Saturday, 20 January 2024

Kilimo Cha spinach

 

Spinachi ni moja kati ya mazao ya mbogamboga inayo limwa sana nchini Tanzania na asili yake ni china na ndo maaana huwa tunaiita chinese na badae jina hili likasambaa katika nchi mbalimbali ikiwemo na Tanzania.

Mboga hii huwa haina msimu, hivyo mkulima anaweza kulima muda wowote ambao anataka, na hii itategemea upatikanaji wa maji wa maji kwa wingi. Kwani mboga hii huhitaji maji kwa wingi katika hatua za awali.

Hali ya hewa inaoyofaa kwa kilimo hiki ni.
Jotolidi; Chinese au  linastawi na kukua vizuri kwenye maeneo yenye jotolidi 18 °c hadi 27° c.

Unyevunyevu
Chinese  ni zao linalo tegemea umwagiliaji kama ambavyo nimekwisha eleza hapo awali hivyo linaitaji maji mengi wakati wa ukuaji.

Udongo.
chinese cabbage linakua vizuri kwenye udongo wa kichanga na wenye unyevunyevu wa kutosha PH; 5.5 hadi 7.6

Namna ya kuandaa shamba.
Udongo unatakiwa utifuliwe vizuri kabla ya kupanda unaweza kutumia jembe la mkono au machaku na chisel na andaa shamba wiki 6 kabla ya kupanda.

Uandaaji wa kitalu.
Kitalu kinatakiwa kiwe na upana wa mita 1 yani sentimita 100 na urefu wa mita 5 yani sentimita 500. Kitalu kitifuliwe vizuri na kiwe na kingo ili kuzuia maji kutoka nje ya kitalu. kisha panda mbegu kwenye kitalu kwa sm 15 hadi 20 mstari hadi msitari na panda mbegu sm 2 kati ya mbegu na mbegu na fukia sm 1 hadi 2.

Kupanda
Kwa kupanda moja kwa moja chimba udongo sm 2 hadi 3 kwa kutumia jembe la mkono na panda nafasi ya 30 mstari hadi mstari na 30 mbegu hadi mbegu na fukia sm1 hadi 2.
Na kwakupandikiza hamisha miche inapo fikia urefu was sm 5 na chagua miche yenye afya na isiwe na magonjwa.

Mbolea.
Kama unatumia mbolea ya ng’ombe, kuku na nguruwe tumia ndoo katika kila kitalu chenye mita 5
Na pia weka mbolea ya kukuzia UREA gram 50 kwa kila kitalu chenye mita 5 pale mmea unapofikia majani matano.

Palizi
Tumia jembe la mkono kupalilia magugu pale yanapo jitokeza.

Magonjwa na wadudu waharibifu
Pale utakapohisi majani ya mboga hizi yameanza kubadikika, ikiwa ni ishara ya kushambuliwa na wadudu, tafadhari unashauriwa uweze kutumia chemical za kuua wadudu kama vile ninja, supercorn, wilcron na perfecron na pia hakikisha kila wakati unakumbuka kuondoa  magugu pamoja na mimea yenye wadudu na pia weka shamba safi wakati wote.

Lakini kama utatokea ugonjwa wa Kuoza kwa mizizi unachotakiwa kufanya kuondoa mazao yaliyo athilika na ugonjwa huo.

Kuvuna
Chinese ukomaa baada ya miezi 2 hadi 4 inategemea na aina mbegu uliyopanda, au muda mwingine hutegemea na hali ya hewa pia.

CONTACT
Whatsapp/call 0683308173
Mawasiliano...
Whatsapp/call 0683308173
EMAIL. shafii.ismail09@gmail.com
website. Http//www.kilimoniuhai.blogspot.com

Saturday, 6 January 2024

 Jinsi ya kutengeneza kiuadudu cha asili kwa kutumia mbegu za mti wa mwarobaini

  


Okoa fedha na linda afya za walaji kwa kutumia viuadudu vya asili kudhibiti wadudu shambani kwako.


Fuata hatua zifuatazo kutengeneza kiuadudu kwa kutumia mbegu za mti wa mwarobaini.


 Kwanza tafuta mwarobaini wenye matunda ambayo yana rangi ya kijani na manjano na kisha vuna matunda yenye rangi ya majano hayo ndiyo matunda yaliyokomaa au kuiva.


 Vuna matunda hayo na yaanike kwenye jua kwa takriban siku 3 hadi 4 ili yakauke.


 Hakikisha matunda yanageuka na kuwa na rangi ya kahawia.


 Ponda ponda hayo matunda ili kutenganisha ganda la juu na mbegu bila kuvunja mbegu ya ndani.


 Kisha pepeta ili kutenganisha maganda na mbegu au kiini cha ndani.


 Baada ya hapo chambua mbegu nzuri na zilizokomaa unashauriwa kuchagua zile zenye rangi nyeusi zinafaa zaidi zile zenye rangi nyeupe unashauriwa kuziacha.


