ongeza virutubisho muhimu kwenye udondo ambavyo hutumiwa na mimea ili kuboresha ukuaji wa mimea na upatikanaji wa mavuno mazuri.

Kuna aina mbalimbali za mbolea kama mbolea za asili Mbolea za asili mfano, Samadi, Mboji, mbolea za kijani na Mbolea za viwandani mfano DAP, YaraMila


1. Mbolea za asili

Mbolea aina ya Mboji (Mabaki ya Mazao). Mbolea hizi hutokana na vinyesi vya wanyama, mabaki ya mazao shambani,majivu na takataka nyingine ambazo ni rafiki kwa mazao na udongo (takataka zisizo na madhara kwenye udongo).



Mbolea za asili zinafaa sana kutumika wakati wa kuandaa shamba/ mkulima anaweza kuchamganya mbolea ya asili na udongo wakati wa kulima au mkulima kuitumia mbolea ya asili kupandia mazao yake mfano mahindi, mharagwe, mboga mboga na mazao mengine.



Mbolea za asili hufanya kazi ya kuboresha hali ya udongo kuufanya udongo uwe na uwezo wa kuifadhi maji na hewa, vilevile mbolea za asili ufanya udogo kuweza kutengeneza matundu mazuri ambayo husaidia mizizi ya mazao na hewa kupenya kwa urahisi.



2. Mbolea za viwandani/ mbolea za kisasa

Mbolea hizi zimetengenezwa kiwandani kwa kuchanganya virutubisho mbalimbali vinavyo hitajika katika ukuaji wa mimea. Mbolea za viwandani zipo za aina mbalimbali na pia hutumika kwa wakati tofauti katika hatua za ukuaji wa mimea, zipo mbolea maalumu kwa ajili ya kupandia mazao mfano DAP , zipo za kukuzia mazao mfano UREA, CAN na NPK



Mbolea hizi zinapaswa kutumiwa kwa uangalifu kulingana na mahitaji ya mimea kwani mbolea ikizidi katika udongo husababisha mimea kukua sana na kusahau kutengeneza matunda ambayo ndio tegemeo kwa mkulima hivyo mkulima anavyo paswa kuweka mbolea kulingana na vipimo vinavyotakiwa kitaalamu (ni vyema mkulima kupata ushauri wakilaamu kutoka kwa mtaalamu wa kilimo aliepo karibu nae ili kujua kiasi cha mbolea anacho paswa kuweka kwenye mimea yake shambani)



3. Mbolea za kupandia

Mimea ya jamii ya nafaka hufanya vizuri zaidi kama itapandwa kwa kutumia mbolea ya NPK au DAP kwa kuweka gramu tano za mbolea husika katika shimo, vilevile mimia ya jamii ya mikunde na mboga mboga hufanya vizuri ikiwa itapandwa kwa kutumia mbolea ya NPK kama inapatikana.



4. Mbolea za kukuzia

Mahindi yaliyofikia ukubwa wa kukuzia. Kuna aina nyingi ya mbolea za kukuzia mazoa, mkulima anashauriwa kuwa anatunza kumbukumbu ya taarifa zake za shamba hii itamsaidia kujua huduma sahihi ya kuipatia mimea yake.



Kwa mfano kama mkulima alipanda mazao yake kwa kutumia aina Fulani ya mbolea mfano TSP au DAP mkulima anatakiwa kuwa na kumbukumbu hii itamsaidia mshauri wa kilimo kuweza kufanya kazi kwa urahisi zaidi, pia itaepusha kutoa ushauri unaohusu kutumia pembejeo mkulima alizo tumia mwanzo.



Kama mkulima alipanda kwa kutumia mbolea inayotoa kirububisho kimoja tuu kwenye mimea mfano UREA au TSP wakati wa kuweka mbolea ya kukuzia mkulima anashauriwa kuweke mbolea itakayo ipatia mimea virutubisho zaidi ya kimoja mfano NPK au CAN kwakua virutubisho vinavyo itajika kwenye mimea hufanya kazi tofauti hivyo mkulima anatakiwa kulizingatia sana hili.



