Saturday, 20 January 2024

Kilimo Cha spinach

 

Spinachi ni moja kati ya mazao ya mbogamboga inayo limwa sana nchini Tanzania na asili yake ni china na ndo maaana huwa tunaiita chinese na badae jina hili likasambaa katika nchi mbalimbali ikiwemo na Tanzania.

Mboga hii huwa haina msimu, hivyo mkulima anaweza kulima muda wowote ambao anataka, na hii itategemea upatikanaji wa maji wa maji kwa wingi. Kwani mboga hii huhitaji maji kwa wingi katika hatua za awali.

Hali ya hewa inaoyofaa kwa kilimo hiki ni.
Jotolidi; Chinese au  linastawi na kukua vizuri kwenye maeneo yenye jotolidi 18 °c hadi 27° c.

Unyevunyevu
Chinese  ni zao linalo tegemea umwagiliaji kama ambavyo nimekwisha eleza hapo awali hivyo linaitaji maji mengi wakati wa ukuaji.

Udongo.
chinese cabbage linakua vizuri kwenye udongo wa kichanga na wenye unyevunyevu wa kutosha PH; 5.5 hadi 7.6

Namna ya kuandaa shamba.
Udongo unatakiwa utifuliwe vizuri kabla ya kupanda unaweza kutumia jembe la mkono au machaku na chisel na andaa shamba wiki 6 kabla ya kupanda.

Uandaaji wa kitalu.
Kitalu kinatakiwa kiwe na upana wa mita 1 yani sentimita 100 na urefu wa mita 5 yani sentimita 500. Kitalu kitifuliwe vizuri na kiwe na kingo ili kuzuia maji kutoka nje ya kitalu. kisha panda mbegu kwenye kitalu kwa sm 15 hadi 20 mstari hadi msitari na panda mbegu sm 2 kati ya mbegu na mbegu na fukia sm 1 hadi 2.

Kupanda
Kwa kupanda moja kwa moja chimba udongo sm 2 hadi 3 kwa kutumia jembe la mkono na panda nafasi ya 30 mstari hadi mstari na 30 mbegu hadi mbegu na fukia sm1 hadi 2.
Na kwakupandikiza hamisha miche inapo fikia urefu was sm 5 na chagua miche yenye afya na isiwe na magonjwa.

Mbolea.
Kama unatumia mbolea ya ng’ombe, kuku na nguruwe tumia ndoo katika kila kitalu chenye mita 5
Na pia weka mbolea ya kukuzia UREA gram 50 kwa kila kitalu chenye mita 5 pale mmea unapofikia majani matano.

Palizi
Tumia jembe la mkono kupalilia magugu pale yanapo jitokeza.

Magonjwa na wadudu waharibifu
Pale utakapohisi majani ya mboga hizi yameanza kubadikika, ikiwa ni ishara ya kushambuliwa na wadudu, tafadhari unashauriwa uweze kutumia chemical za kuua wadudu kama vile ninja, supercorn, wilcron na perfecron na pia hakikisha kila wakati unakumbuka kuondoa  magugu pamoja na mimea yenye wadudu na pia weka shamba safi wakati wote.

Lakini kama utatokea ugonjwa wa Kuoza kwa mizizi unachotakiwa kufanya kuondoa mazao yaliyo athilika na ugonjwa huo.

Kuvuna
Chinese ukomaa baada ya miezi 2 hadi 4 inategemea na aina mbegu uliyopanda, au muda mwingine hutegemea na hali ya hewa pia.

CONTACT
Whatsapp/call 0683308173
Mawasiliano...
Whatsapp/call 0683308173
EMAIL. shafii.ismail09@gmail.com
website. Http//www.kilimoniuhai.blogspot.com

Saturday, 6 January 2024

 Jinsi ya kutengeneza kiuadudu cha asili kwa kutumia mbegu za mti wa mwarobaini

  


Okoa fedha na linda afya za walaji kwa kutumia viuadudu vya asili kudhibiti wadudu shambani kwako.


Fuata hatua zifuatazo kutengeneza kiuadudu kwa kutumia mbegu za mti wa mwarobaini.


 Kwanza tafuta mwarobaini wenye matunda ambayo yana rangi ya kijani na manjano na kisha vuna matunda yenye rangi ya majano hayo ndiyo matunda yaliyokomaa au kuiva.


 Vuna matunda hayo na yaanike kwenye jua kwa takriban siku 3 hadi 4 ili yakauke.


 Hakikisha matunda yanageuka na kuwa na rangi ya kahawia.


 Ponda ponda hayo matunda ili kutenganisha ganda la juu na mbegu bila kuvunja mbegu ya ndani.


 Kisha pepeta ili kutenganisha maganda na mbegu au kiini cha ndani.


 Baada ya hapo chambua mbegu nzuri na zilizokomaa unashauriwa kuchagua zile zenye rangi nyeusi zinafaa zaidi zile zenye rangi nyeupe unashauriwa kuziacha.


 Weka mbegu ulizo chagua kwenye chombo kisha ziponde mpaka ziwe unga mlaini


 Chukua unga wako na changanya na maji safi.