 Weka mbegu ulizo chagua kwenye chombo kisha ziponde mpaka ziwe unga mlaini


 Chukua unga wako na changanya na maji safi.


 Uwiano mzuri wa uchanganyaji ni gramu 350 za unga wa mbegu za mwarobaini kwa lita 10 za maji safi.


 Acha mchanganyiko utulie kwa masaa 24 kabla ya kutumika.


 Chuja mchanganyiko huo kuondoa chembe ndogo zinazoweza kuziba Kichujio cha kinyunyizi au solo


 Baada ya hapo kiuadudu chako kitakua tayari kwa matumizi.


 Kinyunyizi chenye ujazo wa lita 15 kinapaswa kitumike kwenye eneo la takribani mita za mraba 400


Mawasiliano...

Whatsapp/call 0683308173

EMAIL. shafii.ismail09@gmail.com

website. Http//www.kilimoniuhai.blogspot.com

Thursday, 4 January 2024

Tatizo la nyanya kujikunja majani

 Wakulima wengi wamekuwa wakisumbuka saana huhusiana na Tatizo hili. Na mara nyingi tumekuwa tukipigiwa simu kuulizwa tu kuhusiana na tatizo hili.


Hivyo ili kusaidia wakulima wote nchini; makala hii ambayo ni elimishi na yakitaalamu itafafanuwa kiufupi kuhusiana na tatizo hili na kubainisha namna ya kukabiliana nalo.


Habari Mpendwa msomaji wa makàla zetu za kilimo ni uhai tuko hapa kupeana elimu ya kilimo kwa ujumla

Mara nyingi kujikunja kwa majani ya mmea wa nyanya (kujikunja kuelekea juu au chini) husababishwa na Hali ya mazingira, kemikali, wadudu na magonjwa.

KUJIKUNJA KUNAKOSABABISHWA NA HALI YA KIMAZINGIRA.
Hii ni hutokea mara nyingi saana kwenye zao la nyanya na pilipili Hoho; husababishwa na Joto kali na umwagiliaji usio yakinifu.
Mkulima hapaswi kutishika/kupata hofu kutokana na hali hii kwasababu haidhuru wala kuathiri mavuno.
Hali hii Huendelea kwa siku kadhaa na hukoma mara tu Hali ya hewa inapokaa sawa.
Mmea hukunja majani yake (Leaf roll) ili kupunguza uso wa majani (leaf surface) kukabiliana na hali ya upungufu wa maji.

USHAURIMkulima ahakikishe anamwagilia maji ya kutosha na kulainisha udongo ili maji yafike kwenye mizizi yote.

Kujikunja kunakosababishwa na mazingira ya joto au upungufu wa maji 

Kujikunja kunakosababishwa na mazingira ya Joto au upungufu wa maji

KUJIKUNJA KUNAKOSABABISHWA NA WADUDU NA MAGONJWA.

Uwepo wa wadudu waharibifu wanaofyonza kwenye majani kama vile kimamba, Vithiripi na vipepeo weupe, husababisha kueneza magonjwa ya virusi.
Magonjwa ya virusi hayana tiba Mara yanapoingia na yanaathiri mavuno kwa kiwango kikubwa.

Majani yalioathiriwa na virusi kujikunja kwake ni tofauti na kujikunja kwa majani kulikosababishwa na mazingira. 
Kujikunja kwake huambatana na uvimbe uvimbe mdogo mdogo kwenye majani (leaf curling)
Pia kwenye Ugonjwa wa batobato (Tomato mosaic Virus) mishipa ya jani la Nyanya (leaf veins) kwa chini huwa na rangi ya zambarau (purple) kwa mbali.

Ugonjwa mwengine wa virusi (Tomato yellow leaf curl virus- TYLV) ambao huwa na dalili ya uwepo wa rangi ya umanjano kwenye majani.

Tomato yellow leaf curl virus 

Tomato mosaic virus
KUKABILIANA NA TATIZO HILI:
Dhibiti wadudu wasumbufu na waharibifu kwa kutumia viuatilifu sahihi mara tu ugunduapo uwepo wao.
Tumia Dudumectin, Duduacelamectin, Snowthunder, au liberate kuwadhibiti wadudu waharibifu
.

Na tatizo hili sio kwa nyanya tu hukumba Hadi mazao mengine ,kama bamia,bilinganya, maharage,kunde. 

Mawasiliano
Whatsapp/call 0683308173
Whatsapp/call 0683308173
EMAIL. shafii.ismail09@gmail.com
website. Http//www.kilimoniuhai.blogspot.com

Monday, 1 January 2024

Kilimo Cha nyanya chungu. (Ngogwe)

 1603024592551.png


Hatua za kufuata ukitaka kulima nyanya chungu
Nyanya Chungu ni zao la Kitropic linalotoa mazao yake kama matunda au kama mboga. Rangi ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano, au njano-nyupe. Kuna aina mbalimbali za nyanya chungu ambazo ni ni nyanya chungu za asili na zingine ni chotara siyo chungu kama za asili.