Muonekano wa mbolea ya UREA

Pia kama mkulima kama alipanda kwa kutumia mbolea ya samadi wakati wa kupandia anapaswa kutumia mbolea inayotoa kirutubisho kimoja mfanyo UREA hii ni kwa sababu samadi ya wanyama ina virutubisho vingi ambavyo vinahitajika katika ukuaji wa mimea shambani. Lakini mkulima anaweza kutumia mbolea zinazo ongeza virutubisho zaidi ya kimoja mfano CAN na NPK kwa mavuno bora .



Mazao ya jamii ya nafaka hufanya vyema kama yatakuziwa kwa kutumia mbolea ya NPK, vilevile mimeaya mbogambopa na matunda hufanya vizuri kama itakuzwa kwa kutumia NPK au CAN. Kwa mimea ambayo hutoa matunda CAN inafaa zaidi kwa kua CAN hifanya matunda kua makubwa na mazuri



Mbolea za Viwandani

Mbolea za viwandani zimegawanyika katika makundi makuu matatu, nayo ni mbolea za chumvichumvi, chokaa na kijivu,



5. Mgawaniko/makundi ya mbolea za viwandani

(a) Mbolea za Chumvichumvi

Mbolea hizi hujulikana kama mbolea za kukuzia na huwekwa shambani baada ya mimea kuota.

Zina virutubisho vingi vya Naitrojeni ambavyo huifanya mimea kukua haraka.

Zinahusika na utengenezaji wa kijani kibichi kwenye mmea.

Mbolea za chumvichumvi zinazotumika zaidi Nchini Tanzania ni:-

– Sulphate of Ammonia (S/A)

– Calcium Ammonium Nitrate (CAN)

– Urea.

– Mbolea ya mchanganyiko N.P.K.



(b) Mbolea za Chokaa:

Hizi ni mbolea zinazotumika kupandia mbegu au miche.

Husaidia uotaji mzuri wa mimea, huimarisha mizizi, na hutumika katika utengenezaji wa chakula na mbegu kwenye tunda.



Huhusika na usafirishaji wa nguvu kwenye mmea na hufanya mazao kukomaa haraka.

Mbolea hizi huwekwa shambani wakati wa kupanda.

Aina ya mbolea za chokaa zinazotumika hapa nchini ni Triple Super Phosphate (TSP). Vilevile unaweza kutumia N.P.K kwa kupandia.



(c) Mbolea za Kijivu (Potashi):

Potashi ni kirutubisho kinachosaidia mimea katika utengenezaji wa protini na wanga.

Pia huhusika na utumiaji wa madini muhimu kwa maisha ya mimea.

Pia huwezesha matunda kukomaaa, kuiva haraka, na kutengeneza mbegu bora.




Husaidia ongezeko la maji kwenye mmea na kuufanya ustahimili magonjwa, ukame, baridi na hali ya udongo wenye alkalini nyingi.

Mbolea za Potashi zinazotumika ni:-

– Muriate of Potash (MoP)

– Sulphate of Potash (SP)

Monday, 3 July 2023

Fahamu virutubisho vitatu muhimu kwa mimea

 VIRUTUBISHO VITATU MUHIMU

Mmea hutumia virutubisho vikuu vitatu ambavyo huchukua nafasi kubwa katika maendeleo ya mmea. Virutbisho hivyo ni naitrojen (N), fosiforasi (P) na potasiamu (K).

Makala

Fahamu virutubisho vitatu muhimu kwa mimea


Mmea hutumia virutubisho vikuu vitatu ambavyo huchukua nafasi kubwa katika maendeleo ya mmea. Virutbisho hivyo ni naitrojen (N), fosiforasi (P) na potasiamu (K).


MIMea hupata chakula kutoka kwenye udongo. Chakula hicho huitwa virutubisho kwa mmea ambavyo kitaalamu vipo 16, vikiwamo 13 vinavyopatikana kwenye udongo.


Mmea hutumia virutubisho vikuu vitatu ambavyo huchukua nafasi kubwa katika maendeleo ya mmea. Virutbisho hivyo ni naitrojen (N), fosiforasi (P) na potasiamu (K).