 Uwiano mzuri wa uchanganyaji ni gramu 350 za unga wa mbegu za mwarobaini kwa lita 10 za maji safi.


 Acha mchanganyiko utulie kwa masaa 24 kabla ya kutumika.


 Chuja mchanganyiko huo kuondoa chembe ndogo zinazoweza kuziba Kichujio cha kinyunyizi au solo


 Baada ya hapo kiuadudu chako kitakua tayari kwa matumizi.


 Kinyunyizi chenye ujazo wa lita 15 kinapaswa kitumike kwenye eneo la takribani mita za mraba 400


Mawasiliano...

Whatsapp/call 0683308173

EMAIL. shafii.ismail09@gmail.com

website. Http//www.kilimoniuhai.blogspot.com

Thursday, 4 January 2024

Tatizo la nyanya kujikunja majani

 Wakulima wengi wamekuwa wakisumbuka saana huhusiana na Tatizo hili. Na mara nyingi tumekuwa tukipigiwa simu kuulizwa tu kuhusiana na tatizo hili.


Hivyo ili kusaidia wakulima wote nchini; makala hii ambayo ni elimishi na yakitaalamu itafafanuwa kiufupi kuhusiana na tatizo hili na kubainisha namna ya kukabiliana nalo.


Habari Mpendwa msomaji wa makàla zetu za kilimo ni uhai tuko hapa kupeana elimu ya kilimo kwa ujumla

Mara nyingi kujikunja kwa majani ya mmea wa nyanya (kujikunja kuelekea juu au chini) husababishwa na Hali ya mazingira, kemikali, wadudu na magonjwa.

KUJIKUNJA KUNAKOSABABISHWA NA HALI YA KIMAZINGIRA.
Hii ni hutokea mara nyingi saana kwenye zao la nyanya na pilipili Hoho; husababishwa na Joto kali na umwagiliaji usio yakinifu.
Mkulima hapaswi kutishika/kupata hofu kutokana na hali hii kwasababu haidhuru wala kuathiri mavuno.
Hali hii Huendelea kwa siku kadhaa na hukoma mara tu Hali ya hewa inapokaa sawa.
Mmea hukunja majani yake (Leaf roll) ili kupunguza uso wa majani (leaf surface) kukabiliana na hali ya upungufu wa maji.

USHAURIMkulima ahakikishe anamwagilia maji ya kutosha na kulainisha udongo ili maji yafike kwenye mizizi yote.

Kujikunja kunakosababishwa na mazingira ya joto au upungufu wa maji 

Kujikunja kunakosababishwa na mazingira ya Joto au upungufu wa maji

KUJIKUNJA KUNAKOSABABISHWA NA WADUDU NA MAGONJWA.

Uwepo wa wadudu waharibifu wanaofyonza kwenye majani kama vile kimamba, Vithiripi na vipepeo weupe, husababisha kueneza magonjwa ya virusi.
Magonjwa ya virusi hayana tiba Mara yanapoingia na yanaathiri mavuno kwa kiwango kikubwa.

Majani yalioathiriwa na virusi kujikunja kwake ni tofauti na kujikunja kwa majani kulikosababishwa na mazingira. 
Kujikunja kwake huambatana na uvimbe uvimbe mdogo mdogo kwenye majani (leaf curling)
Pia kwenye Ugonjwa wa batobato (Tomato mosaic Virus) mishipa ya jani la Nyanya (leaf veins) kwa chini huwa na rangi ya zambarau (purple) kwa mbali.

Ugonjwa mwengine wa virusi (Tomato yellow leaf curl virus- TYLV) ambao huwa na dalili ya uwepo wa rangi ya umanjano kwenye majani.

Tomato yellow leaf curl virus 

Tomato mosaic virus
KUKABILIANA NA TATIZO HILI:
Dhibiti wadudu wasumbufu na waharibifu kwa kutumia viuatilifu sahihi mara tu ugunduapo uwepo wao.
Tumia Dudumectin, Duduacelamectin, Snowthunder, au liberate kuwadhibiti wadudu waharibifu
.

Na tatizo hili sio kwa nyanya tu hukumba Hadi mazao mengine ,kama bamia,bilinganya, maharage,kunde. 

Mawasiliano
Whatsapp/call 0683308173
Whatsapp/call 0683308173
EMAIL. shafii.ismail09@gmail.com
website. Http//www.kilimoniuhai.blogspot.com

Monday, 1 January 2024

Kilimo Cha nyanya chungu. (Ngogwe)

 1603024592551.png


Hatua za kufuata ukitaka kulima nyanya chungu
Nyanya Chungu ni zao la Kitropic linalotoa mazao yake kama matunda au kama mboga. Rangi ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano, au njano-nyupe. Kuna aina mbalimbali za nyanya chungu ambazo ni ni nyanya chungu za asili na zingine ni chotara siyo chungu kama za asili.