Mazingira
Zao hili hustawi vizuri maeneo yenye baridi ya wastani na joto la wastani kuanzia nyuzi joto 25°C hadi 35°C, hupendelea udongo tifu tifu usiotwamisha maji na wenye rutuba. Kama utaweza kutumia mbolea za samadi na mboji au mbolea za asili pamoja , basi nyanya chungu hustawi vizuri sana.

Kuandaa shamba
Mbegu za nyanya chungu huandaliwa kwenye kitalu kwanza kabla ya kupelekwa shambani.

Maelekezo ya kuandaa kitalu cha nyanya chungu.
- Chagua eneo la kuanzisha kitalu kwenye maeneo yanayopatikana maji kwa urahisi.
- Inua udongo wa kitalu hadi kufikia kimo cha sm 20 na upana wa mita 1 na urefu wowote. Bonda bonda mabonge makubwa ya udongo ili kupata udongo laini.

- Weka mbolea ya asili iliyooza vizuri, changanya ndoo moja kubwa ya lita 20 ya mbolea hiyo kwa eneo la mita 1 kwa mita 1 (1 m2). Kwa hiyo kama tuta lako la kitalu lina urefu wa mita 5 na upana mita 1, utaweka ndoo 5 za mbolea za asili.

- Kama ni wakati wa kiangazi, mwagilia tuta lako kwa siku 3 mfululizo mpaka udongo uloane vizuri.

Kusia mbegu
Maelekezo ya namna ya kusia mbegu kwa usahihi
- Tengeneza vimifereji vyenye kina cha sm 2 kukatisha tuta, nafasi kati kimfereji kimoja na kingine ni sm 15 au nusu rula.

- Sia mbegu zako ndani ya vimifereji hivyo, halafu funika na udongo laini.
- Weka matandazo ya nyasi juu ya tuta ili kuzuia jua kali na matone ya maji ya moja kwa moja.
- Mwagilia maji kitalu chako juu ya nyasi asubuhi na jioni kila siku. Ila inashauriwa kumwagilia kitalu chako maji wakati wa jioni.

- Mbegu za nyanya chungu huota baada ya siku 10 hadi 14 tangu kusia. Baada ya mbegu kuota toa matandazo ya nyasi halafu yaweke matandazo hayo katikati ya mistari ya miche.
- Tengeneza kivuli cha matandazo ya nyasi juu ya kitalu chenye kimo cha mita moja, kivuli hicho cha nyasi lazima kiwe kinapitisha mwanga wa jua walau kidogo ili kuruhusu mwanga kuifikia miche.

Kupandikiza miche shambani
Miche huwa tayari kuhamishiwa shambani baada ya mwezi mmoja hadi mwezi mmoja na nusu tangu mbegu kuota. Nafasi ya kupandikiza nyanya chungu ni mita 1 kwa mita 1 (yaani mita 1 shina hadi shina na mita 1 mstari hadi mstari)

Kabla ya kupandikiza miche chimba mashimo yenye ukubwa kiasi, weka samadi iliyooza vizuri kiasi cha mkono mmoja uliojaa, halafu fukia udongo kiasi. Baada ya kufukia udongo pandikiza mche wako, kila shimo mche mmoja. Kama ni kipindi cha kiangazi pandikiza wakati wa jioni, baada ya kupandikiza mwagili maji vizuri.

Kutunza shamba
Mimea jamii ya mbogamboga ikiwemo nyanya chungu haipendi bugudha ya magugu shambani, kwa hiyo hakikisha unafanya palizi wakati wote kuakikisha magugu hayaathiri ustawi wa mmea.
Dhibiti magonjwa na wadudu mabalimbali wanaoathiri zao hili, kwa kutumia madawa mabalimbali na matumizi ya mbolea mbalimbali za kurutubisha mimea pale inapobidi na iwe ya kilimo hai.
KUVUNA

Nyanya chungu huwa tayari kuvunwa ndani ya siku 90 hadi 120 tangu kupandikiza. nyanya chungu inaweza kuvunwa mara 1 au mara 2 kwa wiki. Matunda ya nyanya chungu yanatakiwa kuvunwa kabla hayajabadilika rangi kutoka nyeupe kwenda njano mpauko.

matunda haya ya nyanya chungu yanaweza kusindikwa kuwa unga. Ili kusindika nyanya chungu kuwa unga fwata hatua zifuatazo;

- Chagua nyanya chungu bora na zioshe kwenye maji
- Kata kata nyanya chungu hizo kutengeneza vipande vidogo dogo, halafu tandaza vipande hivyo kwenye mkeka au turubai safi

- Anika vipande hivyo vya nyanya chungu juani hadi vikauke.
- Baada ya vipande hivyo kukauka vizuri, visage kwa kutumia kinu au mashine ya mkono mpaka viwe unga.