Kwa kifupi wengi huita virutubisho hivi kwa kifupi cha N-P-K. Na kila mbolea huandaliwa na kuwekewa asilimia tofauti tofauti ya virutubisho vikuu hivi

Kwa mfano, kuna NPK (17:17:17), CAN (27:0:0), DAP (18:46:0). Hizi ni aina tatu za mbolea zilizoundwa na virutubisho vikuu vitatu kwa mpangilio wa N:P:K na kiwango chake cha asilimia za virutubisho katika mabano.


Chukua mfano wa mbolea ya DAP hap juu. Fosiforasi ipo kwa kiasi kikubwa (46) naitrojeni (18) na potasiamu (0). Hii inamaanisha kuwa hapa fosiforasi ina mahitaji makubwa kuliko virutubisho vingine.


Ndiyo maana wataalamu tunasema udongo una mengi ambayo kama mkulima atayajua na kuyafanyia kazi, ana nafasi kubwa ya kufurahia kilimo.


Hakuna asiyejua kuwa udongo ni muhimu kwa maisha endelevu ya mwanadamu, lakini tayari sehemu kubwa ya bara la Afrika, ikiwamo Kusini mwa jangwa la Sahara kuna tatizo la rutuba ndogo ya udongo.

Tunaposema rutuba ndogo ya udongo ni upatikanaji mdogo wa virutubisho vitatu vya N-P-K vya mmea katika udongo.


Swali; wakulima wafanyeje kuboresha rutuba ya udongo na hatimaye waweze kupata matunda ya shughuli zao za kilimo?


Umuhimu wa Fosiforasi


Mimea hupata virutubisho muhimu kwa ajili ya ukuaji kupitia udongo. Mizizi ya mimea hunyonya maji yaliyoko kwenye udongo yakiwa na virutubisho hivi.


Fosiforasi huchukuliwa na mimea ikiwa tu iko katika hali ya kuyeyuka katika maji yaliyopo kwenye udongo.Kama ilivyo Nitrojeni, fosiforasi pia ni muhimu kwa ukuaji na ustawi wa mazao.Majukumu yake ni pamoja na kusaidia ukuaji wa mizizi, kuharakisha kukomaa kwa mazao (kuchanua, uzaaji wa matunda na mbegu).


Mengine ni kuimarisha ubora wa mazao (hasa mazao ya mboga mboga) na kutengeneza nitrojeni iliyoko hewani kuwa katika hali ambayo inaweza kutumiwa na mimea hasa ile ya aina ya mikunde.


Lini Fosiforasi inahitajika?


Fosiforasi na hata virutubisho vingine hupotea udongoni kwa sababu mbalimbali.


Hivyo, kuna haja ya mkulima kujua muda mwafaka wa kurudisha virutubisho hivyo na njia maalumu zitakazotumika kurudisha virutubisho hivyo.


Kitaalamu, virutubisho hivi vitatu huongezwa udongoni kwa mbolea asili kama samadi au mbolea za dukani kama UREA, DAP na nyinginezo. Lakini pia kuoza kwa majani katika udongo huongeza virutubisho udongoni

Inasikitisha kumuona mkulima mara anapomaliza kuvuna, badala ya kuacha masalio yaoze, anayachoma moto. Hajui kuwa kuchoma moto ni kuondoa virutubisho.


Kiasi cha fosiforasi kinachotakiwa kwa ukuaji mzuri wa mimea kinategemea aina na umri wa mmea. Upungufu wa virutubisho vya fosiforasi hutokea wakati mimea inapokuwa midogo au wakati mizizi bado midogo.


Mmea mdogo unapokuwa haupati fosiforasi ya kutosha, uwezo wake wa kukua utaathiriwa. Hapa ndipo mmea unapodumaa, majani kuwa ya njano au maua kuanguka.


Kwa hiyo ukuaji mzuri wa mizizi ni muhimu ili kuwa na mwanzo mzuri wa ukuaji wa mmea. Mmea mdogo unahitaji fosiforasi kwa wingi wakati unapoanza kukua, kiasi kingine unapoendelea kukua na kiasi kingine kitasaidia wakati wa kuzaa matunda na mbegu

Unawekaje mbolea?