Mazingira
Zao hili hustawi vizuri maeneo yenye baridi ya wastani na joto la wastani kuanzia nyuzi joto 25°C hadi 35°C, hupendelea udongo tifu tifu usiotwamisha maji na wenye rutuba. Kama utaweza kutumia mbolea za samadi na mboji au mbolea za asili pamoja , basi nyanya chungu hustawi vizuri sana.

Kuandaa shamba
Mbegu za nyanya chungu huandaliwa kwenye kitalu kwanza kabla ya kupelekwa shambani.

Maelekezo ya kuandaa kitalu cha nyanya chungu.
- Chagua eneo la kuanzisha kitalu kwenye maeneo yanayopatikana maji kwa urahisi.
- Inua udongo wa kitalu hadi kufikia kimo cha sm 20 na upana wa mita 1 na urefu wowote. Bonda bonda mabonge makubwa ya udongo ili kupata udongo laini.

- Weka mbolea ya asili iliyooza vizuri, changanya ndoo moja kubwa ya lita 20 ya mbolea hiyo kwa eneo la mita 1 kwa mita 1 (1 m2). Kwa hiyo kama tuta lako la kitalu lina urefu wa mita 5 na upana mita 1, utaweka ndoo 5 za mbolea za asili.

- Kama ni wakati wa kiangazi, mwagilia tuta lako kwa siku 3 mfululizo mpaka udongo uloane vizuri.

Kusia mbegu
Maelekezo ya namna ya kusia mbegu kwa usahihi
- Tengeneza vimifereji vyenye kina cha sm 2 kukatisha tuta, nafasi kati kimfereji kimoja na kingine ni sm 15 au nusu rula.

- Sia mbegu zako ndani ya vimifereji hivyo, halafu funika na udongo laini.
- Weka matandazo ya nyasi juu ya tuta ili kuzuia jua kali na matone ya maji ya moja kwa moja.
- Mwagilia maji kitalu chako juu ya nyasi asubuhi na jioni kila siku. Ila inashauriwa kumwagilia kitalu chako maji wakati wa jioni.

- Mbegu za nyanya chungu huota baada ya siku 10 hadi 14 tangu kusia. Baada ya mbegu kuota toa matandazo ya nyasi halafu yaweke matandazo hayo katikati ya mistari ya miche.
- Tengeneza kivuli cha matandazo ya nyasi juu ya kitalu chenye kimo cha mita moja, kivuli hicho cha nyasi lazima kiwe kinapitisha mwanga wa jua walau kidogo ili kuruhusu mwanga kuifikia miche.

Kupandikiza miche shambani
Miche huwa tayari kuhamishiwa shambani baada ya mwezi mmoja hadi mwezi mmoja na nusu tangu mbegu kuota. Nafasi ya kupandikiza nyanya chungu ni mita 1 kwa mita 1 (yaani mita 1 shina hadi shina na mita 1 mstari hadi mstari)

Kabla ya kupandikiza miche chimba mashimo yenye ukubwa kiasi, weka samadi iliyooza vizuri kiasi cha mkono mmoja uliojaa, halafu fukia udongo kiasi. Baada ya kufukia udongo pandikiza mche wako, kila shimo mche mmoja. Kama ni kipindi cha kiangazi pandikiza wakati wa jioni, baada ya kupandikiza mwagili maji vizuri.

Kutunza shamba
Mimea jamii ya mbogamboga ikiwemo nyanya chungu haipendi bugudha ya magugu shambani, kwa hiyo hakikisha unafanya palizi wakati wote kuakikisha magugu hayaathiri ustawi wa mmea.
Dhibiti magonjwa na wadudu mabalimbali wanaoathiri zao hili, kwa kutumia madawa mabalimbali na matumizi ya mbolea mbalimbali za kurutubisha mimea pale inapobidi na iwe ya kilimo hai.
KUVUNA

Nyanya chungu huwa tayari kuvunwa ndani ya siku 90 hadi 120 tangu kupandikiza. nyanya chungu inaweza kuvunwa mara 1 au mara 2 kwa wiki. Matunda ya nyanya chungu yanatakiwa kuvunwa kabla hayajabadilika rangi kutoka nyeupe kwenda njano mpauko.

matunda haya ya nyanya chungu yanaweza kusindikwa kuwa unga. Ili kusindika nyanya chungu kuwa unga fwata hatua zifuatazo;

- Chagua nyanya chungu bora na zioshe kwenye maji
- Kata kata nyanya chungu hizo kutengeneza vipande vidogo dogo, halafu tandaza vipande hivyo kwenye mkeka au turubai safi

- Anika vipande hivyo vya nyanya chungu juani hadi vikauke.
- Baada ya vipande hivyo kukauka vizuri, visage kwa kutumia kinu au mashine ya mkono mpaka viwe unga.

- Tunza unga huo kwenye chombo kisafi ambacho hakingizi hewa.
- Unaweza kutumia unga huo kwenye maharage, karanga, nyama na mboga zingine, mboga iliyowekwa unga huu wa nyanya chungu inakua tamu mno na inakua na virutubisho vya kutosha

Email address shafii.ismail09@gmail.com
Whatsapp/call 0683308173