- Tunza unga huo kwenye chombo kisafi ambacho hakingizi hewa.
- Unaweza kutumia unga huo kwenye maharage, karanga, nyama na mboga zingine, mboga iliyowekwa unga huu wa nyanya chungu inakua tamu mno na inakua na virutubisho vya kutosha

Email address shafii.ismail09@gmail.com
Whatsapp/call 0683308173


Saturday, 30 December 2023

Kilimo Cha mtama

 


Mtama ni kundi la mbegu ndogo aina ya mazao ya nafaka au nafaka ambayo kwa jina la kisayansi unajulikana kama (Sorghum bicolor), ni mazao yanayolimwa sana duniani kote kwa ajili ya chakula na lishe Mtama hutoa mazao mengi hata kwenye hali ambayo haifai kwa kilimo cha aina nyingine za mazao ya nafaka. Mtama una uwezo mkubwa wa kustahimili ukame.

Mtama unaweza kutumika kwa kuchemshwa na kuliwa kama ulivyo, kusagwa na kutumika kwa uji, kutengenezea vinywaji kama vile bia, kuoka mikate, na aina nyinginezo za vitafunwa. Mmea wa mtama pia hutumika kwa ajili ya malisho ya mifugo kama vile hay  na sileji. Mtama unastawis vizuri kwenye mazingira yenye wastani wa milimita 400 – 700 za mvua kwa mwaka. Pia mtama unavumilia sehemu zinazotuhamisha maji, na unaweza kulimwa sehemu zenye mvua nyingi.

Mtaama unafaa pia kwa sehemu kame zenye wastani wa joto la chini kiasi cha nyuzi joto 18°C, ili kuweza kuota vizuri, na kiasi cha nyuzi joto 25-30°C ili kukua vizuri. Mtama hauwezi kuvumilia barafu. Mtama unaweza kukua kwenye aina zote za udongo. Kwa kiasi kikubwa unafaa zaidi kwenye udongo wa mfinyanzi, lakini pia kwenye udongo ambao una kiasi kidogo cha mchanganyiko wa kichanga. Mtama unaweza kuvumilia uchachu kwenye udongo kuanzia pH 5.0-8.5, na inavumilia udongo wenye chumvi kuliko yalivyo mahindi.

Aina za mtama
Kwa jumla kuna aina zaidi ya 30 za mtama zinazolimwa kama chakula. Mtama hustawi vizuri kwenye joto ikivumilia pia ukame. Hivyo ni nafaka muhimi kwenye maeneo yabisi za Afrika. Katika miaka ya nyuma kilimo chake kiliachwa mara nyingi kwa ajili ya mahindi kwa sababu mahindi huleta mazao makubwa zaidi kwa ekari. Lakini wakati wa ukame mahindi ni hasara na watu hurudi-rudi kwenye kilimo cha mtama.

Aina za mtama zinatofautiana kulingana na rangi zake, kuna nyeupe, nyekundu, na kahawia. Mbegu za asili huwa zinachavushwa kwa urahisi zaidi lakini mavuno yake huwa ni hafifu ukilinganisha na mbegu za kisasa. Hata hivyo, aina za kisasa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi zinapopandwa kwa kufuata kanuni za kilimo bora.

Serena:  Ina punje za kahawia. Aina hii hustawi kwenye eneo lenye mvua za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii huwa na shina na mizizi imara, ambapo huweza kuzalisha kiasi cha kilo 3,000 kwa hekari moja. Ambapo zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.

Seredo:  Hii ni aina nyingine yenye punje za kahawia, na inapendekezwa Kulimwa kwenye eneo lenye mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari. Aina hii huchanua baada ya siku 71 na hukomaa katika kipindi cha siku 120. Aina hii huwa ni ndefu, na ina uwezo wa kuzalisha kilo 5000 kwa hekari moja. Ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa milia, kutu, mabaka kwenye majani, na madoa ya kahawia kwenye majani.

Gadam: Inafanya vizuri katika sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano Kenya, aina hii ya mtama hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii huvumilia bungo na ugonjwa wa majani.

Hakika na Wahi:  Hizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga kwa ajili ya kuoteshwa kwenye mashamba yalioathiriwa na viduha. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa aina zote mbili zinafaa sana kwa kupika ugali.

Utayarishaji wa shamba na kupanda
Kwa kawaida mtama hupandwa kwa kutumia mbegu. Mbegu hupandwa shambani moja kwa moja baada ya shamba kuandaliwa, lakini pia zinaweza kurushwa shambani, kasha zikavurugwa pamoja na udongo. Unapaswa kutayarisha shamba la kupanda mtama, iwe ni kwa ajili ya malisho au chakula kabla mvua za msimu hazijaanza. Zao hili hufanya vizuri zaidi kwenye udongo ulio laini. Linaweza pia kupandwa kwenye udongo ambao haukulimwa vizuri na bado ukaota vizuri.

Nafasi:  Mtama unaopandwa kwa ajili ya malisho, unaweza kupandwa kwa nafasi ya sentimita 75×10. Aina za mtama ambazo zinalengwa kwa ajili ya lishe kwa binadamu na wanyama, zinahitaji nafasi kiasi cha sentimita 60×20. Nafasi hutoa mwanya wa kuwa na kiwango kikubwa cha malisho. Mkulima anaweza kupanda mbegu za mtama kiasi cha kilo 2.4-3.3 kwa hekari moja. Ni mara chache sana mbegu hupandwa kwenye vitalu na kuhamishiwa shambani baadaye.