Unaposafisha shamba lako, hakikisha udongo unauchanganya na mbole. Na hata unapoandaa mashimo maalumu weka tena mbolea huku ukimwagilia kwa siku mbili hadi tatu asubuhi na jioni kabla ya kupanda mche.


Kwa kufanya hivi, utajihakikishia upatikanaji wa virutubisho muhimu ikiwamo fosiforasi ambayo ni muhimu katika maisha ya mbegu yako kuelekea kuwa mmea wenye afya.


Mbegu ikishaota, utahitajika kuweka mbolea, wakati wa kukua utaweka mbolea lakini pia wakati wa kutoa maua pia utaweka mbolea.


Kuna aina ya mazao yanayohitaji fosiforasi kwa wingi. Mazao haya ni kama vile mahindi, kabichi, viazi, maharage, na aina nyingine za mikunde.

Pia, kuna mimea mingine yenye uwezo mkubwa wa kutafuta na kuchukua fosiforasi katika udongo. Mimea hii ni kama sukuma wiki, mbaazi na alizeti mwitu.


Vitu vinavyopunguza virutubisho kwenye udongo


Kuna vitu vya aina mbili ambavyo huondoa au kupunguza rutuba ya udongo au kupunguza virutubisho muhimu udongoni.


Vitu vya asili


Mojawapo ya vitu hivi ni mvua ambayo hufanya virutubisho muhimu viende chini zaidi. Lakini pia joto kali na michakato ya kikemia ambayo hutokea katika miamba.


Udongo wa kichanga pia huwa na virutubisho kidogo, kutokana na uwezo wake mdogo wa kuhifadhi maji.


Kazi za binadamu


Upungufu wa fosiforasi katika udongo pia husababishwa na kazi za binadamu na jinsi wanavyohudumia mashamba yao.


Kwa mfano, kulima mazao mengi kwa mfululizo na kuvuna huondoa fosiforasi kwenye udongo. Uhudumiaji mbaya wa mashamba kama vile kuchoma mabaki ya mazao shambani, kutoongeza mboji katika udongo na kulima kunakosababisha mmomonyoko wa udongo vinachangia kupungua kwa fosiforasi katika udongo. Shughuli zote hizi hufanya udongo katika mashamba uchoke.


Saturday, 1 July 2023

Pili pili kichaa

email Shafii.ismail09@gmail.com 

WhatsApp /call 0683308173 

Website http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

PILIPILI KICHAA 

 Pilipili kichaa kutoka katika bara la Afrika maarufu kama ‘African Bird’s Eye Chilli’ ndizo zinazoonekana kupendelewa zaidi katika anga za kimataifa.


Pilipili kichaa ni zao lililoanza kushika kasi ya mauzo na kufanya vizuri sokoni miongoni mwa mazao ya biashara katika soko la dunia.


Pilipili kichaa kutoka katika bara la Afrika maarufu kama ‘African Bird’s Eye Chilli’ ndizo zinazoonekana kupendelewa zaidi katika anga za kimataifa.


Cha ajabu ni kwamba wakulima wengi wa Tanzania hawajachangamkia fursa hiyo adhimu ambayo kwa sasa imefunguka zaidi barani Ulaya.

Matumizi ya zao hili


Ingawa wengi hutumia pilipili kama kiungo kwenye chakula, yapo matumizi mengine ya zao hilo ikiwa ni pamoja na kutumika kama mojawapo ya malighafi ya kutengenezea dawa za kuchua misuli na dawa nyingine za hospitali.


Pilipili hutumika pia kama malighafi katika kutengeneza bidhaa za viwandani.


Unga unga unaotokana na pilipili kichaa unatumika katika utengenezaji wa mabomu ya machozi.


Lingoda anasema zao hilo pia ni malighafi katika rangi za midomo maarufu kama lipstick.