Kupanda:  Mtama hupandwa mvua zinapoanza kunyesha. Mbegu ni lazima zifukiwe ardhini usawa wa sentimita 3 kwenda chini, hii itasaidia kuepuka kuota wakati ambao si msimu kamili wa mvua. Pia zinaweza kufukiwa kiasi cha sentimita 2 wakati ardhi inapokuwa na unyevu. Mtama unahitaji rutuba ya hali ya juu wakati wa kupanda na wakati wa kuota. Ni vizuri kutumia samadi au mboji iliyooza vizuri wakati wa kuandaa shamba.

Mseto:  Unaweza kupanda mtama mseto na mazao jamii ya mikunde, na kuongeza mboji shambani mwako. Hii inaweza kuwa njia nzuri zaidi ya kupata virutubisho vinavyohitajika. Mseto wa mazao jamii ya mikunde inashauriwa iwe ni kama vile maharagwe, kunde, n.k

Uangalizi na utunzaji
Ni lazima kung’oa baadhi ya mimea inapokuwa na urefu wa sentimita 30, au siku 30 baada ya kupanda, ili kuwa na uhakika wa nafasi ya sentimita 10 kati ya mstari na mstari kwa mtama unaokusudiwa kwa ajili ya malisho, na nafasi ya sentimita 20 kati ya mstari kwa mtama uliokusudiwa kwa ajili ya chakula na lishe ya mifugo.

Palizi ya mkono ifanyike walau mara mbili. Shamba la mtama ni lazima liwekwe katika hali ya usafi na kutokuruhusu magugu wakati wote hasa katika kipindi cha mwanzoni.

Mawasiliano...
Whatsapp/call 0683308173
EMAIL. shafii.ismail09@gmail.com
website. Http//www.kilimoniuhai.blogspot.com

Tuesday, 22 August 2023

Kilimo cha minazi



Email shafii.ismail09@gmail.com 

WhatsApp /call 0683308173 

Website http//www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

 Minazi ni zao la biashara nchini Tanzania ambalo hulimwa na kustawi zaidi ukanda wa pwani ya Tanzania. Mikoa kama Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba, pia kwa uchache Minazi hulimwa kwenye mikoa ya Mbeya, Kigoma na Tabora.

Aina za minazi

Kuna aina kuu tatu za Minazi inayolimwa hapa Tanzania nayo ni (i) Minazi Mirefu ya asili (East African Tall) (ii) Minazi mifupi ya Kipemba (Malaysian Yellow Dwarf) (iii) Minazi Chotara (hybrid) inayotokana na kuunganisha chavua za Minazi mirefu na minazi mifupi ya Kipemba.

Upandaji

Ilikupata mazao yaliyo bora na mengi ni vema kuzingatia yafuatayo;

  • Kuchagua mbegu nzuri na kubwa kwa umbile yenye kuzaa sana.
  • Chagua eneo zuri la kupanda, eneo lenye udongo wa kichanga, pasipo na mwinuko na pasiwe na mwamba karibu wala udongo wa mfinyanzi.
  • Kupanda mapema kwa kuzingatia kalenda ya mvua kwa msimu, panda kwenye kipindi cha mvua za kwanza.

Kuandaa shamba

Ondoa visiki kwenye shamba jipya kwa kuving’oa na kuvirundika pembezoni mwa shamba.

  • Tibua shamba lote, pima shamba kwa ajili ya kuchimba mashimo.
  • Chimba mashimo kwa umbali wa mita 9 kwa mita 9 kwa minazi Mirefu na mita 7 kwa 7 kwa Minazi mifupi na chotara.
  • Andaa mashimo yenye kipimo cha sentimita 60 kwa 60.
  • Changanya udongo wa juu na samadi au mboji kisha rudishia shimoni. (Zingatia kuwa mbolea ya samadi ya ng’ombe isiyopoa si mzuri kwenye mashimo ya kupanda minazi kwani huvutia mazaliano ya mchwa).
  • Panda miche ya Minazi iliyooteshwa kitaluni kwako au kununua kwa mawakala au wakulima wanaootesha miche, chagua miche yenye umri wa kutosha yaani majani 5 na hii maana yeke mnazi utakuwa tayari una umri wa miezi 5, inaaminiwa kuwa mnazi unatoa majani (kuti moja) kila mwezi.

Palizi

Palizi kwenye zao la Minazi ni kitu muhimu sana cha kuzingatia. Palilia kwa kulima visahani kwa kipenyo cha mita 1 hadi 2 kutegemeana na umri wa mche/mti.

Palizi inasaidia mmea kutopata mashambulizi ya baadhi ya wadudu kama vile mchwa. Majani yakikauka ni kivutio kikubwa cha moto wa msituni, Mnazi mkubwa ukiungua moja ya madhara yake ni kukosekana na mavuno kwa mwaka husika. Mnazi ulioungua moto huchukua takribani mwaka mmoja ili kuanza kuzaa tena.