Faida za pilipili kichaa kwa afya ya binadamu


Pilipili kichaa ni zao lenye wingi wa vitamini A na limebarikiwa pia kuwa na virutubisho vya vitamini B, vitamini E, vitamini C, Riboflavin, Potassium na Manganese.


Virutubisho hivyo vyote vina manufaa katika mwili wa mwanadamu na ndiyo sababu ulaji wa pilipili hizi unatajwa kuwa na faida kiafya.


Ndani ya mwili wa binadamu zinafanya kazi ya kusafisha damu, kutoa sumu , kusisimua mzunguko wa damu na kuweka sawa uwiano wa tindikali(acid)mwilini.


Pilipili kichaa pia husaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua na kukufanya upumue kwa urahisi.


Aidha, mlaji wa pilipili kichaa anajiondolea uwezekano wa kupatwa na saratani ya utumbo.


Kilimo cha pilipili kichaa


Zao hili lina sifa kubwa ya kuvumilia hali yoyote ya hewa ikiwamo ukame, joto na mvua za kiasi kati ya mililimita 600 hadi 1200 kwa mwaka.


Pamoja na sifa hiyo, mkulima unapaswa kuwa makini ukame unapozidi sana unasababisha kuanguka kwa maua hivyo ni muhimu kunyunyuzia maji.


Pilipili huhitaji joto la kiasi cha nyuzi 20 hadi 30 na udongo tifutifu wenye kiwango cha tindikali yaani Ph 6.0 hadi 6.5.


Zao hili linapaswa kuoteshwa kwanza kwenye vitalu kabla ya kuipeleka shambani. Tengeneza vitalu vya upana wa mita moja.


Tumia mbolea ya kinyesi cha ng’ombe au mboji


Weka mistari ya mbegu upana wa sentimita 10 kwa kila mstari hadi mstari.


Baada ya kuweka mbegu weka udongo kiasi na weka nyasi kutunza unyevu nyevu na mwagilia maji mara kwa mara.


Mbegu zikiota toa nyasi na nyunyizia dawa ya kuua wadudu, iache iendelee kukua hadi kufikia unene wa sentimita 2-3 kwa urefu sentimita 8-10 ndipo uipeleke shambani.


Ndani ya miezi mitatu zikiwa shambani pilipili zitakuwa zimebadilika rangi na kuwa nyekundu hapo zinakuwa tayari kwa ajili ya kuvunwa na huvunwa mfululizo kwa miezi mitatu hadi minne.


Inashauriwa uvunaji huu ufanyike kila baada ya wiki mbili na haitakiwi kuvunwa pamoja na vikonyo vyake.


Changamoto


Lingodo anasema pamoja na mafanikio makubwa yanayotokana na kilimo hicho, uwepo wa wadudu waharibifu ni kikwazo kikubwa kwao.


Anasema kuna wadudu wadogo wadogo ambao ni nadra kuonekana kwa macho, wao hufanya kazi ya kuharibu maua ambayo yanategemewa kuzalisha pilipili.


Utitiri ni changamoto nyingine pamoja na uwepo wa wadudu wanaoshambulia mizizi.


Kukabiliana na changamoto hizo mkulima anashauriwa kupalilia mapema kukabiliana na na maficho ya wadudu ambao wanaonekana kwa macho.


Mkulima anashauriwa kabla ya kujitosa kwenye kilimo hiki awe na uhakika wa soko, hivyo ni muhimu kuingia mkataba wa makubaliano ili mazao yakitoka shambani moja kwa moja yaende sokoni.

Njia za kuondoa magadi.