Uwekaji wa matandazo (mulch) kwenye Minazi kwa kutumia majani au nyasi kavu ni hatari kwa mashambulizi ya mchwa na pia ni mazalia ya wadudu Chonga wa Minazi.

Mazao mchanganyiko

Ili kupunguza gharama za palizi kwenye shamba la minazi inashauriwa kuwa ni vema apande mazao mchanganyiko jamii ya mikunde kama vile Kunde, Karanga, Njugu, Upupu na pia waweza kupanda Mahindi au Alizeti kwa miaka minne (4) ya mwanzo.

Mavuno

Minazi mirefu huanza kutoa mavuno mwaka wa 5 na 6 ambapo Minazi Mifupi na ile Chotara hutoa mavuno kuanzia mwaka wa 4 na 5. Kwa wastani Mnazi uliotunzwa vizuri hutoa Nazi kati ya 25 hadi 40 kwa mavuno ya mara moja na unatakiwa kuvuna baada  ya miezi Minne.

Kudhibiti wadudu na magonjwa

  • Magonjwa

Minazi haina magonjwa mengi ya kusumbua mmea, bali ugonjwa pekee wenye kuuwa Minazi ni ugonjwa wa Nyong’onyea, ambao kitaalamu hujulikana kama leathal disease. Ugonjwa huu ni wa hatari sana na hauna tiba, ugonjwa wa Nyong’onyea hushambulia minazi mikubwa kwa kuozesha sehemu ya mcha au kilele cha Mnazi na na kufa kabisa.

Dalili zake ni majani kuwa njano ikianza na majani machanga kisha kuenea majani yote, kubadilika rangi majani kutoka njano na kuwa kahawia na kisha kukauka na kudondosha chini sehemu ya juu, wakati huo mnazi unakuwa tayari umeshaathirika na kufa.

Ugonjwa huu ni wa kuambukiza kutoka Mnazi mmoja hadi mwingine kwa njia ya hewa, wadudu na wanyama, hakuna dawa iliyogundulika kudhibiti ugonjwa huo na njia mzuri ya kukinga ni usafi wa shamba na kuondoa kwa kuikata na kuichoma moto minazi yote itakayoonyesha dalili ya kuugua.

 Alama kubwa ya maeneo yaliyoshambuliwa na ugonjwa huo ni kuonekana kwa miti mingi ya minazi iliyokufa na kubaki kama nguzo za umeme au simu, baadhi ya maeneo ya vijiji vya wilaya ya Kilwa na Mafia unaweza kuona hali hiyo.

Wadudu waharibifu

  • Mchwa; Mchwa ni miongoni mwa wadudu waharibifu kwenye zao la Nazi. Mchwa huanza kushambulia nazi zikiwa kitaluni kwa kutafuna magubi ya nazi au ngozi ya nje na kuuwa mche, tumia dawa za kudhibiti mchwa na pia majivu yanasaidia sana. Mchwa pia hushambulia miche iliyopandwa shambani na kuweza kuua kabisa, mche mkubwa kuanzia miaka 4 haidhuriki na mdudu huyu.
  • Mdudu Faru wa minazi; Mdudu huyu ni mkubwa saizi ya kidole gumba cha mtu mzima, ana rangi ya kahawia au wekundu uliofifia, ana meno makali ya kutafuna majani ya mnazi pia umbile lake ni kuwa ana pembe iliyopinda kwa juu sawa na pembe ya mnyama Faru na kitaalamu anajulikana kama Rhinoceros beetle.
Mdudu Faru wa minazi (Rhinoceros beetle).

Mdudu huyu huzaliana kwenye mabiwi yaliyopo shambani, au kwenye miti na magogo yaliyokauka na yenye dalili ya kuoza.

Mdudu huyu hutaga mayai humo na mayai yakishaanguliwa wadudu wakubwa huruka na kutua kwenye minazi kwa ajili ya kupata chakula ambapo hushambulia kilele cha mche wa mnazi, hukitafuna na hatimaye mnazi waweza kufa kabisa.

Minazi ya umri wa kati waweza kuona dalili ambapo kuna lapu lapu za mnazi nchani zikiwa zimetolewa nje ya mti na makuti yakaliwa yatakuonesha alama ya mkato kama vile yamekatwa kwa mkasi. Wadudu hawa wana tabia ya kuruka nyakati za usiku kwa ajili ya kuzaliana (mating) na kuhama mnazi  mmoja hadi mwingine.

Thursday, 17 August 2023

Kilimo cha muhogo

Email shafii.ismail09@gmail.com 

WhatsApp /call 0683308173 

Website  http//www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com

Zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania, zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya mihogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k.


Umuhimu wa zao hili ni kutupatia chakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini mihogo ni chakula kikuu ambacho kinachuku asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya Lindi na Mtwara.  


Kwa siku za karibuni, muhogo unaongoza kwa kuongezeka katika umaarufu kuliko mazao yote ya chakula nchini. Watalaam wanazungumzia umaarufu wa muhogo kuwa ni (pamoja na mambo mengine) uwezo wake wa kustahamili hali ya hewa mbaya kama ukame na mvua zisizoaminika, kutoa mazao mengi kwa eneo na kustahamili mashambulizi ya magonjwa na wadudu.


Hata hivyo uzalishaji wa mihogo kwa eneo bado ni wa viwango vya chini mno. Zipo sababu nyingi zinazo sababisha kuwepo kwa hali hii kama vile:


Ukosefu wa mbegu bora za mihogo za kutosha 

Wakulima kuendelea kungangania mbegu zao za asili kuliko mbegu bora licha ya uzalishaji mdogo na kushambuliwa na magonjwa na wadudu.

Ukosefu wa masoko ya kuaminika ambayo yangeshawishi wakulima kulima mbegu za kisasa ambazo zimeandaliwa kibiashara. 

Wakulima wengi kutotumia teknolojia sahihi za usindikaji ambazo ni mbinu mbadala za hifadhi za asili. 

Kwa muda mrefu tatizo kubwa la zao la muhogo ni ukosefu wa teknolojia ambazo zina uwezo wa kuongeza thamani wa muhogo kama chakula chenye ubora kwa familia za mijini na vijijini.


Vikundi mbalimbali vya uzalishaji na usindikaji vimeundwa na muhogo umeanza kuthaminwa kwani unga wake unatumika kutengenezea vyakula kama maandazi, chapati, chichili, keki na vingenevyo vingi.


Ugali wa muhogo umeongezeka thamani kutokana na ubora wa unga uliosindikwa kwa kwa teknolojia ya kisasa.


Madhumuni ya http//www.kilimoniuhaiblog.blogspot.com  ni kutoa maelekezo juu kilimo bora cha zao la muhogo ili kusaidia wakulima kuinua viwango vya ubora na wingi wa mazao hivyo kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea kipato.


Fahamu Mambo Mawili Kabla Hujaanza Kilimo Biashara

Tambua Thamani Na Jinsi ya Kupanga Bei ya Mazao yako

Umuhimu na Matumizi ya Muhogo

Muhogo ama (kitaalam) Manihot esculentum, ni muhimu sana kwa Tanzania kutokana na sifa zake za kuvumilia ukame, kustawi kwenye maeneo yenye rutuba kidogo hivyo kuhitaji gharama ndogo za uzalishaji. Kwa hali hiyo, zao hili hulimwa sana na wakulima wadogo walio wengi wenye kipato kidogo.

Kwa wakazi wa vijijini, muhogo huvunwa, kutolewa ganda la juu na kuanikwa hadi kukauka maarufu kama makopa. Kwa kawaida makopa hutwangwa kwenye kinu na kupata unga ambao hutumika kama uji au ugali. Makopa mara nyingi hutunwa ama kuhifadhiwa kwenye dari ya nyumba ambako hufukiziwa moshi wa moto ili yasipukuswe. 

Kutokana na hali hiyo, wakulima wengi hulima muhogo mchungu ambao haupukuswi kwa urahisi. Kwa vile muhogo mchungu una sumu nyingi aina ya cyanide, hufanya kiasi kidogo cha muhogo kiliwe kwa kutafuna ukiwa mbichi ama kupikwa kama futari. 

Kwa wakazi wa mijini, sehemu kubwa ya mihogo hutumika kama futari au kitafunwa kwa chai ama humenywa na kukaangwa kama chips maarufu kama chips dume. 

Kutokana na kuongezeka kwa teknolojia za usindikaji, unga wa muhogo hutumika kutengenezea biskuti, chapati,maandazi,chichili,keki na vyakula vingine vingi vinavyotengenezwa kwa kutumia unga wa ngano.

chipsi za muhogo

Chipsi za Mihogo

Mazingira na Aina za Mihogo

Mazingira yanayofaa

Muhogo ni zao la jamii ya mizizi. Hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye mwinuko wa mita 0 hadi 1500 toka usawa wa bahari. Zao hili hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa milimita 750 mpaka milimita 1200 kwa mwaka.


Muhogo hupendelea udongo wa kichanga usiotuamisha maji. Udongo wa kichanga husaidia mizizi kupenya kwa urahisi na kupevuka. Vile vile muhogo una sifa ya kuvumilia hali ya ukame wa muda mrefu.


Aina za Mihogo

Kuna zaidi ya aina 45 za mihogo zinajulikana nchini Tanzania. Zaidi ya asilimia 80 ya mihogo ni ya asili. Hivyo ni kusema wakulima wengi hawatumii mbegu bora.


Wakulima wengi pia hupendelea kulima mihogo michungu kwa sababu haishambuliwi sana na wadudu ama magonjwa shambani na makopa yake yanahifadhika kwa urahisi. Hata hivyo zaidi ya asilimia 70 ya mihogo yote inayolimwa Tanzania ni mihogo baridi.