 Email Shafii.ismail09@gmail.com 


WhatsApp /call 0683308173 


Website http://www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com


FAHAMU NJIA NZURI YA KUONDOA MAGADI(SALTS) SHAMBANI



Katika mashamba mengi tatizo la udongo na ardhi kwa ujumla kujaa chumvi au magadi limekuwa tatizo kubwa kwa wakulima wengi kwani magadi au chumvi huleta madhara makubwa sana kwa mazao na hata mazao mengine hufa kabisa pale yanapooteshwa kwenye udongo wenye magadi mfano wa mashamba yalioadhirika ni Ndungu irrigation scheme,kitivo irrigation scheme, Dakawa,Kiroka na Mkindo irrigation scheme (Morogoro), Kinyasugwe scheme (Dodoma) pia baadhi ya maeneo ya Lower moshi,Mawala,Kikavu chini, na hivyo kufanya mashamba yalio na tatizo hilo yasitumike katika uzalishaji,makala hii itakusaidia kujua namna ya kurudisha ardhi ya shamba lako katika hali nzuri na kuzuia uwezekano wa magadi kuongezeka katika shamba lako na hii itaongeza uzalishaji kwani utaweza kuotesha mazao mengi na ya aina mbalimbali kama udongo wako utakuwa na hali nzuri ya kuupatia mmea wako maji na madini or (nutrients) za kuuwezesha kukua vizuri na kuzaa sana




AINA ZA MAGADI ZILIZOPO KWENYE UDONGO


Kuna aina nyingi za chumvichumvi zilizopo ardhini na huwa katika viwango tofauti kulingana eneo moja na lingine na tofauti hii husababishwa na asili ya udongo wa mahali husika chumvi hizi ni kama Sodium ambayo hupatikana kwenye chumvi ya kawaida(NaCl), Potasium, Boron,Magnesium, Calcium, Phosphorous madini mengine ni muhimu katika ukuaji wa mmea lakini kwa kiwango kinachotakiwa na huwa ni sumu endapo yatazidi kiwango chake




NAMNA AMBAVYO MAGADI HUDHOOFISHA MIMEA


Madhara yatokanayo ma magadi ni makubwa sana na huleta hasara kwa wakulima wengi sana, kitaalamu magadi huzuia mizizi ya mimea kufyonza maji kwenye udongo na kuufanya mmea kushindwa kukua kwani maji ni muhimu katika mfumo wa mimea kujitengenezea chakula chake hata kama utamwagilia maji ya kutosha katika shamba lenye magadi bado mimea haitaweza kupata maji hayo (salts induce water stress to crops through matrix forces build up between the soil particles and the salts ion and hinder plant water uptake via capillarity and osmosis). Pia magadi huharibu mfumo wa udongo(soil structure) na kuufanya udongo kuwa mgumu na kuzuia mizizi ya mmea kupenya vizuri kwenye ardhi na hivyo kupunguza udhabiti wa mimea iwapo shambani na kusababisha kuanguka angauka kwa mazao yanapofikia wakati wa kubeba matunda au maua kwani hukosa nguvu za kujishikilia kwenye ardhi na hali hii husababishwa sana uwepo na sodium nyingi shambani na mkulima hupata hasara kubwa sana.




VYANZO VYA MAGADI KWENYE UDONGO


Asili ya udongo wenyewe


Baadhi ya maeneo yana udongo wenye asili ya chumvi kwa Tanzania maeneo hayo yanapatikana kwa wingi dodoma na singida na hasa wakati wa kiangazi baada ya mvua kukatika unaweza ukaona kabsa mabonge ya chumvi ardhini




Maji yanatumika kwa umwagiliaji


Kuna baadhi ya maeneo maji yake huwa na chumvi kiasi kwenye mito na hapa chemichemi na wakulima hutumia maji kutoka kwenye vyanzo hivyo vyenye maji ya chumvi katika kumwagilia mashammba yao, hii huongeza chumvi kidogo kidogo kwenye ardhi na kama mwendelezo wa kutumia maji hayo utafanyika kwa miaka mitano basi shamba hilo litakuwa limejaa chumvi na halitafaa tena kwa kilimo endapo njia na mbinu stahiki hazitachukuliwa




Utumiaji wa mbolea za viwandani bila maelekezo ya kitaalamu


Tujue ya kuwa sio kila mbolea ya kiwandani inafaa kwenye kila aina ya udongo, pili tunapokuwa tunaweka mbolea shambani lazima tuwatumie wataalamu ili watupe vipimo sahihi vya uwekaji wa mbolea hizi ili ziwe kwa kiwango kinachotakiwa pasipo kuzidisha wala kupunguza , kila shamba lina rutuba tofauti na lingine kwa hiyo ata uwekaji wa mbolea utatofautiana, pia kila zao lila vipimo vyake vya kiasi cha mbolea kinachotakiwa, kumbuka ni muhimu kufuata ushauri wa wataalamu kabla ya kuweka mbolea shambani ili kuondokana na matatizo na uweze kuzalisha mazao yenye tija




Mfumo mbaya wa utoaji maji shambani(poor drainage system)


Tatizo hili ni kubwa sana hasa pale wakulima wengi wanapoamini kuwa katika kumwagilia shamba lazima aone maji yametuama ndio aridhike kuwa amemwagilia, hili ni kosa kubwa kwani tunatakiwa tujue kuwa mimea hufyonza maji yaliyo ardhini tuu(plants absorb water, and they don't drink water ......... Myth), maji yaliyotuama shambani hupandisha chumvi iliyopo chini kuja juu na baada ya ardhi kukauka chumvi ile hubakia juu ya ardhi na kuadhiri mimea


NJIA ZA KUONDOA MAGADI SHAMBANI


Hili ndilo lengo kuu la makala hii ili kumsaidia mkulima kuondokana na tatizo hili, nitaeleza njia za kitaalumu na za gharama nafuu za kuondoa na kupunguza magadi shambani.




Kuzamisha chumvi(Leaching of salts)


Wakati wa kumwagilia shamba unashauriwa umwagilie maji mengi kiasi kuliko yale yanayotosheleza mmea wako ili maji hayo ya ziada yasaidia katika kuzamisha chumvi iliyoko juu wa udongo iende chini zaidi ambako mizizi ya mimea haifiki, njia hii lazima utumie wataalamu wa umwagiliaji (irrigation engineers) kama mimi ambao tutakusaidia kitaalamu kuendena na udongo wako na tutakuambia ni kiasi gani cha maji inatakiwa umwagilie katika shamba lako ili kuondoa chumvi na kusaidia mimea yako kukua (irrigation and leaching requirements)






2. Uwekaji wa Gypsum (Calcium Sulfate)




Gypsum hufanya kitu kinachoitwa neutralization ambapo hubadilisha chumvi iliyopo ardhini isilete madhara kwa mimea na katika maduka mengi ya pembejeo zinauzwa hizi gypsum kwa ajili ya mashamba ili kudhibiti chumvi na magadi lakini njia hii ni ya gharama kidogo




3. Utumiaji wa Samadi




Mbolea za wanyama na mimea husaidia sana kwenye kuongeza rutuba kwenye ardhi pia katika kuhakikisha na kupungiuza magadi kwenye udongo na njia hii matokeo yake ni polepole lakini ina uhakika na pia samadi ina faida nyingine nyingi katika kuimarisha udongo na kuongeza upatikanaji wa madini kwa mimea






4.Njia ya mafuriko (flooding)




Njia hii hufanywa katika maeneo yenye maji mengi na hasa kipindicha mvua , shamba lenye magadi hutifuliwa na kufurishwa au kumwagiliwa mpka maji yanatuama (wakati hamna mazao shambani) na baada ya hapo maji hutolewa kwa mifereji maalumu na maji hayo huchukua magadi katika shamba husika




NB. njia hii usiifanye kwenye mashamba yaliosongamana ili maji yaliyo na magadi yasiende kwenye shamba la jirani yako na kumpa hasara




5. Utumiaji wa njia za kisasa za kufanya umwagiliaji kama drip irrigation,sprinkler system hupunguza uwepo wa magadi kwenye udongo na kama unahitaji system hizi nitafute kwa mawasiliano mwishoni mwa makala hii




Lakini kwa maeneo ambayo yana magadi sana unashauriwa kupanda mazao yanayoshahimili ardhi yenye chumvi




mazao yanayoshahimili chumvi zabibu,mbaazi,Nanasi,Miembe hasa mazao ya miti ndio hushauriwa sana katika ardhi yenye magadi






mazao yasiostahimili udongo wenye magadi


Mahindi,Tikiti maji,Nyanya, Mbogamboga, na mengne mengi