Kuandaa shamba la Muhogo

Inashauriwa kuandaa shamba mapema kabla ya msimu wa mvua haujaanza. Zifuatazo ni hatua za msingi katika kuandaa shamba:


Kufyeka msitu au vichaka 

Kung’oa na kuchoma moto visiki 

kulima na kutengeneza matuta. 

Uchaguzi wa mbegu bora za mihogo

Mpaka sasa hivi kuna aina nyingi sana za mbegu bora za mihogo ambazo zimethibitishwa na tayari zinatumiwa na wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji. Bofya hapa uzifahamu mbegu hizo


Katika kuchagua mbegu inayofaa, pamoja na mambo mengine, zingatia yafuatayo:


Mbegu itokane na shina lililokomaa vizuri 

Isitokane na shina la muhogo ulioshambuliwa na magonjwa. 

Macho yake yasiwe yamekaribiana sana au kuachana sana

Upandaji wa Mihogo

Muda wa kupanda Mihogo

Kanda ya ziwa: December mpaka January mwishoni

Nyanda za juu Kusini: November mwanzoni na Kanda ya Mashariki: kuanzia October mpaka December

Urefu wa kipande cha shina cha muhogo

Baada ya kuchagua mbegu hatua inayofuata ni kukata shina lako la muhogo katika pingili ndogo ndogo tayari kwa kupanda. Inapendekezwa pingili ziwe na urefu wa sentimita 30.


Hata hivyo, urefu wa pingili utategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande. Inapendekezwa kipande kimoja kiwe na macho manne hadi sita.


Nafasi ya kupanda Muhogo

Nafasi ya kupanda kwa shamba linalokusudiwa liwe na muhogo mtupu ni mita moja toka shina hadi shina na mita moja kati ya mistari. Kwa shamba ambalo mkulima anakusudia kuchanganya mazao, inashauriwa nafasi ya kupanda iwe mita 2 hadi mita 4 (kwa kutegemea aina ya mazao yanayochanganywa) kati ya mistari na mita moja toka shina hadi shina.


Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:


Kulaza ardhini (Horizontal)

Kusimamisha wima (Vertical) na

Kuinamisha ( Inclined/Slunted)

Kudhibiti Magugu

Katika miezi minne ya mwanzo muhogo unahitaji kupata chakula cha kutosha na mahitaji mengine ya msingi ili uweze kukua na kujenga mizizi mikubwa na imara.  Hivyo inashauriwa kufanya palizi la kwanza mapema, angalau mwezi mmoja baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua za mwanzo kunyesha.


Kwa kawaida palizi hufanywa kwa kutumia jembe la mkono au dawa ya kuulia magugu. Njia nyingine ya kudhibiti magugu ni kupanda mimea yenye majani yanayotanda juu ya udongo.


Palizi kwa kawaida hufanywa kila inapoonekana kwamba magugu yameota kiasi cha kuathiri ustawi wa muhogo, hivyo unaweza kupalilia mara 3 au 4 zaidi baada ya palizi ya kwanza hadi muhogo kukomaa.


Kuchanganya mazao kwenye shamba la mihogo

Utafiti unaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 80 ya mashamba ya muhogo Tanzania yanachanganywa na mazao mengine. Sababu kubwa zinazotolewa kuhusiana na hali ni kwamba wakulima wanafaidika kwa kupata mavuno ya ziada kama kunde, karanga, mahindi, maharage, korosho ama njugu.


Kwa kuchanganya mazao, mkulima, licha ya kuimarisha uhakika na usalama wa chakula, anaweza kuuza mazao mchanganyiko na kujiongezea kipato. Vile vile mazao ya jamii ya mikunde yanasaidia kuongeza rutuba ya udongo.


Hata hivyo, mazao mchanganyiko ni budi yasilete ushindani na muhogo katika kujipatia chakula, hewa, mwanga, unyevu na mahitaji mengine ya mmea yanayoweza kuathiri ustawi wa muhogo.


Inashauriwa pia kuzingatia muda wa kupanda, yaani muhogo upandwe mvua za kwanza ili mazao mchanganyiko yasiweze kuzidi na kuutawala muhogo.


Jinsi ya kudhibiti Wadudu na Magonjwa

Kilimo cha Viazi mviringo na Faida zake kwa Wakulima Tanzania

Mbolea vunde [Mboji]: Jinsi ya kutengeneza, matumizi na faida zake

Kanuni 12 za kilimo bora chenye tija Tanzania

Uvunaji wa Muhogo

Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua. Mihogo hutoa mavuno ya tani 19 hadi 30 kwa hekta kutegemeana na aina ya mbegu (variety) iliyopandwa.


Uvunaji wa muhogo

Uvunaji wa Muhogo

Usindikaji bora wa Muhogo

Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu tatu:


Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji 

Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo 

Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe. 

Njia bora za usindikaji Muhogo

Kwa kutumia mashine aina ya Grater 

Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.


Kwa kutumia mashine aina ya chipper 

Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.


Matumizi ya Muhogo

Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga 

Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k. 

Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.